Lema apinga kugawana vyeo, hamtambui naibu meya wala meya wa Arusha (tamko)

Matola,

Haitakaa itokee,siwezi kumuunga mtu mkono kwa sababu nitakuwa shabiki,au kipofu.Ukitaka kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa Objective utaona umuhimu wa kuunga mkono hoja na si mtu. Kwanza kabisa Hoja yoyote inayosaliti waliomwaga Damu kwa ajili ya haki,makosa ya kikanuni na hila za kisheria na kimamlaka SIWEZI KUIUNGA MKONO KAMWE,Tafakari.

Kuhusu suala la Arusha,Naamini utata uliopo utajadiliwa ndani ya Chama.Kuna wanaoniandikia Inbox tangu juzi.Hili suala ni lazima maamuzi yafanyike kwa kuzingatia uzito wa Damu za watu zilizomwagika,naamini kama ni fursa ya muafaka ilikuwapo hata kabla ya tarehe 5 January,2011...sasa sijui kama CCM waliona busara baada ya kuona Damu ama ni kipi kipya! Ni lazima mazingira yoyote ya muafaka yazingatie conditions zilizolazimisha maandamano ya January 5, Maslahi ya umma kikanuni,kisheria na haki kwa Ujumla ili tuwe na moral Authority ya kutumia nguvu ya umma katika harakati ,so nje ya hapo ni mjadala mwingine na mpana zaidi.Naomba niishie hapo kwa sasa,ilka natoa Rai kwa WanaJF,Wanamapinduzi wa kweli hawafuati mkumbo,tuwe analytical na nahimiza umuhimu wa kuwa na mijadala mikali mikali ili tuwe na solutions ambazo ni practicals.WanaJF ni wachambuzi mmenielewa

Mkuu nimekuelewa pointi zako kimsingi, lakini katika kusimamia ukweli na misimamo lazima ujuwe kusoma nyakati, vilevile huwezi kusimamisha maendeleo ya watu kwa jimbo zima kisa eti ni kulinda maslahi ya CHADEMA, pamoja kwamba naiunga mkono CHADEMA lakini sintokubaliana na kiongozi yeyote yule kutugeuza sisi wananchi kama ndio mtaji wake.
Tuje kwenye ukweli kama swala lilikuwa ni kukiukwa kanuni hili wote tunalifahamu, sasa tupige kura upya je CCM ina kura ngapi? na ikumbukwe miradi mingi ya maendeleo inategemea manispaa, sasa kuna tija ya kuendelea na msimamo ambao utawaumiza zaidi wananchi?
Tuache porojo hakuna jambo zuri litakalofanyika bila katiba mpya na kuing'oa ccm madarakani.
HITIMISHO: Siungi mkono hoja za Lema.
 
Watu wamepigania nchi hii kwa muda mrefu sana makamanda wamesimama imara bila kuyumba jana niliongea sana kuhusu makubaliano batili kamanda Lema umesimama imara kama kuna madiwani wamechoka harakati watupishe tena mapema sana hoja ni haki si nani awe meya
 
MATOLA .Issue siyo nani kashinda, hapa issue ni mfumo wa uchaguzi ulikuwa mchafu, ukasababisha vurugu na mauaji, sasa uchaguzi urudiwe haijalishi hatakama ccm wakishinda, lakini iwe halali, kisha wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine katika issue nzima wawajibishwe. mkurugenzi wa jiji, kamanda wa polisi mkoa n.k
 
Mkuu nimekuelewa pointi zako kimsingi, lakini katika kusimamia ukweli na misimamo lazima ujuwe kusoma nyakati, vilevile huwezi kusimamisha maendeleo ya watu kwa jimbo zima kisa eti ni kulinda maslahi ya CHADEMA, pamoja kwamba naiunga mkono CHADEMA lakini sintokubaliana na kiongozi yeyote yule kutugeuza sisi wananchi kama ndio mtaji wake.
Tuje kwenye ukweli kama swala lilikuwa ni kukiukwa kanuni hili wote tunalifahamu, sasa tupige kura upya je CCM ina kura ngapi? na ikumbukwe miradi mingi ya maendeleo inategemea manispaa, sasa kuna tija ya kuendelea na msimamo ambao utawaumiza zaidi wananchi?
Tuache porojo hakuna jambo zuri litakalofanyika bila katiba mpya na kuing'oa ccm madarakani.
HITIMISHO: Siungi mkono hoja za Lema.

