MUME MWEMA
JF-Expert Member
- May 16, 2013
- 327
- 44
Khaa!! Kama ule waraka wa dr kitila??
- Kaka NEC ndio Mkutano wa mwisho wa CCM wa kuamua msimamo wa CCM kama Lembeli hautaki ajiondoe mara moja kwenye chama ambachi hakikidhi mahitaji yake!1
Le Mutuz
tgis ninja huwa anapenda kulopoka tuJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, James Lembeli (CCM), amesema kuwa yuko tayari kufanyiwa lolote na chama chake lakini kamwe hatatengua msimamo wake wa kudai Serikali ya Tanganyika.
Kauli hiyo nzito ya Lembeli, mmoja wa wabunge wa CCM wenye msimamo mkali, ilipata kutolewa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere miaka ya 90 wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo chama hicho kilikuwa kikituhumiwa kwa rushwa na hivyo kupoteza mwelekeo.
Katika mazingira hayo, Mwalimu alisema kama chama hicho kisipojirekebisha, anaweza kurudisha kadi yao, kwani CCM haikuwa mama yake.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu huku akitumia maneno hayo ya Mwalimu, Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama alisema baadhi ya wajumbe ni waoga na wanafiki kwa kuogopa kusimamia kile wanachokiamini.
Historia haikarabatiwi, mimi naweza kufa au kuadhibiwa na chama changu kutokana na msimamo huu lakini historia itaandikwa.
Pale Ikulu si kuna picha ya hayati Oscar Kambona, huyu si alifungwa kwa makosa ya uhaini, mbona picha yake haikuondolewa katika viongozi wa historia ya nchi hii? alihoji.
Lembeli alidai kuwa Watanzania wasubiri wamuone wakati wa mjadala wa pamoja wa rasimu ya Katiba bungeni huku akitamba kuwa hatabadili msimamo hata kama unakinzana na wenzake wa CCM.
Sina wa kumfurahisha zaidi ya wapiga kura wangu, hawa ndio wenye uwezo wa kunishughulikia endapo nitaunga mkono jambo ambalo litakuwa kinyume na wao.
Mimi ndiye Lembeli na nitabakia kuwa hivyo, ndiyo maana nilikuwa nataka itumike kura ya siri ili kuhifadhi uhuru wa mawazo yetu. Nyerere alituambia kuwa wananchi wanataka mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM, alisisitiza.
Lembeli aliwataka wajumbe wenzake kuacha woga wa kufungwa na misimamo ya vyama au makundi yao kwani hata Rais Jakaya Kikwete aliwahi kusema: Akili za kuambiwa changanya na zako.
Chanzo: Tanzania Daima
- Kaka baba yako simjui ila one thing habari za kura ya siri na wazi sio ishu tena imeisha tuwe progressive tuongelee mapya ya kura za siri na wazi yamepitwa na wakati sasa!! na Kidumu chama cha mapinduzi
Le Mutuz
Lembeli; CCM si mama yangi
Kumbuka ccm imekufikisha ulipo, kama unataka Tanganyika hiyo sio sera ya ccm, kumbuka uliapa kulinda muundo wa muungano! Leo unageuka, kwanza neno lenyewe Tanga
- TOO BAD Katiba inatengezwa kwa mujibu wa sheria zilizopo sasa ambazo zipo wazi kwamba chama kinachotawala ndio chenye nafasi kubwa ya kuandika Sheria na sio vinginevyo!!
Le Mutuz
Le Mutuz hebu elewa nasema nini,issue ya kura ya siri na wazi haijaisha kwa kuwa wenye akili wanajua kwanini ccm ililazimisha kupigwa kura za aina mbili kuamua jambo moja.Kusema limekwisha sio sahihi isipokuwa ccm wameona ni heri kufunika kombe ili mwanaharamu apite,kwa bahati mbaya sana hakuna mwanaharamu ndiyo maana Mh.Lembeli ameamua kujilipua ili jamii ijue ccm wamen'gan'gania kura ya wazi ili waweze kuwaadhibu wana ccm wa aina ya Lembeli Kangi Lugola na Deo Filikunjombe.Huwezi kuanzisha mfumo huo wa upigaji kura ambao haupo na haujawahi kuwepo popote duniani kwa kutumia lugha nyepesi sana ya kiwango cha chini mno katika kuwashawishi wananchi kwa kuwaeleza eti RAIA WANATAKA KUONA MWAKILISHI WAO AMEAMUA NINI KATI YA SERIKALI 2 au 3,ndiyo sababu ya kukueleza hawa Watanzania sio wale wa enzi zile za kina hekaya za abunwasi ilipotokea sufuria kuzaa.
Hivi bwana mzee hiyo picha yako hapo juu ni ya mwaka gani? Una mawazo ya kijima sana!
By the time you will be realizing the truth that an earth revolves around the sun it will be too rate, hata baba yako mr Malecela anataka na anajua umhimu wa serikali tatu.- CCM ni chama kikubwa sana hakiwezi kuyumbishwa na wabunge 2 tu, so get that right watoke waje huko kwenu kwenye vurugu kila siku!!
Le Mutuz
By the time you will be realizing the truth that an earth revolves around the sun it will be too rate, hata baba yako mr Malecela anataka na anajua umhimu wa serikali tatu.
Kama Zanzibar ni nchi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaundwa na nchi zipi? Huu Muungano ni kiinimacho, ni muungano wa kinafiki na kisiasa(CCM BARA na CCM VISIWANI)Kwa wale waumini wa serikali mbili 1. Nchi iitwayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ipi? Yaani muungano wa Tanzania ni upi? Au ni Jamhuri ya muungano ya Tanzania? Nadhani wajuzi wa kiswahili watudadavulie. 2. Jamhuri hii ina ardhi yake? Je, inaendeshwa kwa mapato yatokanayo na rasilimali za ardhi yake? 3. Nchi ya zanzibar ni nchi ndani ya nchi ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania?
ana hasira na nyalandu kumnyima ulaji.
Ccm,pigachini hii bulukenge.