Leo ni Siku ya Malaria Dunia:Ujumbe Jamii tushirikiane kuutokomeza ugonjwa huu kwa pamoja

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,354
Leo ni siku ya kuadhimisha Ugonjwa wa Malaria Dunia ..Ugonjwa unaongoza kwa kusababisha vifo kwa watoto.

Ujumbe kwa jamii tupambane na mbu,mazalia yake,kuweka mazingira ktk hali ya usafi,kuhakikisha hakuna Mani yaliyotuama,tunafyeka majani.

Wajawazito wanatumia SP kama kinga ya malaria.

Familia tunalala ktk vyandarua vilivyowekwa dawa

Wote wenye dalili za Ugonjwa wa malaria wanafika vituo vya huduma kupata vipimo na dawa.

WHO imezichagua nchi za Kenya,Malawi na Ghana kutoa chanjo ya malaria kwa sababu nchi hizo ina viwango vikubwa vya wagonjwa wa malaria.

WHO imetoa taarifa kuwa kiwango cha malaria kwa nchi zilizo kusini mwaka Jangwa la Sahara kimepungua kwa 21%
 
Malaria ni hatari kuliko hata magonjwa mengine yanayoogopwa kupita kias tushirikiane kuitokomeza tunaweza.....
 
Malaria ni hatari kuliko hata magonjwa mengine yanayoogopwa kupita kias tushirikiane kuitokomeza tunaweza.....
Ni kweli ila watz wanapenda sana mada za siasa
 
Hakika kila MTanzania akichukua hatua kiwango cha maambukizi kitapungua,vifo vya wakina mama wajawazito na watoto vitapungua,na pia jamii itakua huru kwa maambukizi ya malaria.

.Usafi wa mazingira,na ndani pia

kuzuia mirundikano ya vitu

kuchukua hatua ya makusudi kulala ndani ya chandarua zenye viuatilifu

kupata matibabu haraka baada ya kuona dalili

watu wengi huchelewa kwenda hospitali hivyo kusababisha shida kubwa hata ulemavu (degedege)

watoto kutoenda shule ili kupata matibabu

nguvu kazi ya taifa kupotea kwa vifo vinavyotokana na malaria

watu kuhangaika kiuchumi maana pesa nyingi hupotea kwa ajili ya matibabu,

Na kushinda minivan I kuhudhuria misiba kutona na vifo vya malaria nk nk
 
Back
Top Bottom