Lengo ni nini hasa?

Lengo ni nini hasa?

ADUI

Member
Joined
Aug 6, 2009
Posts
82
Reaction score
10
Nimeshtuka kwamba nina zaidi ya filamu 300 katika hard disk yangu . Mimi napenda sana filamu hivyo huzitafuta popote pale zilipo. Kutoka VHS mpaka DVD format ni hatua kubwa sana, na kama kawaida kuna wajanja wanaotuwezesha kupata filamu nyingi kwa wakati mmoja na kwa bei ya chini sana (ubora wake unafanana na bei). Siku hizi, kutokana na wingi wa computers wengi tuzipata hizi films kupitia mtandao (torrents) kitu kimetoka jana keo ninacho! Mimi pamoja na wengi tufurahia sana hii hali, ILA kengele imepiga kichwani, najiuliza ni KWANINI hali iko hivi? Je ni kweli hii ni kutokana na maendeleo ya teknolojia na kwamba ni kitu ambacho hakiwezi kuzuilika? Au ni mpango tu ? Nimejiulliza hivi kutokana na ukweli kwamba mambo yanayooneshwa kwenye filamu nyingi siku hizi si mazuri, tn nyingine zinakuwa labeled kama teen movies au comedy lakini utakayoyaona humo ni mengine kabisa. Ni kizazi gani tunachokiandaa? Inasikitisha kuona hata filamu za hapa nyumbani zimeingia kwenye mkumbo huohuo, mavazi ya kina dada kwenye hizi filamu ni ya aibu… nisiendelee sana, ila ninachotaka kusema kuwa tuwe macho ‘taifa la kesho’ linaangamia. Hivi utamueleza nini mtoto ambae tangu anakua anaona ushoga kwenye tamthilia na filamu ni kitu cha kawaida tu, huu ni mfano. Mungu atusaidie tuujue UKWELI.
 
La msingi ni Kila kitu kifanyike kwa wakati sahihi, Ukiweza zuia mtoto kutazama vinavyozuilika, Maombi yasikae kando, Ila ukiweza mjengee mtoto kadunia kake, mfano _Shule bora, Home, and kuangalia hata marafiki mtoto anao associate nao, La hasha Mh!!!!! I don know:confused2:
 
Back
Top Bottom