Lema 'anasakwa' Jijini Arusha

Lema 'anasakwa' Jijini Arusha

GanjaPlanter

Senior Member
Joined
May 27, 2014
Posts
117
Reaction score
119
Tangia jana katika mitaa ya Jiji la Arusha na viunga vyake, yametapakaa mabandiko ya kuhamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika Uchaguzi zw Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14, 2014.

Moja ya mabandiko hayo ambayo mengine huwekwa kama stika kwenye magari yana heading kubwa "ANATAFUTWA" halafu chini yake kuna picha kubwa ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ikifuatiwa na maelezo ya namna uchaguzi huo utakavyofanyika kuanzia kuchukua fomu kwa wagombea, kujiandikisha wapigakura na hatimaye kupiga kura.

Tathmini yangu ya haraka imeonesha mbunifu wa "tangazo" hili ambalo liko kwenye standard ya juu in terms of quality ameweza kufikisha ujumbe tarajiwa kwasababu wananchi wengi wanashtuka kuona Mbunge Jijini wao ANATAFUTWA na hivyo kujikuta wakivutika kusoma kilichomo. Mbunifu huyu ameweza kusoma vyema uvivu wa watanzania na kupata mahali pa kuwakamata vizuri.

Tafiti yangu imenijuza pia kuwa ubunifu huu wa watu wa Chadema umefikiwa baada ya kugundua wanachodai kuwa ni hila za CCM na Serekali yake kuficha baadhi ya taarifa muhimu kwa umma kuhusu uchaguzi huo ili wao waishie kujuzana na wanaCCM pekee kama moja ya mbinu za kujaribu kujiokoa na uwezekano mkubwa wa kukataliwa na wananchi katika uchaguzi huu. Mambo mengi yanaonekana kwenda kibubububu wakati tarehe zimeshafika..!

IMG_20141118_101238.jpg Mh Lema akiwa kwenye safari zake mitaa ya Jii la Arusha. Unaweza kuona gari yake inalo bandiko hilo pia
10806888_10205591955104519_1411031258_n.jpg bandiko lenyewe hili hapa
 
uongozi wa arusha hoples kabisa wanasumbuliwa na kajitu kama lema mtu mdogo sana kama piliton
 
Mkuu, na chakufurahisha mpaka sasa, chombo kimoja cha kuaminika kinatuabarisha kuwa "TANGAZO TAJWA HAPO JUU LIMESOMWA NA WANA WA ARUSHA WASIOPUNGUA 85%) to kea jana mpaka leo.
 
Mkuu, na chakufurahisha mpaka sasa, chombo kimoja cha kuaminika kinatuabarisha kuwa "TANGAZO TAJWA HAPO JUU LIMESOMWA NA WANA WA ARUSHA WASIOPUNGUA 85%) to kea jana mpaka leo.

CCM sijawasikia kabisa hapa mjini... mara ya mwisho ni wakati ule wananunua watu wa kugombea upande wao...
 
kwa kweli hata mm wakati napita stand nilistushwa na kichwa cha habari Anatafutwa nikajikuta nasoma
 
Ccm wakipata mtaa mmoja Arusha wameiba. Chadema wamejipanga
 
Hamasa inatia moyo na kutukumbusha wajibu wetu hapo 23/11
 
Nimepita kwenye stationery moja ya gamba hapa mwanga mjini nikamkuta kamanda henry kileo akitengeneza bango kama hilo hilo! Hofu yangu huyo gamba atakoma kwa magamba wenzake sema tu huyo gamba ni shida wenyewe wanamagamba wanamgwaya kinoma
Ccm wakipata mtaa mmoja Arusha wameiba. Chadema wamejipanga
 
Hata miye nimeshtuka sana nilipoona heading tu sasa nikajiuliza, Lema kawaje tena Mungu wangu!! Hii ni Nzuri sana, ningefurahi sana kama mikoa yote ingeiga ubunifu huu.
 
Hii inanikumbusha hadithi ya CHOPA TATU, KATA TATU.

kumbukumbu yako haikupi idadi ya askari waliotumika kulazimisha njano kuwa nyeusi!? vipi idadi ya kura zote!? jikumbushe pia nafasi huru ya wananchi kuamua kama ipo.. usijejikuta unahangilia dhuluma ambayo huwa haina guarantee mkaishia kukimbia na masanduku kama Mahanga!

kwa mara ya kwanza Ukawa wanakaba mpaka kijiji ndani ndani kabisa..!
 
kweli ni kadogo but ndo chaguo la wana arusha tunawajua kwa kuwaziba watu midomo but mtaziba wangapi?maana wa tz tumechokaje na ufalme huu!vyovyote iwavyo hatuna cha kupoteza!hofu mashaka kwa mahekalu aah basi!mmetunza nje! tena kikatiba!ila mtaweza kuwa miungu?dunia siyo mali yenu kuna siku mtalala,mtasemaje mbele za Mungu?kwa hawa wanaofariki kwa kukosa huduma hospitali ,kwa njaa ,kwa kukosa elimu ?dhuluma!
 
Tuj
uzane hapa kwetu wanaandika watu katika daftari LA mkazi. Hili daftari lina kurasa 50 na kila kurasa inaandikwa kaya moja kama mpo wengi ktk kaya ni wengi mnaweza kumaliza kurasa kama mbili. Na baada ya kuhji nimeambiwa hayo majina ndo watayachambua ili kupata wapiga kura ambao watawekwa majina yao hapo baadae ktk mbao za matangazo.cha ajabu daftari hili limejaa wakati wengine hatujaandikwa baada ya kuhoji kwa mtendaji anasema daftari ni moja tu wakuu hii imekaaje nitakosa haki ya ngu ya kupiga kura? Maana typo wengi ambao hatujaandikwa tafadhali anayejua vizuri ili na mm nikatoe elimu maana huku sisi upinzani bado lakini kwa sasa vijana wanamwamko wavkuandikwa ili wapige kura(mada ndani ya mada)
 
Futa delete ccm nchi nzima ukawa go go go lema tupo pamoja sana kamanda wetu
 
kweli ni kadogo but ndo chaguo la wana arusha tunawajua kwa kuwaziba watu midomo but mtaziba wangapi?maana wa tz tumechokaje na ufalme huu!vyovyote iwavyo hatuna cha kupoteza!hofu mashaka kwa mahekalu aah basi!mmetunza nje! tena kikatiba!ila mtaweza kuwa miungu?dunia siyo mali yenu kuna siku mtalala,mtasemaje mbele za Mungu?kwa hawa wanaofariki kwa kukosa huduma hospitali ,kwa njaa ,kwa kukosa elimu ?dhuluma!

Asante mkuu
 
Back
Top Bottom