Matola,

Nashukuru sana.Tuko pamoja kihoja.Kuna wanaonilazimisha nitoe majibu ya hii taarifa,sasa nimewaomba/nimewajibu wamuandikie aliyeleta hii thread
Nashukuru hapo kwenye Red,umeelewa Msimamo wangu kuhusu siasa,watu,Utu,Thamani ya nguvu ya umma katika kulipia gharama ya haki,wajibu,sheria na mazoezi mazito ya kidemokrasia.Damu ya watu haina compromise unless kile ulichotaka umekipata.

Tafadhali naomba wasomi wa kweli mjiunge kwa wingi na vyama vya siasa,tusimamie haki hata kama ni kwa upanga kama last Resort.Vinginevyo tuataendelea kushuhudia mashambulizi dhidi ya demokrasia,matumizi mabaya ya Dola na wafuasi wa Democracy na haki..kama watu walikuwa tayari kufa kwa ajili ya haki basi hakuna sababu ya kufanya makubaliano laini.Ni lazima tuepuke mitego ya kusaliti trust itokanayo na mtaji wa nguvu ya Umma

Wasomi wengi jiungeni na vyama vya siasa,ili tuokoe demokrasia,ili tustawi katika kivuli cha Demokrasia..vinginevyo vyama vya siasa vikishindwa sote tutawajibika hasa pale haki itakapotafutwa kwa njia ya Upanga wa moto.Demokrasia ya vyama vingi ikishindwa,basi wale ambao hatupendi umateka wa fikra,kuburuzwa,kufuata mkumbo,kushabikia,kujipendekeza,tunaotaka haki kwa gharama yoyote basi tujiandae kwa safari ya misitu ya Uluguru,Mikumi,Rongai, ili kujikomboa sisi na watanzania kwa ujumla.Itakuwa ni safari ya Sierra Maestro.Basi ni matamanio yangu tusifike huko na nitajitihadi/tujitahidi kadiri ya uwezo wetu ingawa niko tayari tusifike huko.Asante
 
Mh! Kambale wako wengi CHADEMA. Kila mtu ana sharubu chama kile. Tamko hili lilipaswa kutolewa na Mwenyekiti Mbowe au KM Dr Slaa. Vinginevyo tutafute definition sahihi ya DEMOCRACY, UWAJIBIKAJI WA PAMOJA, UTAWALA wa SHERIA na mambo kama hayo.

Lema ameongea kama mbunge na si CHADEMA, na hiyo ndiyo demokrasia ya kweli. Nafasi ya kwanza ni kuwatumikia wapiga kura wako, chama kinafuatia baadae, sualala uwajibikaji wa pamoja hiyo ni dhana inayotumiwa na cabinet (iliyopo madarakani), Mnakaa pamoja mnafanya debate na mwisho wa siku mnaamua ama CEO (President) ana rule out the outcome. Chadema si chama tawala, uwajibaki wa pamoja unakuja pale chama kinapotoa National policy ikija kwenye local politics kila local leader anawajibika kwa constituents wake.

Si Mbowe wala Slaa mwenye kuweza kuwa na veto ya kuwaamulia wananchi wa Arusha mjini, bali mbunge wao na wananchi wenyewe wataamua la kufanya kwa support ya chama. Kama hili limefanyika is the good step towards the strength of CDM, kuwa chama ni wananchi si viongozi. Priority ni wananchi si watu binafsi, huwezi kuja na muafaka simple wa kufukia damu za wahanga kwa mchanga baada ya kupoteza maisha ya watu, ni lazima wauaji washitakiwe. Hii precendence iliyojengwa na CCM na CUF kuwa vunja sheria sasa then tutakaa mezani baadae haijengi nchi, demokrasia na haki, bali ni kudumaza demokrasia na utawala wa haki na sheria.

Kuwalazimisha wafuasi wenu wafanye yale waliyoyakaa kutoka upande wa pili ni kuwapatia upande wa pili legitimacy. Chadema kama taasisi, ijifunze kuwa taasisi hiyo si Mbowe, Mtei, Slaa, Zito et al bali ni wafuasi na wapenda mabadiliko wao ni stewards tu. Wasijipatie uwezo wasiokuwa nao kwani wakifanya hivyo wataupoteza hata walio nao leo.

