SI KWELI PreGE2025 Lema ajitosa kugombea Ubunge, apinga ajenda ya 'No Reform, No Election'

SI KWELI PreGE2025 Lema ajitosa kugombea Ubunge, apinga ajenda ya 'No Reform, No Election'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
π‹π„πŒπ€ π€π‰πˆπ“πŽπ’π€ πŠπ”π†πŽπŒππ„π€ 𝐔𝐁𝐔𝐍𝐆𝐄 , π€ππˆππ†π€ 𝐀𝐉𝐄𝐍𝐃𝐀 π˜π€ "𝐍𝐎 π‘π„π…πŽπ‘πŒπ’, 𝐍𝐎 π„π‹π„π‚π“πˆπŽπ"

Kupitia ukurasa wake wa Twitter (X), Godbless Lema ametangaza kuwa ameungana na wanachama wengi wa CHADEMA wanaopinga ajenda ya No Reforms, No Election.

Lema ameweka wazi msimamo wake wa kushiriki kwenye uchaguzi akisisitiza kuwa ni muhimu kuendelea kupigania mabadiliko ndani ya mfumo wa kisiasa kupitia ushiriki wa moja kwa moja kwenye uchaguzi.

Aidha, amethibitisha kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha Mjini.

photo_2025-04-04_09-58-58.jpg

photo_2025-04-03_17-28-25.jpg
 
Tunachokijua
Godbless Lema ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini. Kupitia ukurasa wake wa X, Lema amekuwa ni moja kati ya viongozi wa chama hicho ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kufanya uchechemuzi kuhusu ajenda ya 'No Reforms, No Election' ambayo msingi wake mkuu ni uhitaji wa mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi ili kuimarisha uhuru na haki wakati wa uchaguzi.

Madai
Kumekuwapo na picha ya chapisho linalosambazwa mtandaoni likidaiwa kuchapishwa na Lema kupitia ukurasa wake rasmi katika mtandao wa X (Zamani Twitter)

Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu yaani (Key Word Search) ulibaini kuwa chapisho hilo si halisi, bali ni la kutengenezwa kwani halikuchapishwa na Lema.

Aidha Chapisho lililotumika kusambaza taarifa hiyo si la kweli, kwani limetumia utambulisho wa JamiiForums ambayo haijachapisha kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Hata hivyo kwa kutumia kiunganishi (QR CODE) kilichopo katika chapisho hilo, JamiiCheck imebaini limepotoshwa kwa kuhaririwa kutoka kwenye chapisho rasmi la JamiiForums lililochapishwa mtandaoni tarehe 26 Februari, 2025 likihusu wito wa chama cha ACT - WAZALENDO kuitaka serikali kumuachia huru aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha walimu wasio na ajira, Joseph Kaheza aliyekamatwa mkoani Geita.

Aidha wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Arusha pamoja na mambo mengine Lema alisisitiza wanaotaka kugombea ubunge na udiwani kupitia chama hicho kuwa kazi yao ya msingi ni kupigania mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi ili kuchochea uchaguzi ulio huru na haki.​
π‹π„πŒπ€ π€π‰πˆπ“πŽπ’π€ πŠπ”π†πŽπŒππ„π€ 𝐔𝐁𝐔𝐍𝐆𝐄 , π€ππˆππ†π€ 𝐀𝐉𝐄𝐍𝐃𝐀 π˜π€ "𝐍𝐎 π‘π„π…πŽπ‘πŒπ’, 𝐍𝐎 π„π‹π„π‚π“πˆπŽπ"

Kupitia ukurasa wake wa Twitter (X), Godbless Lema ametangaza kuwa ameungana na wanachama wengi wa CHADEMA wanaopinga ajenda ya No Reforms, No Election.

Lema ameweka wazi msimamo wake wa kushiriki kwenye uchaguzi akisisitiza kuwa ni muhimu kuendelea kupigania mabadiliko ndani ya mfumo wa kisiasa kupitia ushiriki wa moja kwa moja kwenye uchaguzi.

Aidha, amethibitisha kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha Mjini.
Invisible Mood Ashad

Futeni uzi huu
 
No reform no election yaota mbawa πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Naona dar mabodaboda wanamsimamo sana na no reforms no election
 
Back
Top Bottom