Nina uhakika hujamsikiliza. Amesema akidi ya baraza kuu haikufikiwa. Walikuwepo Mchungaji Mapinduzi, Mwaipaya, Pambalu, Mwamakula ambao sio wajumbe. Hawa wote walipiga kura kama wajumbe wa baraza, technically Mchome yupo 100% sahihi kanuni zilikiukwa. Japo motivation yake inaweza kuwa ni hasira, disappointment.
Unajua haya yote yanatokea sababu Mshindi Lissu hakuitisha baada ya kushinda mkutano wa kuponya majeraha ya uchaguzi, kuwasikiliza 49% walioshindwa na kujenga uongozi jumuishi.
Ukiwa na akili timamu huwezi kuwa dismissive of 49%. Utajaribu kuwaweka karibu. Mshauri wako mkuu akiwa Lema utapotea. Lema yupo vizuri kwenye mipango ya pesa, kutukana na kudhalilisha upinzani ndani au nje ya chama.
Busara ya upatanishi hana. Anawaita wenzake maboya, wapumbavu, wajinga. Kisa amepewa ukimbizi Canada. Watanzania wote anawaona ni wapuuzi anamtukana Magu, watu wa kusini wote, yoyote. Kwake huu ndio ujasiri.
Lema is not intellectual sound, sio mpatanishi, anatumia maneno ya kejeli. dharau, matusi, ndio maana alifungwa sana ila ndio anapopata umaarufu, pesa Canada.
Ila yupo vizuri kwenye kampeni kama Tone tone, join the chain. Ni mhamishaji mzuri kupata pesa. Ila yupo very crass, intellectually Lema is extremely limited. Atampoteza Lissu na kumjengea maadui wengi zaidi.