Lema 'anasakwa' Jijini Arusha

Lema 'anasakwa' Jijini Arusha

Chadema wanatumia nguvu kubwa Arusha wanafikiri nchi inaongozwa kwa kushinda Arusha!
 
Awareness. Watu wameshajua nini kinatakiwa. Lema sio jembe tu bali sururu hah hah
 
kumbe na wewe hujui?mpango mzima ni kuwaandikisha wale ambao mlengo wao unajulikana wa kifisadi zaidi na ni kwa nchi nzima angalieni sana ikibidi iwe mapema kieleweke tuanze na watendaji watuandikishe hatuwaombi! ni haki yetu wanajua wamepitwa na wakati wanakumbukumbu ya 2010 asilimia 52 ya wa tz. wakaamua kusingizia kwamba hawakupiga kura!kumbe wapi!!!
 
Chadema wanatumia nguvu kubwa Arusha wanafikiri nchi inaongozwa kwa kushinda Arusha!

Hata mto Rufiji umeamza kwa kuchangiwa maji na vijito vidogo vidogo bali huko unakomalizia ni mkubwa mno.

Mto wa upinzani halikadhalika umeanza hivyo,hatimaye unazidi kuwa mkubwa. Arusha, mbeya,kigoma,iringa,Dar,Mara,mpanda, kilimanjaro,Karatu,Zanzibar,pemba,mtwara....
 
huyu jamaa alishazoea kusakwa na polisi kwahiyo si ajabu kwetu kusikia akitafutwa na polisi
 
huyu jamaa alishazoea kusakwa na polisi kwahiyo si ajabu kwetu kusikia akitafutwa na polisi

Mmbea mpe heading tu, story atatunga mwenyewe, lol mkuu usiwe unaishia kwenye heading tu
 
Huyu ndo professor, mbunifu sana. Hapo wa kwanza kusoma watakuwa ni magamba na mapolisi.
 
Mtaa wa Bondeni mjini kati ni mtaa wa CCM utake usitake.

si mtaa tu mji wote kwa sasa wamemchoka Lema, wanataka mbunge mwenye kujitambua, lema anafanya mambo yake kitoto mno angalia sasa hilo tangazo very childish, huyu jamaa hakui tu
 
Hapo wanamaanisha anatafutwa Mtu wa CALIBRE ya Mh. Lema nasi kumaanisha Lema anataftwa na polis
Tangia jana katika mitaa ya Jiji la Arusha na viunga vyake, yametapakaa mabandiko ya kuhamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika Uchaguzi zw Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14, 2014.

Moja ya mabandiko hayo ambayo mengine huwekwa kama stika kwenye magari yana heading kubwa "ANATAFUTWA" halafu chini yake kuna picha kubwa ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ikifuatiwa na maelezo ya namna uchaguzi huo utakavyofanyika kuanzia kuchukua fomu kwa wagombea, kujiandikisha wapigakura na hatimaye kupiga kura.

Tathmini yangu ya haraka imeonesha mbunifu wa "tangazo" hili ambalo liko kwenye standard ya juu in terms of quality ameweza kufikisha ujumbe tarajiwa kwasababu wananchi wengi wanashtuka kuona Mbunge Jijini wao ANATAFUTWA na hivyo kujikuta wakivutika kusoma kilichomo. Mbunifu huyu ameweza kusoma vyema uvivu wa watanzania na kupata mahali pa kuwakamata vizuri.

Tafiti yangu imenijuza pia kuwa ubunifu huu wa watu wa Chadema umefikiwa baada ya kugundua wanachodai kuwa ni hila za CCM na Serekali yake kuficha baadhi ya taarifa muhimu kwa umma kuhusu uchaguzi huo ili wao waishie kujuzana na wanaCCM pekee kama moja ya mbinu za kujaribu kujiokoa na uwezekano mkubwa wa kukataliwa na wananchi katika uchaguzi huu. Mambo mengi yanaonekana kwenda kibubububu wakati tarehe zimeshafika..!

View attachment 203489Mh Lema akiwa kwenye safari zake mitaa ya Jii la Arusha. Unaweza kuona gari yake inalo bandiko hilo pia
View attachment 203491bandiko lenyewe hili hapa
 
Chadema ni Chama Makini sijapata ona...

Hongera Jemedari Lema pamoja na timu nzima ya Makamanda hapo Arusha..
 
Lema amemuiga mdogo wake Sheikh Yahya aliyeibuni hii 2010

attachment.php
 
Back
Top Bottom