Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,608
- 93,384
Matola,
Haitakaa itokee,siwezi kumuunga mtu mkono kwa sababu nitakuwa shabiki,au kipofu.Ukitaka kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa Objective utaona umuhimu wa kuunga mkono hoja na si mtu. Kwanza kabisa Hoja yoyote inayosaliti waliomwaga Damu kwa ajili ya haki,makosa ya kikanuni na hila za kisheria na kimamlaka SIWEZI KUIUNGA MKONO KAMWE,Tafakari.
Kuhusu suala la Arusha,Naamini utata uliopo utajadiliwa ndani ya Chama.Kuna wanaoniandikia Inbox tangu juzi.Hili suala ni lazima maamuzi yafanyike kwa kuzingatia uzito wa Damu za watu zilizomwagika,naamini kama ni fursa ya muafaka ilikuwapo hata kabla ya tarehe 5 January,2011...sasa sijui kama CCM waliona busara baada ya kuona Damu ama ni kipi kipya! Ni lazima mazingira yoyote ya muafaka yazingatie conditions zilizolazimisha maandamano ya January 5, Maslahi ya umma kikanuni,kisheria na haki kwa Ujumla ili tuwe na moral Authority ya kutumia nguvu ya umma katika harakati ,so nje ya hapo ni mjadala mwingine na mpana zaidi.Naomba niishie hapo kwa sasa,ilka natoa Rai kwa WanaJF,Wanamapinduzi wa kweli hawafuati mkumbo,tuwe analytical na nahimiza umuhimu wa kuwa na mijadala mikali mikali ili tuwe na solutions ambazo ni practicals.WanaJF ni wachambuzi mmenielewa
Mkuu nimekuelewa pointi zako kimsingi, lakini katika kusimamia ukweli na misimamo lazima ujuwe kusoma nyakati, vilevile huwezi kusimamisha maendeleo ya watu kwa jimbo zima kisa eti ni kulinda maslahi ya CHADEMA, pamoja kwamba naiunga mkono CHADEMA lakini sintokubaliana na kiongozi yeyote yule kutugeuza sisi wananchi kama ndio mtaji wake.
Tuje kwenye ukweli kama swala lilikuwa ni kukiukwa kanuni hili wote tunalifahamu, sasa tupige kura upya je CCM ina kura ngapi? na ikumbukwe miradi mingi ya maendeleo inategemea manispaa, sasa kuna tija ya kuendelea na msimamo ambao utawaumiza zaidi wananchi?
Tuache porojo hakuna jambo zuri litakalofanyika bila katiba mpya na kuing'oa ccm madarakani.
HITIMISHO: Siungi mkono hoja za Lema.