Mimi sina chama chochote japo I used to have a CCM card long time ago, ambayo niliipotezea mbali long time, ila nimevutiwa na utendaji wa CDM katika kuwaamsha wenye nyumba kwa kelele zao za mlango. Hawa jamaa wa CCM wamezoea kulala hivyo msiache mlango ukafungwa endeleeni kuuchezea wasipate usingizi mpaka wafanye kile walichostahili kukifanya 50 years ago, vinginevyo mtatufanya tukose alternative 2015, ambalo ni lengo la CCM kwenye hii miafaka uchwara.
 
Lema amekuwa akishuhudia jinsi Mhe Zito, Chairman Mbowe wanavyotoa press releases kuhusiana na mambo mbalimbali.
Ameona huu ni wakati muafaka na yeye aonekane kuwa yupo, anaweza kutoa tamko...ndo maana amemwaga hayo maji-taka hapo.
CHEAP UNETHICAL POPULARITY.
Shame on you Lema. You are a disgrace to Arusha people.

Fair comment, kwa standard yako, the lowest ever!
 
Mimi nadhani sasa kama kuna watu wanaotaka kanuni zote na haki zote zipatikane natoa hoja kwamba waanze na Kikwete kumtoa madarakani, maana CHADEMA inapinga mfumo uliomuweka madarakani.
Nasisitiza Lema ni bangi zinamsumbuwa, hatuwezi kukaa na ajenda moja kila siku wakati yeye anatumbuwa marupumarupu jimboni. zamani kabla sijajuwa maslahi ya wabunge nilikuwa rahisi kudanganywa na hawa wanafki lakini sio sasa, sidanganyiki ng'ooooo!
 
Kama ungekuwa na uchungu na watanzania wenzako waliouwawa tarehe 5 january pasipokuwa na hatia yoyote, basi ungeielewa hoja ya Lema.

Kama ungekuwa unatambua ni kiasi gani familia na wategemezi wa watanzania waliouwawa wanateseka kwa kuwakosa wapendwa wao, basi ungeona mantiki ya hoja ya Lema.

Kama ungejiruhusu kuangalia kwa mapana kwamba muafaka uliofikiwa ni kwa maslahi ya watu wachache kugawana vyeo na si kwa maslahi ya maendeleo na haki kwa wanaarusha, basi ungeona uzito wa hoja ya Lema.

Na kama ndugu yako ndiye angekuwa aliuwawa tarehe 5 january na muafaka hauzungumzi kitu chochote kuhusiana na kuwajibishwa kwa waliouwa na waliosababisha mauaji, na muafaka hauzungumzii ni kwa namna gani familia za waathirika wa mauaji hao zitaweza kusaidiwa kukabilana na maisha na maendeleo yao binafsi, basi usingemuona Lema kwa miwani ya kuvuta bangi.

Hata hivyo ni bora kuwa na mbunge mvuta bangi anayejali maslahi ya watu wake na kuyasimamia kuliko kuwa na mbunge mnywa bia asiyejua wananchi waliomchagua wanataka nini na yeye kusimamia maslahi yao hata kama kuna viongozi wachache ndani ya chama chake ama nje ya chama chake hawakubaliani nae. Maslahi ya wananchi kwanza then vyama baadae!!
 
MATOLA .Issue siyo nani kashinda, hapa issue ni mfumo wa uchaguzi ulikuwa mchafu, ukasababisha vurugu na mauaji, sasa uchaguzi urudiwe haijalishi hatakama ccm wakishinda, lakini iwe halali, kisha wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine katika issue nzima wawajibishwe. mkurugenzi wa jiji, kamanda wa polisi mkoa n.k

Mimi ningeuona muafaka umezingatia maslahi ya wanaarusha kama ungesisitiza kuzingatiwa kwa kanuni na sheria za uchaguzi. Na katika kuzingatia kanuni na sheria za uchaguzi wa meya wa arusha suluhu ilikuwa niu kurudiwa kwa uchyaguzi ili hata kama nafasi ya meya na naibu meya zingechukuliwa na ccm ama chadema, ama mojawapo kwenda tlpm bado ingekuwa ni sawa maadam utaratibu na kanuni za uchaguzi zimezingatiwa, kinyume na hapo huo muafaka ni feki wala haujazingatia maslahi ya wananchi wa arusha na maendeleo yao.
 
Kama ungekuwa na uchungu na watanzania wenzako waliouwawa tarehe 5 january pasipokuwa na hatia yoyote, basi ungeielewa hoja ya Lema.

