Lema kupanda kizimbani pamoja na viongozi wa CHADEMA wa Arusha mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema kupanda kizimbani pamoja na viongozi wa CHADEMA wa Arusha mjini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Henry Kilewo, Oct 31, 2011.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema pamoja na viongozi wa chadema wa Arusha mjini na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo watapanda kizibani leo kwenye mahakama ya Arusha.

  Hii ni kwasababu ya Lema kutembea kwa miguu kutoka mahakamani na kuelekea kwenye ofisi zake zilizopo maeneo ya ofisi ya mkuu wa wilaya na baadhi ya wananchi waarusha waliyokuwa wametoka kwenye kesi mbalimbali kurudi kwa miguu nao walikamatwa siku ya ijumaa na kufunguliwa mashitaka. tupo mahakamani nitawajuza kinachoendelea.
   
 2. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Polisi wamezidi uwakala, utafikiri ni green guard. Kuna haja ya kudai jeshi letu la polisi, siyo hawa green guards.
   
 3. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,145
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  tujuze upuuzi wote utakao fanywa na police/vibaraka-wa ccm
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  hao polisi nao naona hawana kazi ya kufanya... afadhali wagawiwe mashamba wakalime
   
 5. FIDIVIN

  FIDIVIN Senior Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Human we are full of biases, we want things to be seen the way we want them.
  Naamini story yako umejaribu kuegemea upande mmoja, mbona hujaeleza vizuri kosa la Lema wanalomtuhumu? Haiwezekani akamatwe hivi hivi, lazima kuna sababu wameitaja hata kama unadhani si ya kweli basi ungeisema.
   
 6. d

  dotto JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Siku hizi kutembea kwa miguu ni kosa!. Polisi wengi wazee wasokuwa na elimu ndo ving'ang'anizi wa vyeo kwa kuwa ni vibaraka wa magamba. Hata hivyo watafungua kesi ngapi kila baada ya muda wa kesi kuahirishwa!! Nyerere alivunja jeshi la ukoloni na kuunda jeshi la wananchi ingawaje sasa nalo linaanza kujikanganya. jeshi hili la Polisi nalo liundwe upya na jina jipya na waanzilishi(waundaji- wakuu) wapya.
   
 7. O

  Omr JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwani huwajui CDM wewe?
   
 8. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #8
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  kamanda soma post yangu vizuri utapata jibu. kunasehemu nimesema, hii ni kwasababu lema kutembea kwa miguu kutoka mahakamani kuelekea ofisini kwake.
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Nchi inaongozwa na sheria kwa nini ufanye maandamano kienyeji na kundi la vibaka watu wanashindwa kufanya kazi wakihofia kuporwa na vibaka
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Tujuze yajirio na achana na hawa baadhi ya vilaza unaokutana nao humu kwani mbinu zao tunazijua.
   
 11. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Umesoma vizuri bandiko lake?hebu rudia tena utaona kakamatwa kwa kosa gani.
   
 12. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Em waulizen hao waendesha mahakama kuwa, walitaka hao raia watembee na nin hasa! Non sense!
  Hv ccm kwa nin huna Aibu, ama kwel skio la kufa haliskii dawa! ccm nchi s yenu wala hzo mahakama haziwahusu! Get away from our Hon MP, Lema!
   
 13. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Alitembea akiwa peke yake au alizungukwa na wenziwe?
  Mbona unatoa mambo nusu nusu!
  Kama walikuwa wengi na wanatembea kama ninavyofanya, hayo ni maandamano yasiyo na kibali, umempa afwandi Arufonsi sababu ya kukuning'niza.
   
 14. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mi nilifikiri ni Dr.Kiiza Besigye wa Mu7 Uganda,Kumbe na Tanzania hii ina-apply?Kweli East African Community Kiboko.Tunachoshukuru Bongo ni Vita ya Arusha tu na Chuki za CCM kwa Lema,naomba wasirogwe Kumzuia Dr.Slaa eti naye asitembee ya miguu akitaka.Nadhani ndio sababu ya UDSM kuwatunuku PhD JK na Mu7,kwamba akili zao zinafanana namna wanavyowatumia Pilisi kifedhuri.Aibu yao wenyewe.
   
 15. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #15
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  kesi ndiyo inaanzwa kusikilizwa sasa, watuhumiwa wanaitwa majina.
   
 16. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #16
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  baada ya dakika chache nitawajuza kinachoendelea zaidi maana watu wamejaa mno hakuna muda wa kuandika kila kinachondelea
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Sasa hao walioenda kusikiliza kesi wakitoka hapo watapanda garimoshi au watatembea kwa miguu?
  Si watakamatwa tena?
   
 18. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Na leo sijui watakamatwa tena wakitoka mahakamani......maana wengi hawana magari
   
 19. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Tupe habari zaidi mkuu Kilewo
   
 20. U

  Uyole12 JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 586
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  mbona tulivyotoka kwenye mechi ya simba na yanga watu walitembea kwa miguu na hawakukamatwa tena walikuwa wengi kweli.
   
Loading...