Lema alimpua Meya wa Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema alimpua Meya wa Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FJM, May 24, 2011.

 1. F

  FJM JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) ameendeleza msimamo wake wa kutokumtambua Meya wa Jiji la Arusha, safari hii akiibua malumbano mbele ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), baada ya kulumbana na Naibu Meya wa Jiji hilo, Bashiri Msangi.

  Malumbano hayo yalitokea wakati wabunge hao wa EAC walipokwenda kupanda miti kwenye shule ya msingi ya Nadosoito, Arusha. Wabunge hao waliongozwa na Mbunge kutoka Tanzania, Kate Kamba, akimwakilisha Spika wa Bunge hilo, Abdurahin Abdi, ambaye alishindwa kuhudhuria kutokana na majukumu mengine ya kiofisi.

  Mara baada ya Lema kupewa nafasi ya kuzungumza alianza kwa kusema kuwa hamtambui meya wa Jiji hilo kwa kuwa hakuchaguliwa kwa mujibu wa sheria zilizopo. Wageni wengine waalikwa waliokuwa katika hafla hiyo ni madiwani, maofisa kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha, wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na walimu na wanafunzi.

  Meya wa Manispaa ya Arusha, Gaudence Lyimo, hakuhudhuria hafla hiyo na badala yake alimtuma Naibu Meya, Bashiri Msangi, ambaye ni diwani wa Kata ya Daraja Mbili kumwakilisha.

  "Napenda kuwaelezeni kwamba sitambui uwepo wa meya katika hafla hii…suala la umeya hapa Arusha tuna mgogoro nalo, hakuchaguliwa na yuko kinyume cha taratibu na sheria," alisema Lema. Akizungumza baada ya shughuli ya kupanda miti, Lema alisema alitoa kauli hiyo mbele ya wabunge wa EAC ili kufikisha suala la mgogoro wa umeya kwa jumuiya hiyo."Nilitaka kufikisha suala hili mbele ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili watambue kwamba hapa Arusha watu wananyimwa haki zao za kidemokrasia," alisema.

  Naibu Meya, Msangi alipopata nafasi ya kuzungumza, naye alirusha madongo kwa Lema akisema anamtambua meya kwani alichaguliwa kihalali. "Mimi hapa hatuvutani kuhusu meya wa Arusha kwa sababu amechaguliwa kwa mujibu wa sheria zilizopo," alisema na kuongeza: "Sisi ni timu moja, hatutofautiani na mbunge wetu na ndio maana yupo hapa."

  Lakini akizungumza na NIPASHE, baada ya kulipuliwa na Lema, Msangi alisema kitendo alichokifanya Lema ni cha hatari sana.

  "Kauli ya Lema ni hatari sana, na hasa imetolewa mbele ya wageni…na hii inaonyesha jinsi asivyo na mapenzi na nchi yake," alisema.

  Akitoa shukrani baada ya kumalizika kupanda miti, diwani wa Kata ya Terati, Julius Sekayani, alisema wanachohitaji wananchi wakati huu ni maendeleo na sio siasa.

  "Suala la uchaguzi limeisha, wananchi wetu wanataka kuona kazi sasa na sio siasa, binafsi nitakuwa sina adabu nikisema simtambui meya kwani alichaguliwa kihalali na kwa mujibu wa sheria za nchi hii, zinazosimamiwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa," alisema na kuongeza:

  "Naomba waheshimiwa wabunge waelewe kwamba wakati wa siasa umepita na sasa ni muda wa kuchapa kazi."


  Source: Nipashe 24th May 2011

  My take: kwenye red - CDM waanikeni hao kila kona ya dunia wakose hata sehemu za kuuza sura!
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Go on Lema
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mojawapo ya shida ninayoipata ni kutenganisha SIASA na MAISHA ya kila siku. Hebu chama cha magamba nisaidieni.
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu Selous heshima yako
  Siasa ni kila kiitu katika maisha yako ya kila siku japo huipendi maana hao wanasiasa ndio wanaoamua ni nini ufanye na nini kisifanyike. Watawala ni wanasiasa na wanaongoza kila sehem ya maisha yako kuanzia mtaani kwako kwa balozi sijui mtendaji wa kijiji au kata wanatawala maisha yako ya kila siku japo kwa muda mwingine hawana impact kwenye maisha yako ila jua wapo pale kwa ajili hiyo
   
 5. i

  ibange JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huwezi kuficha uovu. Lazima hata wageni waambiwe uovu wa Magamba. Kama mna hakika uchuguzi ulikuwa halali kwanini mnaogopa wageni kujua?
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Wataipata fresh! Mwendo ni kuwalipua mwanzo, mwisho mpaka kieleweke! Huyo naibu meya nae kaingizwa mkenge tu! Meya feki hathubutu kuhudhuria tukio lolote maana anaishia kuzomewa na wananchi. Anaishia ofisini tu. Mtaani hakukaliki!
   
 7. D

  DENYO JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Safi sana lema unakubalika mkuuuuuu
   
 8. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,654
  Likes Received: 1,439
  Trophy Points: 280
  hivi hizi kauli za uchaguzi umekwisha tunatakiwa tuchape kazi wamekaririshwa? kuna mtu hajui kwamba uchaguzi umekwisha??

  mi nina hasira sana na hawa wapuuzi... mungu nipe moyo wa kuvwavumilia hawa watu
   
 9. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mwizi ni mwizi tu hata akiwa kwenye nyumba ya ibada ni mwizi, Lema tupo pamoja kaka
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Endelea kumlipua mbele ya wageni:pound:
   
 11. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Tunahitaji akina Lema kama kumi ili tupate uhuru dhabiti
   
 12. m

  matawi JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huwezi kutenganisha ni kama gari na petroli kimoja kinabeba kingine
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sijui huyu meya wa Arusha anapate usingizi akujua watu wamempinga hadi wengine kupoteza uhai!
   
 14. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ukiwa smart ni burudani 2.
   
 15. Mbeu

  Mbeu Member

  #15
  May 24, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red, these fake leaders, who have never been to school do not know the meaning of politics, "politics is the live blood of Development", i think we should now consider the Level of Education before electing leader, who can not even define what politics is, to hell. Alafu tabia ya kusema uchaguzi umekwisha sasa tuangalie Maendeleo ya wananchi, this is pure NONSENSE Maendeleo gani anazungumzia huyu Diwani, Mh. Diwan i advice you to learn more books inorder to be in a position of defining politics and the roles of opposition parties in Tanzania.
   
 16. M

  Mikefe Member

  #16
  May 24, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mh Lema ameropoka kama mwendawazimu kuwa hamtambui meya wa Arusha.Hivi kiongozi kama huyu si anaweza kuiabisha nchi akipewa majukumu makubwa.Hajui kuwa mambo ya kijiweni tangu alipokuwa mbunge ndio basi.Inawezekana hata aliwahi kuwa mwizi mifukoni standi ya Arusha jinsi anavyoropoka kama vile hana akili.
   
 17. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mlidhani mambo ya arusha yameisha?
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mikefe niliwahi kusoma hoja kama hii hii miaka ya nyuma kidogo yaani 1947 - word for word.
   
 19. M

  Mr. Masasi Member

  #19
  May 24, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wananchi wako nyuma yako Lema vuta soksi mpaka kiunoni
   
 20. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135

  Teh teh teh! Ina maana amedesa? Shida ni chama chao cha magamba ambacho kinaishi mwaka huo ulioutaja.
   
Loading...