Leo ninawiwa kuliongelea Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

Buffet

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
639
1,569
Naomba nichukuliwe tu kuwa mimi siyo mwanataaluma ya habari na mawasiliano.

Hili shirika letu naomba kukiri kuwa limeanza kufufuka, linajitahidi sana kuisemea serikali na jamii kupitia makala mbalimbali (kwa mawazo yangu hakuna chombo cha habari kinachorusha hewani makala nyingi nchini) za kiuchumi, kijamii na kisiasa japo katika siasa wanalalia sana upande wa chama tawala.

Hawana uwiano sawa wa kuvipa airtime vyama vingine kulinganisha na CCM.

Eneo lingine ambalo wamejitahidi ni upande wa online broadcasting. Hapa nawapa heko.

Toka tarehe 22 November mwaka jana nilitakiwa kuja Jerusalem kwa muda wa wiki 26, naomba niwe mkweli, TBC na JamiiForums ndio platforms zinazonipatia updates za yanayoendelea nyumbani Tanzania, heko kwao.

Naomba nitaje baadhi ya watu ambao katika kufuatilia kwangu nimeona wanaing'arisha TBC ya sasa:

1. Hosea Cheyo
- Huyu jamaa ana weledi sana katika kuripoti taarifa zinazoangukia kwenye anga zake, huyu nadhani anaripot kutokea Katavi nadhani. Taarifa zake huwa zimejikita sana kwenye kuwasemea watu wa chini. Mara chache sana kukuta karipoti taarifa yenye sura ya kumpa political mileage mwanasiasa.

2. Monica Lyampawe - Huyu mama mkongwe huripoti kutokea Morogoro, yupo toka enzi za TVT na RTD. Taarifa zake haziegemei upande wowote.

3. Chunga luza - Akisoma taarifa huyu jamaa utagundua kitu fulani cha ziada kwake.

4. Tuma Dandi - Huyu kaka huleta makala fulani hivi za kusisimua sana, huibua sana watu wenye uhitaji katika jamii hasa walemavu, ni Mwana habari ambaye huandaa makala zinazoweza kukuliza.

5. Florence Mavimbi, Paul Alfonce, Marin Hassan na Ashel Thomas wanajitahidi pia.

Wafuatao wajirekebishe kidogo tu kwa maoni yangu:

1. Elisha Elia - Akihoji mtu unaweza ukatabiri the next question hata kama hajauliza, anapoteza mvuto wa interview.
2. Yule mzee wa kipindi cha tunatekeleza (nimemsahau jina) anapoteza weledi kwenye kusifia kupita kiasi, ni kawaida kumsikia akisema ni kazi za Mh Jemedari Amiri Keshi Mkuu raia namba moja chuma kiongozi shupavu Dr John Pombe Joseph Magufuli, mvuto hupotea pia.

3. Grace Kingalame - Sijui awamu hii kawaje, nilikuwa namkubali sana before, ila huyu dada kumbe ni mjumbe wa NEC ya CCM akiwakilisha UWT kutokea Songwe (nakubali kusahihishwa).

Kuwa kada siyo shida, tatizo ni kushindwa kujificha mbele ya chombo cha umma, anafeli sana katika hili.

Hayo ni maoni yangu mimi buffet, hongera TBC kwa kukabidhi gawio la milioni 500, ni mwanzo mzuri, all the best.
 
Kuwa kada sio shida tatizo ni kushindwa kujificha mbele ya chombo cha umma, anafel sana katika hili.

Hayo ni maoni yangu mimi buffet, hongera TBC kwa kukabidhi gawio la milioni 500, ni mwanzo mzuri, all the best.
hongera mkuu kama bado unaujasiri wa Kuona TBC vip imesha kuwa HD na vip BADO vipind 90% ni kuunga juhudi za mkuu wa wanyonge
 
mng'ao wa picha bado sana,hawajafikia kiwango cha HD,vipindi vya kuunga juhudi havipo tena,wanazo makala nyingi sana za kuelimisha siku hizi,unaweza ukafuatilia TBC jtatu hadi jpili siku hizi,mpangilio na flow ya vipindi wana jitahd sana,tatizo wanalopaswa kulifanyia kazi ni wao kujua kuwa siyo chombo cha chama tawala,ni chombo cha umma,wakibalance ktk hilo watakuwa mbali kiuweledi
 
Sidhani kama kuna watu humu wanaangalia huo uchafu

Sent using Jamii Forums mobile app
unamaanisha nini kusema hivyo wakati mm ni mmoja wa wanaofuatilia TBC???unamaanisha mm siyo mtu au mm sipo jf???au wewe kutokufuatilia tbc ina maana wote hawafuatilii??mbona comment yako inajicontradict sana kamanda wangu??najua TBC wana matatizo yao lakin haimaanishi kuwa hawafuatiliwi,hata ww ulifuatlia ndo kwa mtazamo wako ukajua kuwa ni uchafu vinginevyo usingejua hilo,tuheshimiane kiongozi
 
Back
Top Bottom