Lema: Nilifunga kula kuliombea Taifa

Alokwambia kuwa alikuwa anatuombea wana wa Arusha nani! Ye alikua anaombea wahisani wamuongezee posho kwa kuwa kakaa lockup.
Mkuu Rais si ndie aliyesema tumuombee? Sasa Mh Lema anaomba inakuwa tabu tena, au ni wana ccm tu ndio wanatakiwa waombe?
 
Lema soma alama za nyakati mdogo wangu kila siku tunakusihii zama hizi sio zile ulizozizoea
 
nimependa jinsi alivyo jenga hoja alikuwa amefunga kuombea taifa siyo kwamba aligoma kula.
 
Sasa hapo wangempatia wapi kwa kosa la kujaribu kujiua wakati imani yake inamruhusu kufunga?.
 
Polis walikuwa wanataka kunfungulia kesi ya kutaka kujiuwa.....ili kuikwepa ndio maana amesema hivyo
 
Hapo sasa Lema alikuwa amefunga kuliombea Taifa,sijui wabaya wake watayakataa maombi vipi kwa kuwa nao ni sehemu ya Taifa.
 
Tutakosea kumuita mbunge huyu kigeu kigeu wa kauli?juzi alisema amesusa kula kwa kuwa kadhalilishwa,leo anasema alikuwa amefunga kuliombea taifa,moja ya sifa ya kamanda ni kuwa na kauli thabit....kuna umuhimu wa kamanda huyu kujipima kama anastahili kuitwa kamanda.
 
Ah ah ah lema ametisha km ngamia wa jangwani next time tutampeleka kisimayu somaliaaaa ili tujue uwezo wake wa kukaa na njaa
 
Una uhakika.kama.alisema.hivyo? Haya aliyosema leo tumesikia wote na kina video clip, hayo ya juzi alisemea wapi? Tumwamini nani, Lema muhusika mwenyewe au wewe wa JF.
 
"Nilifunga kuliombea taifa"… .Maneno matatu tu ila yana ubora mara 1000 zaidi wale wanaotokwa na povu humu ndani kwa kubeza ulichokisema najua sio level zako hivyo hutakiwi kuwajibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…