GE2025 Leo Magari yenye chata za Makonda na kombati ya kijeshi yameenea jijini Arusha kuelekea uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu

GE2025 Leo Magari yenye chata za Makonda na kombati ya kijeshi yameenea jijini Arusha kuelekea uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Makonda ni mtu wa hovyo sana.

Sijui kwanini chama changu kilimpitisha?
 
Shamra shamra za kampeni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea kushika kasi!

Leo magari yenye chata la mtia nia kupitia Jimbo la Arusha Mjini, Paul Christian Makonda yameonekana yakizunguka mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha yakitoa hamasa na ishara ya uzinduzi mkubwa wa kampeni.

Soma pia: Paul Makonda ateuliwa kugombea ubunge jimbo la Arusha Mjini

View attachment 3468177

Paul Christian Makonda ni jina lililosubiriwa kwa hamu na wananchi wengi kutokana na msimamo wake thabiti na upekee wake wa kusimama na watu. Ni kiongozi aliyekuwa kivutio, sasa akiingia rasmi kwenye ulingo wa ubunge Arusha Mjini.

Uzinduzi rasmi wa kampeni unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Septemba 2025 katika Viwanja vya Soweto, Arusha, huku mgeni rasmi akiwa Mgombea mwenza wa Urais, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.

Hizi ndizo shamrashamra kuelekea siku ya kihistoria kwa Arusha!
Haya yote ni madhara ya chama kuwa juu ya serikali kwa hiyo wala hakibanwi na sheria zozote za nchi , wenye akili timamu CCM wameisha wote, mabilioni kwa mabilioni yanatumika wakishindana na CHAUMMA, hii ni mbinu ya kutakatisha pesa za chama
 
Mbona uwanja wa soweto utakua mdogo?Wangefanyia stadium kabsa.
 
Huyu Bashite nani amemruhusu atumie rangi za Jeshi letu la wananchi kuhalarisha wizi aliiloutebfs enzi za nafuguli?

Tumeruhusu Jeshi letu pendwa na linaroheshimika kuanza kubagazwa?
 
P
Mkuu kwa wiki 3 mfululizo kupitia Polepole JK na Rostam wametuhumiwa mangapi!?, umeona wakikonda?, point yangu sio watu wapotezee, ila nikipata nafasi nawashauri watu wapambanie matumbo yao, kwa watanzania wa leo hakuna wa kuingia Front kufanya lolote, kuendekeza lugha za jinai haiozi ni kusubiri embe chini ya mnazi. Lazimisha, force connection, kuwa hata CHAWA upate maisha mazuri. Leo hii baba Levo na Mwijaku wana maisha mazuri, wakati ma lecturer wa UDSM bado wanaishi kutegemea kuuza maziwa kwa ng'ombe watano. Mambo yamebadilika, tubadilike pia. Hawa watanzania wa leo sio wa kuwategemea kwenye mabadiliko ya kweli nchini. Ukituliza kichwa utanielewa.
Point kubwa hapa ni kwamba hakuna wa kukupambania, jipambanie mwenyewe. Ukipata nafasi itumie vyema
 
Shamra shamra za kampeni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea kushika kasi!

Leo magari yenye chata la mtia nia kupitia Jimbo la Arusha Mjini, Paul Christian Makonda yameonekana yakizunguka mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha yakitoa hamasa na ishara ya uzinduzi mkubwa wa kampeni.

Soma pia: Paul Makonda ateuliwa kugombea ubunge jimbo la Arusha Mjini

View attachment 3468177

Paul Christian Makonda ni jina lililosubiriwa kwa hamu na wananchi wengi kutokana na msimamo wake thabiti na upekee wake wa kusimama na watu. Ni kiongozi aliyekuwa kivutio, sasa akiingia rasmi kwenye ulingo wa ubunge Arusha Mjini.

Uzinduzi rasmi wa kampeni unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Septemba 2025 katika Viwanja vya Soweto, Arusha, huku mgeni rasmi akiwa Mgombea mwenza wa Urais, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.

Hizi ndizo shamrashamra kuelekea siku ya kihistoria kwa Arusha!
Aanze kwanza kukemee sheria kandamizi za utoaji maoni na kufungulia jakwa hili ndo ulete haya maigizo hapa
 
Back
Top Bottom