Leo nimekutana na Kalikonji

Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
10,087
15,962
Well..kwasis watoto wa mujini kuna watu tumewabatiza majina kutokana na maisha yao kiujumla
Mfano kuna

1. Chawa--huyu ni mtu ambaye hujiweka karibu, bega kwa bega na mtu fulani mwenye hali fulani nzuri kipesa. Yaani huyu anakufata fata muda mwingi kwa maslahi ya kumpa pesa inshort anakuganda

2. Kalikonji--sasa huyu ni advanced chawa. Yaani huyu hata funguo za gari za boss muda mwingne anakua nazo yeye. Yaani michepuko ya boss yote anaijua yeye na mipango yote anafanya yeye huyu hata wew kama ni mfanyakaz unafanya kaz kwa boss. Huyu kalikonji anauwezo wa kumwambia boss akufute kaz na akakufuta kazi.

Huyu yuko radhi kupoteza maisha yake kwa ajili ya boss wake.mara nying wanakuaga hawajaenda shule wala hawana maisha mazur.

Huyu ndo mpambe nuksi ukisikia.

Popote alipo boss na huyu yupo akisafiri Boss na huyu yupo hana kazi maalumu.

Sasa leo nimefika mahala fulani nikapak gar nikashuka..wakat naondoka nkaskia et hapo hamna parking.nkasema kwann.et kwanza hujasalimia bla bla.nkasema kwahyo hyo ndo sabab nikamuuliza hili eneo ni lako et hapana ni la mtu. Nikamuuliza kwahiyo wewe ndio huyo mtu? Je, we ni mlinzi? Yaani eneo lenyewe ni barabarani kabisa na magari kibao yamepaki. Baada ya mabishano sana nkaona isiwe tab nkatoa gar..wakatokea vijana wa bodaboda wakasem bro achana nae huyo kalikonji..skuwaelewa..ikabid niulize

Uzi tayari.
 
Hawa wapo, wanatumika sana na wahindi na waarabu, kaajiriwa hana kazi inayoeleweka, umbeya, majungu, unafiki na kujipendekeza ndiyo job description.

Everyday is Saturday........................... :cool:
 
Hili neno nimeona mtu wa klabu fulani ya futiboli watu wanamwita hivyo. Katika kutafuta maana mtandaoni ndio nimeletwa huku.
 
Back
Top Bottom