Lema apinga kugawana vyeo, hamtambui naibu meya wala meya wa Arusha (tamko) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema apinga kugawana vyeo, hamtambui naibu meya wala meya wa Arusha (tamko)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Henry Kilewo, Jun 27, 2011.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
  Msingi wa Maendeleo ni Haki.


  "Ninawasalimu wote .

  Hivi karibuni tarehe 21 Juni 2011 siku ya jumatano kuna taarifa nyingi ziliandikwa katika vyombo vya habari kuhusu muafaka dhidi ya mgogoro wa uchaguzi wa umeya uliokuwa unaendelea hapa mjini Arusha .

  Ni kweli kabisa mgogoro wowote humalizwa kwa vikao na mashauriano, na ndivyo ambavyo CHADEMA tumekuwa tukitaka toka awali na mimi binafsi natamani tukae kwa amani katika nchi yenye misingi ya haki na utawala wa kuzingatia sheria. Kimsingi kabisa tulitaka serikali ya CCM itamke kuwa kosa limefanyika kwa kutozingatia kanuni ya uchaguzi wa umeya wa Arusha na kupelekea hapa tulipofika.

  Mchakato wa muafaka ulipoanza mwanzoni mwa mwezi APRILI 2011 ulikuwa na nia ya kuitaka serikali ione makosa hayo na ichukue hatua kwa wahusika waliosababisha kufika katika hali tata tuliyofikia sasa na sio kufarijiana kwa vyeo. Mgawanyo wa nafasi au vyeo ni mapendekezo tu yenye kutaka madiwani wote kushiriki utumishi kwa wananchi lakini haikuwa msingi wa madai yetu.

  Baada ya kufanya utafiti na kufikiria kwa makini juu ya mchakato wa kufikia muafaka huu ndipo nilipogundua pamoja na nia nzuri ya CHADEMA, serikali ya CCM haijachukulia kwa nia na dhati ya kweli ili kutoa majibu ya msingi ya madai yetu kuhusu HAKI na KUZINGATIA KANUNI lakini pia kuonyesha toba na ukiri wa makosa yaliyofanyika ili wananchi waweze kutuelewa.

  Kwa sababu ya muafaka huu kushindwa kutoa majibu ya msingi kwa kweli siwezi kukaa kimya hata kidogo juu ya muafaka huu ambao ni udhalilishaji wa utu wa Mwanadamu na haki kwa kiwango cha hali ya juu sana na katika mambo ya msingi tuliyokuwa tunapinga katika suala la umeya ni ukiukwaji wa haki , taratibu na sheria katika uchaguzi wa umeya uilokuwa umefanyika Arusha Mjini pamoja na sababu nyingine hii ilikuwa ni sababu ya msingi ya kupinga jambo hili hata tukaamua kufanya maandamano tarehe 5/1/2011 yaliyopelekea watu watatu kuuwawa kikatili na polisi na wengine zaidi ya 26 kuhumizwa vibaya huku wakiachwa na vilema vya maisha.

  Hatukupinga utaratibu huo ili tugawane vyeo na nafasi mbali mbali katika manisipaa ya Arusha hili halikuwa lengo letu na kamwe haliwezi kuwa lengo langu .
  Hatukuwa tunampinga Meya wa Arusha kwa dini yake au kabila lake au rangi yake tulipinga mfumo uliomchagua ambao ulikiuka utaratibu wa msingi wa kanuni na sheria za uchaguzi pamoja na mambo mengi yaliyohusu haki na usawa ,ukweli .

  Tulisema Ocd wa Arusha aondolewe na polisi washitakiwe juu ya mauwaji ya watu wasio na hatia na familia zao zilipwe fidia.

  Tulitaka mkurugenzi wa manisipa ya Arusha aondolewe kazini kwa kusimamia uchaguzi batili nakusababisha majonzi mengi na vifo vya raia wasio na hatia.
  Tulitaka uchaguzi wa umeya urudiwe hapa mjini Arusha na haki itendeke na sio kugawana uongozi na mambo mengi ya msingi ambayo kila mtu anajua na hata ulimwengu mzima unajua.

  Hivyo basi siwezi kukubali dhambi hii na udhalimu huu eti tu kwa sababu chadema imepewa unaibu meya kwani huu sio msingi mama wa muafaka na kama suala ni unaibu Meya mbona tulimuona Diwani wa kata ya Sokoni one Mh Kivuyo kuwa ni msaliti alipokuwa ni naibu Meya?

  Ninatambua na ninajua inaweza kuwa vigumu kueleweka katika hili au kupewa tafsiri nyingi nyingi tu, napenda kujiweka wazi kuwa nitasimamia ukweli daima kwa maslahi ya wananchi na niko tayari kusimama na wananchi kukabiliana na upinzani wowote ili kuwatetea maana mimi ni mtumishi wao kwani Haki na utu sio jambo la kupuuza na kujadiliwa kwa vyeo au pesa.

