Lembeli: Lowassa naye asafishwe

Lembeli: Lowassa naye asafishwe

Bintiwangara

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
551
Reaction score
287
Mbunge wa Kahama Mjini, James Lembeli (CCM), ameaungana na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba, baada ya kuzungumzia ripoti ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue iliyowasafisha baadhi ya watendaji serikalini waliohusika katika kashfa ya Escrow na Operesheni Tokomeza.

Akichangia bungeni jana, Lembeli alisema wakati Serikali imewasafisha baadhi ya watendaji, haoni jitihada kama hizo za kumsafisha Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa aliyejiuzulu uwaziri mkuu kutokana na kashfa ya Richmond.

Lembeli alikuwa akichangia Hoja ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoiwasilisha bungeni juzi akiomba Sh trilioni 5 kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016.

Lembeli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Utalii na Mazingira, alishangazwa na taarifa hiyo iliyowasafisha baadhi ya watu waliohusishwa katika kashfa hiyo na kuwaacha wengine, jambo ambalo alisema halitoi taswira ya usawa.Katika mchango wake, Lembeli alisema haoni mantiki kwa Serikali kumsafisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Maswi na Waziri Profesa Sospeter Muhongo na kuwaacha wengine.Katika mchango wake juzi Serukamba alijikita zaidi katika kashfa ya Escrow wakati Lembeli alijikita katika kashfa ya Operesheni Tokomeza.

Mapema mwezi huu, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, alisema uchunguzi dhidi ya Profesa Muhongo na Maswi, umebaini kuwa viongozi hao hawakukiuka maadili yoyote katika suala hilo.Mbali na viongozi hao, uchunguzi mwingine wa malalamiko ya utekelezaji wa Operesheni Tokomeza uliosababisha waliokuwa mawaziri watatu kujiuzulu, pia umebaini mawaziri hao hawakujihusisha moja kwa moja na upungufu wa operesheni hiyo.

Viongozi hao ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. David Mathayo David.Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
 
Kwa hiyo mnakubali ni mchafu mpaka saa hizi hapo umewaingiza kingi lumumba wanakula kichwa kiulaini maana hata kwenye hansard za bunge mmejichafua
 
Lowasa na Escrow vinauhusiano gani? Mahakamani hakuna washitakiwa wanaoachiwa huru kwa kutokuwa na hatia?
Kazini hakuna watumishi wanaorejeshwa kazini kwa kufutiwa tuhuma?
Akina Serukamba walitakaje?
 
Asafishwe, arudishwe kwenye nafasi yake,pia waliosafishwa waludishwe kwenye nafasi zao.
 
Serikali dhaifu inaongozwa ki dhaifu
Vitu vipo wazi kabisa
Sasa kama ndio hivi mama yangu pia asafishwe n a mzee wa vijisenti pia
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Siku zote tunajua kuwa kitu kichafu ndicho kinachopaswa kusafishwa ili kiwe kisafi. Ni mwendawazimu tu anaweza kufikiri kuwa kitu kisafi kinapaswa kusafishwa. Kauli zilizotolewa na mbunge wa Kigoma Mjini Peter Serukamba na James Lembeli wa Kahama Mjini kutaka Lowasa asafishwe ni kiashiria tosha kuwa Lowasa ni mchafu. Ndo maana wanataka bunge limsafishe ili awe msafi.

Hata hivyo, si kila kichafu kinaweza kusafishika na kikatumiwa na wasafi. Vitu vingine hata ufanyeje haviwezi kutakata. Ni sawa na kupika mawe ukategemea yatalainika na kuwa kama kiazi. Pia kuna kinyesi. Kinyesi siku zote ni kichafu. Hata ukikisafisha vipi hakiwezi kutakata na kuwa kisafi kikaliwa tena na binadamu. Katu na haijuzu.

Ndivyo ilivyo kwa Lowasa. Uchafu alionao hauwezi kusafishwa au kutakaswa kwa namna yoyote. Ataendelea kuwa mchafu kama vile kinyesi kinavyoendelea kuwa kinyesi hata ufanyeje. Ifike wakati akina Serukamba na Lembeli wabaini kuwa si kila kichafu kinaweza kusafishwa kikasafishika. Vingine vinabaki katika asili yake na vinaweza kutumika kwa namna nyingine ili kupata kitu kisafi. Kama vile kinyesi kinavyoweza kutumika kuzalisha umeme au kurutubisha udongo ili mazao yastawi. Lowasa anaweza kutumika kwa namna nyingine kama kuchangia kwenye harambee za ujenzi wa nyumba za ibada lakini si kuwa Mkuu wa nchi. Haiwezekani na hautakuja kuwezekana.
 
ndani ya ccm kuna double standard nyingi sana kupita maelezo. niseme tu kwanza ccm ina wenyewe.
 
