mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 324
- 347
Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Godbles Lema,ameanza kuwa na wasiwasi juu ya uaminifu wa Mwenyekiti wake wa Taifa Freeman Mbowe na Chama Cha Mapinduzi(CCM),kuwa unaweza kumpofusha kiongozi wake huyo asione hila yoyote kutoka kwao.
Lema ameonyesha hofu hiyo kupitia Ukurasa wake wa Twitter,leo Juni 23 ambapo ameandika na kumuasa Mbowe juu ya ukaribu wake na CCM hasa wakati huu ambao sakata la wabunge 19 wa Chama hicho likiwa linazungumzwa katika mazingira tofauti.
Katika kuonyesha hofu yake hiyo kupitia Twitter Lema ameweka picha inayomuonyesha Mbowe,Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Kanali Mstaafu Abdul Rahman Kinana
Katika picha hiyo ambayo Mbowe ameweka mikono yake mbele mithili ya mtoto anayeomba msaada kwa Mzee wake Lema ameandika
"Mwenyekiti nimefanya kazi na wewe kwa muda Mrefu.Naujua moyo wako juu ya nchi,najua Nia yako.Ninakiri kuwa umejitoa kwa ajili ya Tanzania.Tunapokuwa kwenye mazungumzo ya Tanzania Bora muombe Mungu akuonyeshe hila"
Kisha akauliza swali kuwa
"Unafikiri Spika anaweza kuvunja sheria Bila baraka za CCM?"
Kauli hiyo ya Lema imebebwa kwa uzito mkubwa na wachangiaji mbali mbali ikizingatiwa kuwa ni mkosoaji na mtu mwenye maono ambayo mara kadhaa yamekuwa yakijidhihirisha.
Miongoni mwa waliomuunga Lema Mkono juu ya hofu yake hiyo ya Mwenendo wa Mwenyekiti ni pamoja na mwanaharakati wa mitandaoni Mdude Chadema ambaye aliishauri badala ya kutumia neno CCM Lema angepaswa atumie neno Samia.