  Mwisho naomba mwenyezi Mungu anisaidie na watu wote wa Arusha mjini na watambue mgogoro hauwezi kuzuia maendeleo ya Arusha Mjini hata kidogo kwani hata bajeti ya 2011 -2012 ilipitishwa bila hata kuzingatia kanuni na taratibu. Kuna wafanyabiashara wachahe wa Arusha wanaoshawishiwa kuwa Haki hii tunayoitafuta inadumaza ukuaji wa biashara zao, napenda kuwaambia kuwa Mgao wa Umeme, Ufisadi, Rushwa, uonevu, kutokufutwa kwa kanuni na Ulaghai wa Serikali iliyopo madarakani ndivyo vinavyodumaza uchumi wa Taifa na Chadema inapambana ili kuhakikisha inajengwa Tanzania Mpya yenye kufuata Kanuni na utaratibu na mfumo wa sheria utakaoleta Neema ya kweli Tanzania.

  Ni nayo ilani yangu kwa wananchi wa Arusha nitatimizakwa mipango yangu na yale ya kisera yanayohusu Nchi nitaendelea kuongea kwa nguvu zote kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutumia vyombo vingine kama Mbunge.

  Na pia niwaombe Madiwani Wafikirie kwa makini utashi wenu dhidi ya jambo hili nimatumaini yangu mtakuwa mlifanya maamuzi kwa haraka sana bila kiuzingatia ukweli.

  Arusha nawaomba sana na mnapaswa kuwa wavumilivu na majasiri wakati huu ambapo tunapita katika majaribu mengi katika kupigania ukweli ,hatuwezi kuudhalisha utu wa mwanadamu na haki kwa kugawana vyeo kwa kisingizio cha maendeleo, Hata hivyo hakuna maendeleo Duniani yanayopita haki ,ukweli , utu , usawa ,na kama kuna mtu yeyote anafikiri anaipenda Nchi yake basi awe mfano wa kufikiria na kutenda Haki .

  Msiogope Mungu yuko pamoja nasi Ukweli utashinda. Mungu Awabariki sana.

  GODBLESS J LEMA ( Mbunge Arusha Mjini )

  …………………..........

  27/6/2011.
   
 2. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Bring it on!
   
 3. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii imekaa njema Mh Godbless Lema,
  Kaza buti mpaka tuambiwe kisa cha kupindisha sheria na kanuni za uchaguzi kulikosababisha vurugu Uchaguzi wa Meya Arusha.
  Na Pinda atueleze kwanini alitudanganya pale mjengoni,sio kwamba aliwadanganya wabunge tuu,alinidanganya mimi mtanzania
  mwenye haki ya kupata ukweli kuhusu maendeleo ya nchi yangu.

  Ndugu zangu wamekufa kwa sababu ya yale maandamano,kwahiyo tunataka kujua ukweli.
   
 4. T

  Technology JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Lema: During your life, never stop dreaming. No one can take away your dreams
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  kAULI ILIYOSIMAMA...HII inatoka mdomoni mwa Lema Live, haijaongezwa au kupunguzwa neno!
  Kuna watu hapa ndani baada ya kusoma habari kuwa CDM wamekubaliana kuingia muafaka na ccm, walisema kuwa lazima Godbless Lema atatoa kAuli, na hakika ndiyo hii hapa!
  Jamani, jamaa ameeleweka, hasa kwa hoja kuu kuwa ishu si kugawana vyeo!
  Spport you pal, hali ni tata sana mjini hapa, there was no way!
   
 6. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wooow!! It is fantastic. Bravo Mhe Godbless Lema hakika wewe ni kamanda wa Ukweli. ARUSHA itajengwa na watu jasiri kama wewe na sisi unaotuongoza. Regia Mtema umesikia mwanaume kaunguruma sio wewe kufuata walichosema wenzako.
  GODBLESS LEMA, U WILL NEVER WALK ALONE. TOGETHER AS 1. BIG UP KAMANDA LEMA.
   
 7. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa yuko sahihi, kwani lazima vitu vya msingi viwekwe wazi ili waliopoteza ndugu zao wasije kujutia maamuzi ya kuunga mkono CHADEMA, ukiwa muwazi hutatengeneza majuto, Bigup Mhe. Lema
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mhhh........! Though Men are nearly always willing to believe what they wish. There is nothing more dreadful than the habit of doubt. Doubt separates people. It is a poison that disintegrates friendships and breaks up pleasant relations. It is a thorn that irritates and hurts; it is a sword that kills-Budha

  Na Pia....Dhamira, Utashi na matamanio ya jambo fulani huchanganyika kama Rangi za upinde wa Mvua.

   
 9. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,315
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Heko Lema. Labda CDM watueleze huo unaibu meya wameupata kwa uchaguzi upi wakati wao ndio walisema uchaguzi ulikiuka kanuni.
   
