Daud Salum na Ibrahim Malekano nilisoma nao. Daud Salum alikuwa mbele yangu mdarasa matano, yaani nikiwa form 1 yeye alikuwa form 5. Yeye tulikuwa naye shule moja Tabora School. Ibrahim Malekano alikuwa Kazima akiwa mbele yangu madarasa mawili, yaani nikiwa form 1 yeye alikuwa Form 3; alikuwa darasa moja na mchezaji mwingine Marsha aliyejiunga na Yanga. Mola wetu aiweke pema peoponi roho ya marehemu Malekano.