Kama ungekuwa unatambua ni kiasi gani familia na wategemezi wa watanzania waliouwawa wanateseka kwa kuwakosa wapendwa wao, basi ungeona mantiki ya hoja ya Lema.

Kama ungejiruhusu kuangalia kwa mapana kwamba muafaka uliofikiwa ni kwa maslahi ya watu wachache kugawana vyeo na si kwa maslahi ya maendeleo na haki kwa wanaarusha, basi ungeona uzito wa hoja ya Lema.

Na kama ndugu yako ndiye angekuwa aliuwawa tarehe 5 january na muafaka hauzungumzi kitu chochote kuhusiana na kuwajibishwa kwa waliouwa na waliosababisha mauaji, na muafaka hauzungumzii ni kwa namna gani familia za waathirika wa mauaji hao zitaweza kusaidiwa kukabilana na maisha na maendeleo yao binafsi, basi usingemuona Lema kwa miwani ya kuvuta bangi.

Hata hivyo ni bora kuwa na mbunge mvuta bangi anayejali maslahi ya watu wake na kuyasimamia kuliko kuwa na mbunge mnywa bia asiyejua wananchi waliomchagua wanataka nini na yeye kusimamia maslahi yao hata kama kuna viongozi wachache ndani ya chama chake ama nje ya chama chake hawakubaliani nae. Maslahi ya wananchi kwanza then vyama baadae!!

Unafaa sana kujiunga na harakati za JIHAD, unaposhindana na adui sio vibaya kubadili strategy then ndio unaatack. siasa ambazo hazina macho ni siasa za kitoto.
Napinga kwa nguvu zote misimamo ya kipumbavu ya huyu Lema, na kama Lema mnamuita shujaa kwa upuuzi huu, basi neno shujaa limepata tafsiri mpya hapa Tanzania.
Kwa wale wataalamu wa maandishi hebu nisaidieni, hizo fonts alizotumia Lema kwenye hii taarifa yake kwa vyombo vya habari kweli huyu mtu ana angalau know how ya computer? kwa sababu kwa ufahamu wangu fonts zinazotumika kiofisi mara nyingi ni Tahoma size ni 24. ebu tuijadili na akili yake vilevile.
 
Hii ndiyo demokrasia ya kweli kwamba hata ndani ya chama cha siasa mtu mmoja mmoja (awe mwanachama wa kawaida au kiongozi) anaweza kuwa na mtamazamo tofauti juu ya kile anachoona hakina maslahi wa watu anaowawakilisha. Godbless Lema anawakilisha watu wa Arusha mjini, na uchaguzi wa mayor wa Arusha mjini ulifanyika kinyume na taratibu zilizowekwa kisheria.

Katika kudai sheria/haki itendeke makosa makubwa yamefanywa na vyombo vya dola na kusababisha vifo vya raia watatu wasio na hatia (watanzani 2 na mkenya mmoja). Mpaka hapa Lema anakuwa na haki ya kuliongelea swala ya mayor wa Arusha kuliko kiongozi mwingine yeyote kwa sababu yeye ndiye watu wamemtuma awawakilishe. Na kwa press release yake hii ni kwamba wana-Arusha mjini wanasema (categorically) walichodai na wanachoendelea kudai ni utawala wa sheria. basi.

Viongozi wetu wengi wamukuwa na kasumba mbaya sana, mara nyingi wamekuwa wanafanya maamuzi, na hata kuungana na itikadi za vyama vyao huku wakisahau wapo kwa ajili ya kuwakilisha wapiga kura wao na sio chama au itikadi fulani. Kama wananchi wanasema tunataka sheria ifuatwe, huwezi hata siku moja kama kweli wewe ni mwakilishi wao kukubaliana na hoja zinazovunja sheria hizo hizo watu waliokutuma kutunza. Na hili liko kwa vyama vyote ila CHADEMA wanaonekana kuwa na ngozi ngumu inayoruhusu demokrasia ya kweli.

Na huu utaratibu wa kugawana vyeo kati ya winners & loosers umeota sugu Africa, na naweza kusema inaondoa maana halisi ya uchaguzi au hata demokrasia. LOOSERS wanatakiwa waende nyumbani sio kupewa cheo! Lakini sasa tunaona tafsiri ya neno looser au kushindwa' linapewa maana nyingine.

CHADEMA sasa mnatikiwa muoneshe njia ni vipi chama cha siasa kinaweza kukabiliana na mitazamo na maamuzi toafauti ndani ya chama bila ya kuingiza kasumba ya 'kuzibana midogo'.
 
honestly i was shocked to learn that some people congratulated that truce! ukweli ni kwamba CHADEMA deserved more that 'just' unaibu meya...ulisema lema ndo yamsingi...Songa mbele lema.God bless you zaidi
 
Kiukweli Lema yupo sahihi kabisa hili swala la Chadema kugawana vyeo na hao ccm utakuwa ni usaliti mkubwa sana.Binafsi sipingi muafaka ila muafaka wenyewe lazima uzingatie haki kwanza na sio huu wakugawana ulaji ilihali kuna Watu waliuawa na wengine kupewa ulemavu wa Maisha.Viongozi wa juu wa Cdm Watoe ufafanuzi wa hili coz habari ya hili swala tunasoma Magazetini tu hatujasikia kauli.
 
Nashukuru Mjadala umenoga humu ndani lakini tunapaswa tupate majibu ya haya yafuatayo ambayo hayajajibiwa hadi sasa.

1.Uwiano wa madiwani kati ya CCM na CDM ukoje ukiweka kando TLP (Japo anaonekana kuwa na influence pia kwa pande zote)?

2.Maamuzi ya kumaliza mgogoro yana baraka za nani kati ya madiwani wenyewe (manispaa) na Viongozi wa CDM? Maake toka taarifa ya muafaka itolewe,hakuna kiongozi wa juu wa CDM aliyepinga isipokuwa Dr. Slaa aliwahi kutoa taarifa kuwa mgogoro upo katika hatua za awali za utatuzi.

3.Lema hana Veto katika council kwani ni mjumbe mwenye single vote kama wenzake,vilvile yeye si mwakilishi zaidi ya wenzie ambao mbali na kutoka kwa wananchi hao hao anaodai Lema pia maamuzi yao ya kufuta mgogoro yamekuwa ya pamoja kwa maana ya collective responsibility (ushahidi ni kupigiwa kura).Hapa napata wasiwasi ni aje Lema(pekee) anauchungu kuliko madiwani zaidi ya 14 wa CDM?

MAONI:Lema anaumizwa na mengi zaidi ya Wanachi anaowawakilisha kwani amekuwa mstari wa mbele kumsakama Meya aliyepo wakati mwingine hata katika misiba tena hadharani.Kwa hali hii,inakuwa ngumu kwake kuyatafuna matapishi yake kwa maana kumkubali Meya na kuhudhuria vikao vya Council tena kwa nidhamu kama inavyopaswa huku Meya akiwa katika kiti cha enzi!

Inapohitajika busara kutumika huwa haitizami wangapi wamekufa ama vilema.Kwa mtizamo wa LEMA basi Wahutu na Watusi wasingekaa leo kwa pamoja na kuendeleza nchi yao.
 
Ili kujua msingi wa msimamo wa mtu kwenye suala kama hili mi lazima tuelewe Siku zote kwenye bargaining ni lazima uangalie Uimeleta nini mezani na umepata nini at the end, ilikuwa ni udhalimu vs haki,CCM vs Chadema,Unaibu Meya vs Damu iliyoimwagika katika mchakato wa kudai haki(kwa mazingira yanayojadilika hata hivyo hii ni ajenda nyingine) inorder/respectively/sequently
 
Ulikua kati ya chama cha majambazi na chama cha magamba,Lema hakustahil kuhusika mana c wamagamba, na tamko hl ni la cdm kupitia mbunge wa Arusha Godbless Lema, una swali lingine?
 
Lema kaza buti usikubali kununuliwa simamia haki daima na MWENYEZ MUNGU ATAKUSAIDIA, hao wanaokuita mvutabani hawajaonja joto la uongozi wa kufoji
 
Ulikua kati ya chama cha majambazi na chama cha magamba,Lema hakustahil kuhusika mana c wamagamba, na tamko hl ni la cdm kupitia mbunge wa Arusha Godbless Lema, una swali lingine?

Jifunze kusoma kwanza ndio uwe unacomment, kwa sababu nina uhakika hata wewe mwenyewe ulichokiandika ukiambiwa usome na bado hautoelewa umeandika nini, huu ni utoto sio lazima uchangie.
 
Lema kaza buti usikubali kununuliwa simamia haki daima na MWENYEZ MUNGU ATAKUSAIDIA, hao wanaokuita mvutabangi hawajaonja joto la uongozi wa kufoji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom