Lema inabidi aende shule ili atimize malengo

Lema inabidi aende shule ili atimize malengo

Ndugu yangu Lema-

Huu ni ushauri wangu kwako ili kukujenga na kukufanya uwe bora zaidi (constructive criticism). Lema ndugu yangu, unatatizo kubwa sana la kuongea kiingereza- kama mimi. Huna utawala mzuri wa lugha hiyo. Hivyo basi, jifunze kiingereza na epuka kuweka maneno ya kiingereza kila wakati unapoongea kiswahili. Hii ni tabia mbaya sana ya sisi watanzania. Ndio maana tumejikuta hatajui lugha zote mbili. Usione aibu kukiri kutojua na kujifunza.

Ndugu yangu Lema- unatatizo kubwa sana la kuchambua mambo. Huwa unachanganya sana mambo. Nadhani mara nyingi unakuwa na jazba na kutaka kuongea kila kitu. Mwanasiasa mzuri ni yule aliyekuwa mtulivu. Adui wako wa kisiasa leo ni rafiki kipenzi kesho (mfano mzuri Lowassa).

Ndugu yangu Lema- kwa nafasi yako ya waziri kivuli haiendani na elimu yako na wala utawala wa lugha na kuchambua mambo. Nakushauri soma zaidi ndugu yangu. Julius Malema wa EFF wiki iliyopita kahitimu degree yake ya kwanza na anataka kusoma masters. Wewe pia unaweza na unauwezo huo.

Ndugu yangu Lema- mwanasiasa mzuri ni yule anayeyaona haya na kuchukua hatua.
Wewe unajua zaidi Lugha gani?
 
Tatizo watanzania tunapenda kutupia lawama kwa serikali au viongozi wetu,lakini ukweli ni kwamba aina ya viongozi au serikali inaakisi jinsi watanzania wenyewe walivyo.

Sasa ukiona kiongozi kachaguliwa mwenyewe wa ajabu ajabu hana sifa za kuwa hapo alipo,basi ujue tatizo limeanzia kwa wananchi wenyewe nao wana matatizo na ndiyo maana ikawezekana kuchaguliwa kiongozi wa aina hiyo.

Ukiangali comments za watu katika jukwaa la siasa utagundua kwanini hao viongozi wameweza kupata uongozi.
 
Kama kuogopa kusema ukweli ni nidhamu basi bora niendelee kuwa msukule.
Aiseee unajua leo ni Ijumaa. Baada ya weekend ndefuuuu ya kutafuta ndio kwanza nimeingia sehemu hapa muhudumu Betty ananifungulia safari ndogo baridi ili nilegeze vyuma. Tuachane na haya mambo mpaka jumatatu tafadhali. Kila la kheri.
 
Back
Top Bottom