Asafishwe,tena tunataka rais mwenyewe atangaze kuwa Lowasa msafi kama sufi
 
Hahahahahahahahaaaaaaaa! Ahsante kaka Lizaboni kwa kuniongezea siku za kuishi. Nimecheka sana kwenye hii mada. Kuna watu kama akina Serukamba hawajui kuwa siku zote kinachosafishwa ni kichafu
 
Hahahahahahahahaaaaaaaa! Ahsante kaka Lizaboni kwa kuniongezea siku za kuishi. Nimecheka sana kwenye hii mada. Kuna watu kama akina Serukamba hawajui kuwa siku zote kinachosafishwa ni kichafu

mkuu lakini si mwanaccm mwenzenu kama ni mchafu mbona bado mpo naye ndani ya chama
 
Umesema kweli mkuu mzee Lowasa mchafu kuanzia kichwani mpaka miguu hafai msikitini wala kanisani tupa kule.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Siku zote tunajua kuwa kitu kichafu ndicho kinachopaswa kusafishwa ili kiwe kisafi. Ni mwendawazimu tu anaweza kufikiri kuwa kitu kisafi kinapaswa kusafishwa. Kauli zilizotolewa na mbunge wa Kigoma Mjini Peter Serukamba na James Lembeli wa Kahama Mjini kutaka Lowasa asafishwe ni kiashiria tosha kuwa Lowasa ni mchafu. Ndo maana wanataka bunge limsafishe ili awe msafi.

Hata hivyo, si kila kichafu kinaweza kusafishika na kikatumiwa na wasafi. Vitu vingine hata ufanyeje haviwezi kutakata. Ni sawa na kupika mawe ukategemea yatalainika na kuwa kama kiazi. Pia kuna kinyesi. Kinyesi siku zote ni kichafu. Hata ukikisafisha vipi hakiwezi kutakata na kuwa kisafi kikaliwa tena na binadamu. Katu na haijuzu.

Ndivyo ilivyo kwa Lowasa. Uchafu alionao hauwezi kusafishwa au kutakaswa kwa namna yoyote. Ataendelea kuwa mchafu kama vile kinyesi kinavyoendelea kuwa kinyesi hata ufanyeje. Ifike wakati akina Serukamba na Lembeli wabaini kuwa si kila kisafi kinaweza kusafishwa kikasafishika. Vingine vinabaki katika asili yake na vinaweza kutumika kwa namna nyingine ili kupata kitu kisafi. Kama vile kinyesi kinavyoweza kutumika kuzalisha umeme au kurutubisha udongo ili mazao yastawi. Lowasa anaweza kutumika kwa namna nyingine kama kuchangia kwenye harambee za ujenzi wa nyumba za ibada lakini si kuwa Mkuu wa nchi. Haiwezekani na hautakuja kuwezekana.

Mwaka huu utatanuka moyo tuu........Simama uhesabiwe huu ni mwaka wa matumaini na ENL
 
Kumsafisha Lowassa kutatakiwa Richmond nyingine mpya ili zipatikane fedha za kutosha kununulia marobota ya steel wire zitakazo tosha kumsafisha Lowassa,kwani Lowassa hawezi kuwa safi bila kuchubua ngozi yake kama mbuzi wa ndafu.
 
mkuu lakini si mwanaccm mwenzenu kama ni mchafu mbona bado mpo naye ndani ya chama
Wasira aliwahi kusema kuwa hakuna chma cha mafisadi ila kunamafisadi ndani ya vyama kama alivyo Lowasa kwa ccm na Mzee slaa kwa chadema yote haya ni mafisadi tena mpaka kwa wake za watu.
 
Serikali dhaifu inaongozwa ki dhaifu
Vitu vipo wazi kabisa
Sasa kama ndio hivi mama yangu pia asafishwe n a mzee wa vijisenti pia

wewe una kichwa cha bata inamaana umesahau kuwa muhongo na maswi waliundiwa tume ya uchunguzi ili kujiridhisha?
 
Umesema kweli mkuu mzee Lowasa mchafu kuanzia kichwani mpaka miguu hafai msikitini wala kanisani tupa kule.
Nashangaa hayo makanisa na misikiti yanamshobokea. Najua wanachotaka ni fedha zake na si yeye mwenyewe. Wanatimiza usemi wa kiswahili usemao kuwa Baniani mbaya kiatu chake dawa
 
Sijui kama Lowasa hajawahi kuiba kwenye eneo alilowahi kuwa kiongozi mzee mwizi mpaka anajiogopa yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom