Lema: Nitabeba zigo la mabilioni ya Uswisi

Lema: Nitabeba zigo la mabilioni ya Uswisi

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2009
Posts
2,975
Reaction score
3,436
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), amesema atamshawishi mbunge mwenzake wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ili ampatie majina ya vigogo walioficha fedha Uswisi awataje bungeni. Zitto ndiye aliibua hoja hiyo bungeni na kuwasilisha hoja binafsi akitaka Bunge liazimie kwa kauli moja na kuunda kamati teule ya kuchunguza tuhuma hizo na kuwachukulia hatua, vinginevyo serikali ikishindwa atawataja.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Kahama mkoani Shinyanga, alipopata mapokezi ya kifalme akiwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche na kada mwingine, James Ole Millya, alisema kuwa atataja majina hayo bungeni. Lema alisema kuwa Watanzania wamekuwa na shauku ya kuwafahamu viongozi wao mafisadi waliopora fedha zao na kwenda kuzificha katika nchi za ughaibuni kama Uswisi, Mauritania, Dubai na Morocco.

Alisema tangu hoja hiyo ifikishwe bungeni na serikali kuahidi kufuatilia, hadi sasa kumekuwa na ukimya ambao unazua maswali juu ya ukweli wa suala hilo kutoka kwa wananchi. "Nitamuomba Kamanda Zitto anipatie majina hayo nami Bunge lijalo niyaanike ili kukata kiu ya Watanzania walio na haja kubwa ya kuwafahamu, hata kama hatua hiyo itanisababishia kifo, mimi siogopi kufa," alisema Lema.

Aliwataka wakazi wa Kahama kuondokana na woga pindi linapofikia suala la kupigania haki zao na akasema wasiwaachie viongozi na wanachama wa CHADEMA pekee.Lema aliishutumu Serikali ya CCM akidai imeshindwa kuwajengea miundombinu mizuri na kuwakopesha mitaji mikubwa wachimbaji wadogowadogo pindi wanapovumbua maeneo yenye madini.

Alisema kuwatimua wachimbaji hao ni kupanua wigo wa watu wasiokuwa na ajira, ombwe ambalo linaweza kuigharimu nchi hata kuingia katika machafuko. Wakati huo huo, kada mashuhuri wa CCM, Frank Mwaisumbe, aliyeitikisa ngome ya upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 akiwania ubunge katika Jimbo la Mbeya Mjini, amehamia CHADEMA. Mwaisumbe aliyewahi kuwa Mhadhiri Msaidizi wa Kitivo cha Uchumi na Biashara katika Chuo Kikuu cha Tumaini-Iringa, kabla ya kuachana na kazi hiyo, ametangaza kujiunga na CHADEMA juzi.

Alisema CCM imeshindwa kushughulikia kero na matatizo ya wananchi ikiwemo rushwa na makundi yanayowania madaraka. Jimbo hilo la Mbeya Mjini kwa sasa linaongozwa na Mbunge wa CHADEMA, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu baada kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Benson Mpesya.

Katika hatua nyingine, vijana wametakiwa kutokuwa na fikra mgando katika kupambana na matumizi mabovu ya rasilimali yanayofanywa na baadhi ya watu wachache ili kuliokoa taifa linaloangamia. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Iringa, Joseph Lyata katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Luganga wilayani Kilolo.

Lyata alisema ili taifa liweze kusonga mbele, lazima liwe na watu wenye uchungu na rasilimali zilizopo na kujali matumizi ya pamoja. Habari hii imeandaliwa na Ali Lityawi (Kahama), Gustav Chahe na Happiness Elias (Iringa)
 
Huyu jamaa ananikumbusha wale wapigania haki wa South Afrika ambao walijitolea maisha yao kwa ajili ya ukombozi.
 
Tupo pamoja kamanda Lema,mwenzako anaishia tu kusema NItaje nisitaje,
 
Spika atampa hiyo nafasi?

Ushauri wangu ni kuwa afanya kama alivyofanya Dr. Slaa alipotutajia ile list of shame pale Mwembe yanga.
 
Najivunia chama changu CDM,najivunia makamanda Lema,Lissu,Nassari,Heche,Wenje,Msigwa,Sugu,Kigaila,Mawazo,ila Lema namfananisha na Mandela,kila la heri kamanda Lema
 
Bila kumsahau kamanda Mnyika hili ni jembe muhimu hata aliweza kutufumbua macho kwa kutuambia serekali na viongozi wake dhaifu gogogogogooooooooooo CHADEMA
 
ZITTO ANAVOPENDA UMIMI

SIDHANI KAMA ATARIDHIA KUKUKABIDHI MAJINA HAYO

labda nayeye lema akubarik kwenda kwa waganga
 
najivunia chama changu cdm,najivunia makamanda lema,lissu,nassari,heche,wenje,msigwa,sugu,kigaila,mawazo,ila lema namfananisha na mandela,kila la heri kamanda lema
hv huo ukamanda mnautoa wapi?
 
Bila kumsahau kamanda Mnyika hili ni jembe muhimu hata aliweza kutufumbua macho kwa kutuambia serekali na viongozi wake dhaifu gogogogogooooooooooo CHADEMA

hahaha mbona aligwaya?? tumieni vizuri vitablet mlivyohongwa hivyo
 
Haka Ka-lema kwa jinsi kalivyo kabishi kanaweza kunitaja kweli..! Ehe baba uliye juu ya jua niepushe na kikombe hiki..!
 
Lema tuambie Chopa na ambulance za UK zimefikia wapi?
Nasikia hawezi tena kwenda Uk kwa sababu anatafutwa kwa kesi ya kujaribu kubaka, kwa hiyo akikanyaga UK tu na ubunge ndio basi manake atafungwa na sizani kama katiba ya tanzania inaruhusu wahalifu kuwa wabunge
 
Back
Top Bottom