Leo nataka niwape kisa kimoja hivi kinanihusu mimi

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
424
1,044
Mwaka 2018 hadi 2019 tulikuwa na kampuni, by share mimi nikiwa na share ya 40% wengine wawili 30%

Picha linaanzia Bukoba mwaka 2019 mwezi February nilimfungulia wife biashara sokoni ya kuuza nafaka aina zote pamoja na mafuta n.k.

Sasa mimi nikaendelea na mishe zangu za hapa na pale ili tuongeze nguvu, maana kutegemea kipato kwa mtu mmoja siku ukikoswa itakuwaje na mambo yakabadilika utaishije ikabidi nifanye plani hiyo ili na yeye apambane.

Biashara ilienda vizuri mwanzo, baadae mwezi wa 3 kwenda wa 4 biashara ikaisha bwana . Nikaanza kuuliza, mtaji umeenda wapi na wakati hununui chakula kila kitu nanunua mimi ? Akaanza kukwepa baadae akasema ukweli, kwamba huwa anacheza mchezo baadae waje wagawane vyombo .

Nilishindwa hata kimpiga ikabidi nimuangalie tu, nilichosema ni kwamba mimi na wewe kuhusu suala la biashara tumemalizana sihitaji tena kelele kwa baadae.

Kweli siku zimezidi kwenda mwezi wa 4 tarehe za mwishoni, tukafunga ofisi yetu sababu za uendeshaji, nikamwambia unaona nilichokuwa nakwambia, niliona mbali hivyo ulivyokuwa unajiingiza kwenye makundi ya kinamama ambao walishashindikana.

Wengine walishazoea kwenye hiyo michezo, wewe ndio umeanza unakurupuka umepata faida gani au mnagawana lini hivyo vitu? Nilimuuliza kwa upole tu bila hata kugombana.

Baada ya wiki akaja na dina seti ya vyombo vya udongo, nilimuangalia nikatikisa kichwa tu. Kwamba hapa hamna mtu nivile tunasukuma siku ziende.

Baada ya hapo life lilikuwa gumu kiukweli, na nilijionea kumbe mwanamke mzuri niyule anayepokea tu kuliko anayetoa na yeye. Mimi kwa mwezi mmoja nilikaa home sikuwa na connection yeyote, hapo natafuta kazi siyo kwamba nimekaa tu home, hapana.

Kitu nilichojifunza kwa wanawake wetu hawa, jitahidi sana uwe na hela kama siyo hela basi uwe na sehemu ukitoka unaenda kufanyakazi unaleta chochote lasivyo huwezi kuishi na mwanamke.

Kwa mwezi huo ambao nilikaa huku nikitafuta mchongo tabia niliyoiona kwa mwanamke ni nyingine kabisa na huwezi amini. Sema sisi wanaume Mungu alituumba bwana pamoja na kwamba tunakula kwa jasho ila alitupa kitu kinaitwa moyo wa uvumilivu hapo Mungu tusimlaumu aisee.

Ila baada ya kuwa vizuri sikukata tamaa kwamba mwanamke ni mtu wa kukaa tu au mwanamke hubadilika, nilichofanya tena nimemfungulia duka, maana niliyataka mwenyewe. Mzigo wako huwezi kuuacha hapo mpaka itokee ishu nyingine ila bila hivyo hakuna namna.

Awamu hii niliweka mikwara kwanza kabla ya kufungua duka, naona imesaidia toka 2021 mpaka sasa duka limesimama na matumizi anatoa yeye humo humo mimi kazi yangu ni maendeleo ya nyumbani. Hapo simkufuru, naomba kimdudu kisije kikamuingilia maana hawaaminiki hawa viumbe .

Kwanini nimekupa hii stori, ni kwamba, sisi wanaume siyo kwamba hatupendi wake zetu wafanye biashara, tunapenda sana, sisi siyo kizazi cha kale ambacho mwanamke alikuwa akiolewa anakuja kufanya kazi za kilimo au kuchunga.

Kizazi chetu tunajitambua sana, sema watu ambao tunataka tusaidiane nao ndio changamoto kwetu. Wamekuwa ni watu wakusikiliza watu wa nje kuliko wewe uliyemtoa kwao au uliyemuoa na kumpa mtaji na ndicho kitu ambacho kinatupa wanaume wengi, kinawapa hasira wanakataa kuwamini wanawake kwa kiasi kikubwa na kuna wanaume wengine huwezi kuwapa wazo la kumsaidia mwanamke akakuelewa.

Wanawake wamekuwa ni chanzo cha migogoro mingi ndani, ila ndio watu wanaoongoza kulalamika kuwa wananyanyasika kuliko wanaume ambao ndio watendewa wakubwa.

NB: Msininukuu vibaya, nimeleta Threads hii tujifunze siyo kutoleana mapovu.
 
Back
Top Bottom