Leo nimegoma kumpisha kwenye siti binti mjamzito

Ki ukweli hua siwezi kukaa Kwa Amani kama mjamzito au mwenye mtoto kasimama pembeni yangu.
Mtoa mada hicho ulichofanya hata si cha kujisifia kweli mwanaume mzima unajisifia Kwa kutokumpisha mjamzito

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kabinti kadogo tu lakini ndio kametundikwa mimba

Nikiwa kwenye siti ndani ya daladala, kakaanza kuniangalia kwa huruma Mara kakaropoka, kaka naomba unipishe nikae mimi mjamzito

Nikakaambia mtafute mwanamke mwenzako akupishe, kwani nyinyi wote mnajua kama kuna ugumu wa kusimama. Pindi unapokua mjamzito, mimi sikupishi

Wanawake wote wakajikausha kumpisha mwenzao ndio Safari ikaenda hivyo, alisimama mpaka mwisho wa safari

NB: Wanawake mkishindwa kusaidiana nyinyi kwa nyinyi. Mimi nitaendelea na katabia haka aka
Sent using Jamii Forums mobile app
Usichoke kutenda mema kaka, ukitenda mema unajitendea mwenyewe and vice also versa is true.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimemuelewa mtoa mada..Ujauzito si kigezo cha kutoa kauli za kulazimisha.
Mtu ajifunze kuomba apewe msaada..maana hujui naye aliekaa kwenye siti ana changamoto zipi..alafu ni kabinti kadogo ( yawezekana kalistahili kuwa shule ila kamependa ngono..)
Kalitakiwa kapewe escort na Bwana yake..
Mwisho wanawake wasaidiane..
 
Wanamakusudi gari imejaa anapanda halafu anakuja kukusimamia karibu anakugusagusa na tumbo umpishe akimkuta mtu kauzu anajifanya kalala ;););)
 
Huyo binti yeye pia hakuwa mstarabu. Ilibidi yeye asimame tu na tumbo lake halafu aone kama watu wenye hekima hawatampisha kukaa kwenye siti.

ulichukua uamuzi sahihi ili iwe somo kwake na siku nyingine aache kuropoka hovyo.

NB: ukiwa na tatizo watu wanaona na wapo wenye busara watakuja kutoa msaada na sio lazima mtu ujionyeshe kuwa una shida.
 
Hapo ndo utajua tofauti kati ya wanaume wa Dar na wanaume wa mikoani uliona raha kukaa huku mama mjamzito amesimama unakuja kujisifu kabisa huku JF wewe ni mwehu
 
Back
Top Bottom