 10. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  huo muafaka ilikua kati ya nani na nani?, viongozi chadema hawakuhusika? Lema je?, alikua wapi?, tamko hili ni la chadema au lema!, sijaelewa kabisaaaaa!
   
 11. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  umma utashinda
   
 12. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kumbe Mh Lema ni kifaa, duh.....! Watakoma na pipi, pipi zao lakini watagonga ukuta. Komaa nao Lema haya mambo ya kupindisha sheria na kuziacha chini ya mvungu hatutaki. Tunataka sheria zifanye kazi sio kubabaishana.
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwani huo muafaka ulifanyika bila kushirikisha Chadema? Mbona kuna kugeuka tena?
   
 14. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nilihoji Sana hapa Jamvini juu ya Muafaka huu una Uhalali na Maslahi gani kwa wananchi wa Arusha lakini nikaishia kuitwa Mwanaharakati Mmbeya,Mchonganishi, Gaidi tena niliitwa hivyo na REGIA MTEMA MB Viti Maalum CDM. Sasa niliyonena yametimia wanaoweza kusimama kwa miguu yao wanajidhiirisha na wanaofuata mkumbo wa viongozi wao wameonekana.
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Labda naomba tu mnielimishe CCM ina wapiga kura wangapi na CHADEMA inawapiga kura wangapi? naomba jibu ili nifanye mahesabu yangu ya kumuunga mkono Lema kumpinga.
   
 16. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huo ndio kamanda wa ukweli hayupo kwa ajili ya Chama bali ameweka Taifa na wananchi mbele kuliko chama. Hongeara Lema kwa kutambua hivyo
   
 17. i

  ichawinga Member

  #17
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii nzuri mh. LEMA tupo pamoja sas naamimini watu wa arusha walichagua mwakilishi hodari na sio hodari mwakilishi big up A. town, na nawaomba muendelee hivyo hivyo wamesubiri watu wamekufa ndio wanakuja na muafaka, 2natka haki itendeke wale wote waliosababisha mauaji ya watu wasio na hatia wasurubishwe na wao safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii sana mh. Lema.
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Mrema alihama CCM baada ya kutokubaliana na maamuzi ya serikali, kwahiyo nategemea Lema kama hakubaliani na maamuzi ya chama chake basi tunahitaji kumsikia anajiondoa ndani ya CHADEMA.
  Hayo ndio maamuzi pekee ya mtu mwenye msimamo, kinyume cha hapo mimi nitamuhesabu kama mvuta bangi tu na hana lolote zaidi ya kufuta cheap popurality.
   
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  nilikuwa naangali ile documentary ya arusha hapa....kweli ningeshangaa sana kuona lema analowanisha msomamo ghafla namna hii.....
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Lema nina hakika kuwa upo sahihi kwenye hili. CHADEMA msijidanganye kuwa mtu mmoja au wawili wanaweza kukaa chini kwa niaba ya wananchi wanaowaunga mkono na kutoa maamuzi kama yaliyofikiwa Arusha.

  Kama ni Umeya achaneni nao simamieni haki, CCM walikuwa wameisha wa-fix kwenye hili it was a matter of time tu wangeanza kuli-spin na kumomonyoa support ya wananchi juu yenu. Kama nilivyosema hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/147581-mwafaka-wa-umeya-wa-arusha-wapatikana-6.html#post2127305 CHADEMA wajue kuwa wananchi wa Arusha na maeneo mengi Tanzania hawataki muafaka na CCM, kwani waliisha wakataa kwenye sanduku la kura japo hawasikilizwi matakwa yao kwa CCM kutumia dola kunng'ang'ania kuwatawala. Wananchi wanataka kuondokana na CCM, any deal which led to the continuation of CCM will only serve well to the CCM. Huwezi kuvunja sheria mpaka kufikia kupotezea watu uhai wao halafu, mwisho wa siku unakuja kulazimisha mazungumzo na muafaka wa kupeana ulaji, Jifunzeni kutoka CUF, wamejikaanga kwa mafuta yao. This was a big victory to CCM towards dismantling CDM.

  Waachieni Umeya wao, hakikisheni mnasimamia utaratibu kufuatwa na kuhakikisha wauaji wana-face the legal action. Huwezi kutengeneza documentary, inayosikika afisa wa polisi akisema "Aje Killer mara moja aje killer", halafu ipite hivi hivi. Ni bora mgogoro uendelee mpaka 2015 kuliko ku-BOW kwa kupewa unaibu meya. Hongera Lema ninataka na Mbowe naye aliyekaa na counterparty wake Pinda atoe kauli kama hii bungeni. Kuwa hakuna muafaka uliofikiwa au utaofikiwa bila a, b ,c niliyotaja hapo juu. Otherwise this is the beginning of the end of the strong support for Chamema nationalwise and particularly in Arusha. Wananchi wana imani na ninyi, wakikata tamaa wataacha kuja kwenye maandamano yenu.
   
Loading...