SI KWELI Lema na Sugu wamepongeza tume ya uchunguzi

SI KWELI Lema na Sugu wamepongeza tume ya uchunguzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
LEMA, SUGU WAMPONGEZA DKT. SAMIA KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA UVUNJIFU WA AMANI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema na Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu wamempongeza Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.

Viongozi hao wamesema hatua hiyo inaleta mustakabali mzuri wa Taifa kurudi katika umoja na Rais Samia amejibu kilio cha Wana-CHADEMA na kuwakemea wachache wanaotaka kuvuruga amani.

“Alichofanya Rais Samia ni hatua kubwa sana, Jumuiya za Kimataifa zinapaswa kumpongeza. Sisi Chadema tunaona kile tulichokipigania anakifanya kwasababu tunataka Tanzania kuwa wamoja tena,” alisema Sugu

Naye Lema alisema, “Tunakwenda kutumia Watanzania wenzetu katika Tume hii kutupa majibu ambayo yataenda kuponya Taifa. Wakafanye kazi yao vizuri na sisi tutawapa ushirikiano,”​

LemaSugu.jpg
 
Tunachokijua
Novemba 18, 2025 Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka alitoa taarifa kwa umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliunda Tume ya kufanya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.

Aidha kupitia makamu mwenyekiti wake John Heche, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ilitoa msimamo wake kuhusu tume iliyoandaliwa kuchunguza “matukio ya uvunjifu wa amani” baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 na kwamba haiitambui tume hiyo.

Madai

Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikiwataja Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) na Godbless Lema kuwa wamepongeza tume hiyo ya uchunguzi.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani viongozi Sugu na Lema hawakutoa kauli hizo bali ni taarifa iliyotengenezwa na wapotoshaji.

Aidha kupitia ukurasa wake wa X, Lema amekanusha taarifa hiyo akibainisha kuwa imetengenezwa na wapotoshaji.

"Siwezi kupongeza chochote kinachofunika damu ya watu iliyomwagika. Wapotoshaji waache kutumia jina langu kusafisha maovu."

Aidha baada ya tume ya uchunguzi kutangaza Lema alisisitiza kuwa tume hiyo haiwezi kuwa huru kutokana na msingi wake umetegemea uteuzi wa wanaolalamikiwa.

"Tume haiwezi kuwa huru iwapo msingi wake umetegemea uteuzi wa wale wanaolalamikiwa, huo ni mgongano wa maslahi tangu mwanzo."
Machawa ya Samia na genge lake la wahuni yanafikiri watu ni mafala kama wao, uwongo mtupu mpuuzeni huyu
 
Back
Top Bottom