Leo ni siku ya tumbaku duniani

Leo ni siku ya tumbaku duniani

chaUkucha

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Posts
3,382
Reaction score
1,221
Leo ni siku ya kupiga marufuku matumizi ya tumbaku duniani.

Achana na tumbaku, kuboresha afya na mazingira bora uvute bange.
 
Leo ni siku ya kupiga marufuku matumizi ya tumbaku duniani.

Achana na tumbaku, kuboresha afya na mazingira bora uvute bange.

chaukucha tayari ulishalipuliza mkuu asubuhi hii. haya bana ila kumbukua hiyo tumbaki na sigara na pombe kodi zao ndio zinaongoza nchi
 
Tumbaku ni cancer stop smokin cigar

REAL_COHIBA_CUBAN_CIGARS.jpg
 
Tumbaku ni cancer

ila imetoa ajira kwa watu wengi kuanzia wakulima,madereva, wafanya kazi viwanda vya sigara, na wajasiriamali wenye maduka mtaani. toa chanzo mbadala cha ajira na kodi kubwa ambayo serikali inapata kutoka tcc
 
chaukucha tayari ulishalipuliza mkuu asubuhi hii. haya bana ila kumbukua hiyo tumbaki na sigara na pombe kodi zao ndio zinaongoza nchi

ni kweli usemacho ila watu wengi wanadhurika mvutaji na yule aliye karibu naye hata kama havuti.
 
Zimekuja sigara za ki electronic mnazijua nyie?

hizo ni sigara bandia sasa huu ndo ushuzi mwingine ukianza kuvuta hii ipo siku utavuta ile yenyewe ya ukweli alafu utasema unashindwa kuacha.
 
Mwili wa mtumiaji tumbaku
1. nywele kunyonyoka
2. mtoto wa jicho
3. kukunjamana kwa ngozi
4. kutokusikia vizuri
5. kansa (saratani ya ngozi)
6. meno kuoza
7. mapafu kushindwa kufanya kazi vizuri
8. ulaini wa mifupa
9. magonjwa ya moyo
10. vidonda vya tumbo
11. kubadilika rangi vidole
12. kansa ya kizazi na kuharibika kwa mimba
13. kupungua nguvu za kiume
14. ukurutu
15. kuziba kwa mishipa midogo ya damu
16. kansa ya mapafu na viungo vingine
 
sasa wanazuia tumbaku kivipi? mbona watu wakikutwa na madawa wanakamatwa, kwa nini watu wanaozalisha tumbaku au wanao process wakamatwe? nani asiyevijua viwanda vya sigara. hawa jamaa wasilete sanaa kama wanazuia au hawataki itumike ni vema kuiharamisha
 
uchunguzi unaonesha kuwa uvutaji wa sigara Tanzania ni wa huru zaidi ukilinganisha na nchi ya jirani ya kenya.
Tanzania watu wanavuta sigara hadharani, kwenye mikusanyiko ya watu, kumbi za starehe jambo ambalo ni hatari hata kwa wasiovuta sigara.
 
Back
Top Bottom