Leo ndio nimegundua uzandiki wa wanawake

Leo ndio nimegundua uzandiki wa wanawake

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,664
Nilikuwa saloon moja nanyoa nywele za kichwani, ni ya kiume lakini imepakana na ya kike, ghafla nikasikia sauti kubwa kutoka loudspeaker ya simu, sijui ni tecno hiyo, mwanaume akiongea na mdada mmoja hapo saloon ya kike huku wadada wengine wakiwa kimya.

Dada alimpigia jamaa simu, ikawa inaita ndruuu, ndruuuu, ndruuuu kwa sauti kubwa mno, jamaa akawa amepokea halafu mdada akamwambia "wewe ni nani, maana ulinipigia nikakuta miss call?",

Jamaa akaitikia, aahh Lydia! Yule mdada akasema ndio, kwani vipi? Namba yangu umeipata wapi? Basi jamaa akajitetetea, ametongoza, amejielezea, na kuonyesha hisia zake za ndani mno.

Mpaka mimi nikamwambia jamaa aliyekuwa ananinyoa kama amezoeana na hawa wadada akamwambie aache kuweka loudspeaker mpaka sisi tunasikia wakati maongezi ni yake na huyo mtu, awe mstaarabu. Jamaa akanijibu, hiyo ni micharuko achana nayo.

Baada ya maongezi yaliyodumu kwa kama dakika tano hivi, wadada walizua kelele, wakishangilia na kufanya ushambenga na ushakunaku kama mnavyowajua huku wakireplay mazungumzo, nilikerwa sana na hivyo vitendo.

Ndio wakawa wanashauriana aidha waiweke facebook, sijui mara blog ya nani, lakini mwisho walikubaliana kwamba hiyo audio waitupie kwenye group lao la whatsapp isambae mpaka imfikie mke wa jamaa, maana jamaa alionekana ana mke kwa jinsi alivyokuwa anajitetea na yule mdada inaonekana anamjua tu vizuri.

Huu ndio uzandiki wa wanawake, shenzi type. Hivi inakuwaje jitu linamrekodi mtu kisa amemtongoza? Kama hataki kwa nini tu asipokee simu au kukata au kumban? Hii mi miss chagga kweli balaa tupu kaeni nayo chonjo.
 
Si ajabu ukichunguza huyo jamaa ni kapuku tu, hana pesa, hana swaga then tayari ana mke ..!! Sasa anapotongoza vicheche vya mtaani anategemea nini kama sio muadhara kama huo ?

Sometimes kabla hujamtongoza mtu, jiangalie mara mbilimbili kabla hujamuingia. Vicheche vya mjini vinataka tu pesa, angepanda dau then aone kama angewekwa loudspeaker, mbulula huyo ....!!!
 
Kumbe mume wa mtu..acha wakamtangaze..next tym atajua mbinu nzuri ya kudili na michepuko
 
mi sijaelewa kuhusu video........imekujaje kwenye hii simulizi? samahani labda nazeeka na kiswahili kinakua haraka sana.

Wanawake wenzake wapambe walikuwa wanamrekod mwenzao anavyoongea na simu, mm ndivyo nilivyoelewa.
LifeHacker best yangu naona Leo umeamka na sisi toka asubuhi uko na mada za ke tu.....
 
Last edited by a moderator:
mi sijaelewa kuhusu video........imekujaje kwenye hii simulizi? samahani labda nazeeka na kiswahili kinakua haraka sana.

hapo ndo tunaambiwa ukiwa muongo uwe na kumbukumbu!!

si unajua story za kutunga, halafu huyu jamaa leo hii ni story ya tatu kuileta hapa jf
 
Awekwe tu kila siku wanasikia matangazo kuwa MICHEPUKO SIO DILI, TULIA NJIA KUU hasikii inamana ?????? Nyie ndugu mliooa mtulie tu mtuwache masingle tusumbue na kutenda dhambi maana tutatubu mbeleni.
 
Wanawake wenzake wapambe walikuwa wanamrekod mwenzao anavyoongea na simu, mm ndivyo nilivyoelewa.
LifeHacker best yangu naona Leo umeamka na sisi toka asubuhi uko na mada za ke tu.....
Khaa!! Sasa mkewe atamtambua vipi?? Hii pombe sasa
 
Last edited by a moderator:
Baada ya maongezi yaliyodumu kwa kama dakika tano hivi, wadada walizua kelele, wakishangilia na kufanya ushambenga na ushakunaku kama mnavyowajua huku wakireplay mazungumzo, nilikerwa sana na hivyo vitendo. Ndio wakawa wanashauriana aidha waiweke facebook, sijui mara blog ya nani, lakini mwisho walikubaliana kwamba hiyo audio waitupie kwenye group lao la whatsapp isambae mpaka imfikie mke wa jamaa, maana jamaa alionekana ana mke kwa jinsi alivyokuwa anajitetea na yule mdada inaonekana anamjua tu vizuri.

Mmmmmmh!!!!!!!!!!!! kazi kweli kweli.
 
Khaa!! Sasa mkewe atamtambua vipi?? Hii pombe sasa

Mkuu wewe naye una Rohombaya kama ya swetain, jamaa anajieleza hadi majina na anakoishi, yaani details zake full, walichotaka kufanya ni kutuma hiyo audio kwa mkewe, ila mwishoni wakasema tuitupie whatsapp.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom