Leo Sikukuu ya Mashujaa: Mtwa Abdallah Mkwawa wa Kalenga (1855 - 1898)

Leo Sikukuu ya Mashujaa: Mtwa Abdallah Mkwawa wa Kalenga (1855 - 1898)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
LEO SIKUKUU YA MASHUJAA: MTWA ABDALLAH MKWAWA WA KALENGA (1855 - 1898)

Makala hiyo hapo chini ni nyongeza ya makala fupi ilyoandikwa na kijana mmoja kumuadhimisha Mtwa Mkwawa.

Makala hii ndiyo iliyonishawishi kunyanyua kalamu:

Bismillah...

Naomba niongeze taarifa kidogo katika historia ya Mtwa Mkwawa mambo muhimu lakini ajabu hayaelezwi.

Sababu yake bado sijaifahamu.

Kwanza ni kuwa jina la Mkwawa alilichagua baada ya kusilimu na kuwa Muislam ni Abdallah na aliyemsilimisha pale Kalenga ni Abushiri bin Salim Al Harith.

Katika mapambano yake akiongoza majeshi ya Wahehe Mtwa Abdallah Mkwawa alikuwa akitumia bunduki aliyopewa na nduguye na rafiki yake Abushiri bin Salim.

Bunduki hii ipo hadi leo Mkwawa Museum pale Kalenga.

Kutoka na bunduki hii Mtwa Abdallah Mkwawa kupitia mafundi wake waliotengeneza bunduki nyingine wakitumia chuma kilichokuwa kinapatikana Kalenga.

Mkwawa alikuwa anajua kusoma na kuandika na barua zake zipo zimeandikwa kwa herufi za Kiarabu mtu akifika Mkwawa Museum ataweza kuziona na kuzisoma.

Tuje kwa Wissman.

Katika jeshi la Wissman kulikuwa na Wazulu 400 kutoka Kijiji cha Kwa Lukunyi, Inhambane, Mozambique alikokwenda kutia mkataba wa kupata askari kuja German Ostaafrika kupigana na majeshi ya wananchi waliokuwa wanapinga utawala wa Wajerumani adui mkubwa akiwa Bushiri wa Pangani.

Wissman alitia mkataba huu na Chief Mohosh Shangaan na ndiye alikuwa Kiongozi wa jeshi hili lililopiga kambi yake Pangani.

Katika jeshi hili alikuwa Sykes Mbuwane babu yake Abdulwahid Kleist Sykes.

Huyu Sykes Mbuwane ndiye baba yake Kleist Sykes aliyezaliwa hapo Pangani mwaka wa 1894 mama yake mwanamke wa Kinyaturu jina lake Kwema.

Kwema kitukuu yuko ameolewa Zanzibar jina lake kamili ni Kwema Ali Kleist Abdallah Sykes Mbuwane.

Chief Mohosh Shangaan alipigana pembeni ya Wissman akiongoza jeshi la Wazulu Nzole, Bagamoyo ambako jeshi la Abushiri lilisambaratishwa na Bushiri alifanikiwa kujinusuru akakimbia akiwa hana silaha.

Sykes Mbuwane, Chakulan na Machakaomo walishiriki katika vita hivi.

Ukoo wa Machakaomo uko Dar es Salaam Mtaa wa Kipata (Sasa Mtaa wa Kleist Sykes).

Walipomshinda Abushiri na kumnyonga 1889 ndipo Wajerumani wakaenda Kalenga kupigana na Mtwa Abdallah Mkwawa aliyejiua 1898.

Wissman akaelekea Old Moshi kwa Mangi Meli na yeye wakamnyonga 1900.

Baada ya vita hivi Chief Mohosh Shangaan akafanywa kuwa Mkuu wa German Constabulary akiongoza jeshi hili lililokuwa na Wazulu kutoka Mozambique na Wanubi kutoka Sudan akabadili jina lake akawa anajulikana kama Affande Plantan.

Affande Plantan amefariki mwaka wa 1914 wakati wa Vita Vya Kwanza Vya Dunia na mwanae wa kuzaa Schneider Abdillah Plantan na mwanae wa kulea Kleist Sykes wakiwa Mwele Juu Tanga wakipigana ndani ya Jeshi la Kijerumani chini ya Kamanda von Lettow Vorbeck dhidi ya Waingereza.

Huyu Afande Plantan ndiye aliyewazaa Thomas Saudtz Plantain, Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan na hawa wote wamepigania uhuru wa Tanganyika kuanzia enzi za African Association 1929, Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 hadi TANU 1954.

Affande Plantan amezikwa makaburi ya Ilala jirani na Ilala Stadium sasa Karume Stadium.

1753472267358.jpeg

Chief Adam Abdul Mkwawa
 
Ali kibao shujaa ambaye hata hakuwa mwenye mda na CCM ya kujiogopa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom