Lema azidi kupata umaarufu baada ya kushtakiwa tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema azidi kupata umaarufu baada ya kushtakiwa tena

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngongo, Oct 8, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Wakuu jana Godbless Lema alishikiliwa kwa muda na polisi baada ya kushtakiwa kwa kosa la kujipatia fedha isivyo halali.Inadawa Bwana Lema alimkopesha fedha [kiasi hakijulikani] Bi Maimuna Rashid mkaazi wa Arusha, Bwana Lema aliweka dhamana kadi ya gari namba T 140 ABK kwa makubaliano ya kurejesha fedha na kukabidhiwa kadi muda ulipopitiliza Bi Maimuna Rashid alilikamata gari lakini ikabainika gari si la Bwana Lema bali linamikiwa kisheria na Bwana Joseph Augustino Mangilima.

  Godbless Lema ana kesi nyingine ya kutishia kuuwa Bwana Estomieh Chang'a kaimu mkurugenzi wa Jiji.Umaarufu wa Bwana Lema umeongezeka kwa kile wakaazi wa Arusha wanachodhani ni uonevu.
   
 2. M

  MZEE SERENGETI JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Haya yote ni mapito tuko pamoja na chadema
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Watu kukopeshana magari na kuvunja mikataba ya makubaliano ni kesi za madai na wala siyo za jinai lakini CCM ni mfa maji na hata jana hukamata.


  Kesi ya kutishia kuua Msimamizi wa uchaguzi haina shahidi pale ofisini kwake na jamaa huyu mwenye uchu wa madaraka angeweza kabisa kujitungia na ieleweke huyu jamaa anapalilia U-DED baada ya bosi mstahiki Bw. Mbuya kutimuliwa kwenye mazingira tatanishi.


  Kifupi tu CCM yaelewa kuwa HER TIME IS UP ONCE AND FOR ALL.

  Kwa Chama ambacho REDET wanakibeba kwa nguvu zote mbona kinatumia nguvu za faulo kuuthibiti upinzani? Hii ni dalili nyingine ya kuwa CCM is gonna lose this election big time.

  Na huyu Mama Batilda Buriani mbona hakemei polisi kuvunja haki za binadamu kama kweli yeye ni Mwana-Arusha? Ni dhahiri kama jina lake linavyobashiri Buriani yake imo njiani kwenye chaguzi hii
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ngongo chukua :A S thumbs_up: na endelea kutujuza yanayojiri huko A town.
   
 5. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu wakazi wa Arusha,, embu tujiulize huyu batilda alikuwa mbuge wa viti maalumu kwa muda wa miaka 5, hapo hapo ni naibu waziri na mwisho waziri kamili.. Ametufanyia nini????

  Sipendi tena sitaki kusikia mambo ya Shule wakati shule zimejengwa wa mfuko wa TASAF ..... tena hazina maabara, library na walimu hata vibanda vya kulala hakuna achilia walimu wa kufundisha... Zimesaidia nini???? tiba hakuna arusha, miundo mbinu mibovu....

  Ukweli ni kwamba hajafanya kitu chochote kile hata, sasa ukimpa ubunge kamili ndiyo itasaidia????? hakuna kitu,,,, Huyu mama anatumia hela nyingi kuhonga Mf. alitoa reflector wa watu wa pikipiki sijui 100, wengine wamepewa bajaj,, wacha hizo anazotoa kama posho kwenye kampeni,, kuna kijana mmoja wa pikipiki alilipwa 20,000 siku ya kampeni za JK arusha na 10,000 kule njiro na sombetini.. sasa swali hizi hela atalipaje????? na amezipata wapi?????? na nikwanini ananunua ubunge?????

  Lema ni kijana wetu, anajua hali yetu na umaskini wetu... atatusaidia zaidi kuliko huyu mama... pia ni kijana ambaye anaweza kuelezwa kitu na kusikiliza hizo kesi walizomfungulia zitaisha tuu na hafungwi mtu... kwani wanajua kitakachowapata...

  Lema ni mkombozi wa kweli Arusha Mjini.
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Ewaaa wapenzi wa kitimoto wanakwambia ukitaka kumhalalisha Nguruwe bila vurugu unamdanganyia pingiri mbili za mua wakati anachekelea utamu wa sukari unamtandika rungu la kichwa habari inamalizika.

  Mkuu Mzee Serengeti, yanamalizikaje msaidie kulipa deni kesi ifutwe utakuwa umemsaidia vinginevyo Mama maimuna atamburuza mahakamani.Nilisema tangu mwanzo Lema ni tapeli wa kutupwa mmeanza kuyaona wenyewe.

  Mkuu Ruta,Hii si kesi ya madai ni kujipatia fedha kwanjia ya udanganyifu.Lema kaweka reheni gari ambalo linamilikiwa na mtu mwingine mama Maimuna kakubali kutoa fedha akijua anayo dhamana akishindwa anachukua mkoko.Muda unapita Mama wa watu anakamata mkoko akidhani mmliki wake ni Lema anashangaa kukuta gari linamilikiwa kihalali na mtu mwingine.
  Mkuu Ruta mimi si mwanasheria ila nimesoma business law akili na upeo wangu unaniambia hii kesi ni jinai [utapeli]


  Mkuu Ntemi kazwile,

  Mimi naiangalia Tanzania kuliko kutazama maslahi ya chama Lema anatuagusha sana nishamweka pembeni tangu mwanzo hakutakiwa kujiingiza kwenye mambo machafu kiasi hiki.Tunayapigia kelele haya mambo yanaturudisha nyuma ndio maana tunataka kuiweka pembeni CCM sasa nashangaa mambo haya akifanya mtu wetu hatuoni ni kosa tunatafuta maneno matamu ya kufarijiana.

  Mkuu Martin davd,Ni kweli Batilda hana mchango wowote Arusha hilo halina ubishi hata mtoto mdogo analijua sawasawa.Unaharibu unaposema Lema ni mkombozi wa kweli Arusha mjini.ukombozi wake uanziae kurejesha fedha za Mama Maimuna na aombe radhi kwa kumkabidhi kadi ya gari ambalo si lake.Huu ni utapeli mbaya unaotegemewa kufanya na wahuni wa stand.mbunge mtarajiwa akifanya mabo kama haya halafu mpiga kura kama wewe huoni ubaya wake ujue Tanzania imefikia mahali pabaya mno.Utapeli huu ungefanywa na mwanaCCM tungechambua kwa mapana na marefu lakini kwakuwa kafanya Lema tutatafuata maneno matamu kupooza "Kukopeshana & kuvunja mkataba". Duh kazi kweli kweli inahitaji moyo kujisifia eti mimi mtanzania.

  Nilisema tangu mwanzo Lema yuko kibiashara zaidi muda utakuja kuthibitisha maneno yangu.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ngongo natanguliza heshima!

  Nimegundua kuwa wewe ni mwanamageuzi uliye makini sana!
  Nimegundua pia kuwa umechoshwa na chama tawala kama sisi wengine tulivyo!

  LAKINI pia nasikitika kwasababu kazi yako ni kumnanga LEMA kila post unayopandisha hapa ndani, na kueleza mapungufu yake kwa kila lugha unayoweza.
  Bahati mbaya zaidi unashindwa kumtaja mgombea ambaye ni sahihi kwa wanamageuzi wa Arusha!

  Toa altenative, usiwe mtu wa kulaumu tu, which is not very scientific.Be part of solution: kama kama utaendelea kulaumu tu, hata ukifanikiwa kuongea hadi kwa lugha za MALAIKA haitasaidia!
  Tunacholilia ni mageuzi, na si vinginevyo. Kama unaona mgombea wa TLP, au yeyote anafaa, si useme?

  Nimefuatilia sana post zako broda, kwakweli unaishia kutuweka roho juu tu wanajimbo la Arusha Mjini!
  Simtetei Lema kwa unayomtuhumu nayo, lakini mbona wako wengi, ina maana wengine ni MALAIKA?
  STOP BEING BIASED my broda.

  Analysis zako huwa ni makini sana, na huwa napenda kuzisoma, ila jaribu kuwa fair-player!

  RESPECT BRODA!
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mama maimuna kapewa card ya gari iloandikwa jina la mtu mwingine?....Huo umiliki wa kisheria unaouongelea wewe ni upi sasa.

  This is just too LOW
   
 9. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145

  Enyi watu wa ARUSHA HIII Mumeiona na sipindishi wala siongezei kitu naitoa kama nilivyo tumiwa na mdau mmoja toka huko ARUSHA. sasa sielewini nikwa ajiri ya wana Chadema au CCM


  HATUDANGANYIKI
  • Wanadai LEMA hana PHD siyo Msomi! MPE KURA maana arusha siyo chuo kikuu wala hatuitaji mwalimuwa chuo kikuu!TUNAHITAJI MWAKILISHI-anafaa
  • Wanadai mtangao wa LEMA si WAKIMATAIFA! Arusha tunahitaji MBUNGE si waziri wa mambo ya nje KURA YAKO KWA LEMA anafa kuwa mbunge wako
  • Wanadai LEMA kala PESA ya POSITIVE THINKERS wanaolalamika ni MAWAZO,MWALUSAMBA,J MILYA ambao wao ni NEGATIVE THINKERS wa CCM.Wameishiwa SERA wameanza MIPASHO kura yako kwa LEMA tuwamwage!

   KAZI ZAO NINAWAKUMBUSHA

   MILYA-rudi kuuza bar ni kazi yako acha siasa inawenyewe!

   MWALUSAMBA-rudi salon saidiana na mkeo kutengeneza nywele na kuosha kucha za wadada unapendezea huna tofauti na wao

   MAWAZO-rudi kwa baba yako LEMA mwombe msamaha!

   MWISHO nikwa bidhaaa wanayuzwa na CCM arusha mjini!HAIUZIKI vyou vikuuu vinaupungufu wa waalimu katafute ajira!

   TUWAPUUZE na maneno yao CCM!


  Hiindio nilivyo ipata frm Arusha mmmmh mnakazi kweli kweli naona ni majunguzi time
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako PakaJimmy,

  kwanza naomba kukushukuru kwa jinsi unavyochangia hoja unamfanya mtoa hoja kusoma mara mbili kabla ya kujibu natumaini wengine watajisahihisha na kufuata mwelekeo wako.Kabla sijaanza kukujibu naomba usisahau,usidharau,usishawishike tarehe 31/10/2010 kapige kura wewe,mkeo,beki tatu,jirani na marafiki Dr W Slaa anahitaji kura yako ushabiki pekee bila kura ni kazi bure.

  Mkuu nilianza kumpinga Lema siku nyingi hata kabla hajajiunga CHADEMA,alipojiunga nilitoa angalizo kwa chama wawe makini na sababu nikazitaja bila kuongopa,mambo mengi niliyosema yamedhihirika na mbele ya safari mtasikia mengi.

  Mkuu hivi Lema kushikiliwa na polisi kwa kujipatia fedha isivyo halali ni habari zisizotakiwa jamvini ?.Tunatakiwa kuleta habari za kumsifia tu ?.PakaJimmy naamini JF haiko hivyo ila kuna watu wanataka kutulazimisha tuwe hivyo nina hakika mimi,wewe na great thinker wa kweli hawatakubali.Tunategemea CHADEMA kishike madaraka hivi Lema akipewa uwaziri atakuwa na tofauti gani na akina Karamagi ? mtu anyetapeli watu akikabidhiwa dhamana usitarajie ataacha utapeli badala yake tutarajie atakuwa tapeli mkubwa zaidi kwasababu atakuwa na uwanja mzuri na mkubwa wa kufanya utapeli.

  Mkuu unajua Mama Maimuna Rashid ameathirika kiasi gani kwa kutapeliwa na mtu tunayempigania aende mjengoni,unaweza kukuta kashindwa kumpeleka mtoto chuoni hilo hatulioni wala hatutaki kusikia mtu akisema na anayelisema atapewa majina yote mabaya unayoyafahamu na usiyoyafahamu.

  Mkuu chama kinachotarajiwa kuleta mabadiliko lazima kihakikishe kinakuwa na viongozi sahihi[wasafi] ili waweze kusimamia mabadiliko hayo vyema.chama ni watu bila watu hakuna chama, watu wasafi,waadilifu,wabunifu na elimu nzuri ufanya chama kiwe kizuri.Mwl Nyerere aliwahi kusema "Utajiri unaotokana na wizi wa mali ya umma,na wizi wa fedha za kigeni na unyonyaji na uharamia wa aina mbalimbali hautupunguziii umaskini wetu,bali unaongeza.Chama chetu hakiwezi kukubali hali hii na kikaendelea kuwa CCM,na wala kisitazamie kuwa wananchi watakikubali" .Mkuu Pakajimmy CCM imejaa viongozi wabadhirifu wa mali ya umma,wezi,waongo,wasiojali maslahi ya taifa ndiyo maana tulimsikia Chenge akijibu kwa dharau mamilioni aliyoweka kweny account za nje ni vijisenti,tulimsikia Mramba akiwatukana watanzania kwamba ndege ya rais itanunuliwa hata ikibidi tule majani,tulimsikia Lowasa akillalama kaonewa pamoja na kuliingiza taifa hasara kubwa kupitia mradi wake wa Richmond.Hawa ni watu wanaounda ule mkusanyiko wa chama kinachoitwa CCM.CCM kimekuwa chama kibovu kwasababu ya kukumbatia watu wa aina hii,hawakutaka kutenda maonyo ya Mwl Nyerere kimefika mahali ambapo hakikubaliki tena sana sana wanalazimisha kama Kibaki au Mugabe.Mkuu PakaJimmy pamoja na Lowasa,Karamagi,Mramba,Chenge na nk kufanya uharibifu mkubwa lakini bado wana watetezi wengi kuliko unaweza kufikiri.Mkuu PakaJimmy ikiwa CHADEMA wataendelea kulea matapeli tofauti yake na CCM itakuwa haipo matarajio makubwa ya wananchi juu ya hiki chama yatatoweka kama mvuke nasisitiza lazima CHADEMA kichague watu wasafi ili kibaki kuwa chama safi na imara.

  Wapo wapiganaji wengi wazuri ambao nina hakika wakifanikiwa kuingia bungeni hatuataliona pengo la mpiganaji wetu Dr W Slaa mfano mzuri ni mgombea ubunge Arumeru mashariki jina limenitoka anampeleka mbio Mhe Sumary isivyo kawaida kama wizi wa kura ukidhibitiwa nina hakika tutamwona Zitto mwingine mjengoni.Pamoja na kashikashi anazopata Sumary sijasikia mpinzani wake akiandamwa kwa kashfa yoyote eti kwasababu anaelekea kushinda ! .
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ngongo,
  Pamoja na maelezo yako mareeeeeeeeeeeeeefu, Pakajimmy kakuuliza swali jepesi kabisa lakini umelikwepa.
  Narudia kusisitiza swali la PJ na mi mwenyewe nilikuuliza kwenye posti nyingine hapo kabla hukujibu.
  Tunakubaliana na mawazo yako ya kimapinduzi na kimageuzi ya kweli, lakini tunataka uende mbele kidogo, usiishie kuripoti habari mbaya za Lema, tujulishe basi na wagombea wengine wa arusha mjini wana sifa gani? na pengine kwa kuwa Lema hafai, nani basi apewe ubunge hapo arusha mjini? Vinginevyo utaonekana wewe ni "hater" na huna nia wala mchango wowotekatika kuleta mabadiliko ya kweli kwa manufaa ya wana arusha wote. Labda nikushauri tu kama hauna lolote la kutueleza kuhusu wagombea wengine, na hivyo ukabaki kuleta majungu hapa JF kama Maggid, basi taarifa zako tutakuwa tunazitupa kule,....................
  Tupe habari za wengine arife.
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Mwita Maranya,

  Hii ni post ya PakaJimmy sijui kama nahitaji kutoa maelezo zaidi sikumjibu kwakuwa najua aliamua kuchangamsha jamvi.  Re: Kuhusu mTZ anayewania knunua Liverpool

  thread hii ipo, na imeanzishwa leoleo na MwanaArusha namba MOJA, na mwana TLP wa Ukweli, anayekwenda kwa jina la NGONGO!..tafuta uone!
   
Loading...