Sijui kama nitaeleweka kwa wepesi.. anyway:
Ukitaka kuelewa vizuri hii dhana, Jifunze historia kidogo kuhusu nafasi ya mwanamke kwenye jamii na alikua anachukuliwaje kutokea enzi. Pia wazazi walikua wana nafasi gani katika hilo. Pia tendo la kuolewa lilikua linachukuliwaje?
Ngoja niiangalie kimaandiko kidogo:
Mwanzo 34:12 ''Mjapoongeza sana
mahari na zawadi,
nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini
mnipe huyu msichana, awe mke wangu''
Kutoka 22.16 Mtu akimshawishi mwanamwali, .......na kulala naye, lazima atatoa
mahari kwa ajili yake ili awe mkewe
22.17 Ikiwa
baba yake huyo mwanamwali akataa kabisa kumpa,
atalipa fedha kama hesabu ya mahari ya mwanamwali ilivyo.
Kuna kastori huwa nakapenda kapo kwenye kitabu flani kiitwacho Mathayo chapter 17:25-27 kwenye Biblia. Iko hivi Bwana Yesu akiwa na Petro na wengineo.. waliingia mji flani, wakakuta watu wanalipishwa ushuru. Yesu akauliza hio ni kwa wageni au wana wao? akajibiwa ni kwa wageni. basi akamwambia Petro aende akashushe nyavu na samaki atakayetokeza wa kwanza atakua na shekeli kinywani ''uichukue akalipe kwa ajili yetu ili
TUSIJE TUKAWAKWAZA''
Ukikuta mzazi akasema hapokei mahari, ni vizuri lakini pia ukakuta anaepokea usilalamike TOA usije ukawakwaza maana imeandikwa OLE wake alitaye Makwazo.
MAHARI NI HALALI KWA WAZAZI KUPOKEA. KWENYE HAKI AU NI SAWA AU KIASI GANI NI SAHIHI, HILO NI JAMBO JINGINE.