Visao da futuro
Senior Member
- Nov 7, 2016
- 121
- 40
hapo umenikumbusha mbali sana!!!!!!
Umenena vema.Hekima gani? Hekima ya kuita maoni ya wazee wenzake utoto? Hekima ya kulinda maslahi ya familia yake? Hekima gani hiyo?
Good!Kisiasa, Uongozi wa Mwinyi ulifanikiwa katika mambo makuu mawili; kufunguliwa kwa milango ya demokrasia na Uhuru wa Vyombo vya Habari. Dhana ya demokrasia, japo haikutumika katika chaguzi za kipindi chake, lakini angalau miaka miwili kabla ya kuondoka madarakani nchi ilifungua mlango wa demokrasia ambapo siasa za vyama vingi zilianza wakati yeye akiwa madarakani.Kwa pamoja na Uhuru wa Vyombo vya habari, nchi ikajenga mazingira mapya kutoka yale ya utawala usiokosolewa kuja utawala uliokosolewa hadharani. Kwa mara ya kwanza ikashuhudiwa demokrasia ya Rais kuchorwa na kusemwa vibaya.
Vijana wa Chuo Kukuu cha Dar es Salaam wao walifikia hatua mbaya zaidi pale walipoifuja demokrasia hiyo kwa kuchora picha za matusi dhidi ya Rais Ali Hassan. Kama tutakavyoona katika kipengele cha elimu, Mwinyi alileta nafuu kubwa ya maisha ya Wanataaluma Chuoni hapo.
Japo wanataaluma walianza kuonesha mfano mbaya wa matumizi ya uhuru wa kujieleza ambao haukuwepo enzi za Nyerere lakini bado Mwinyi hakufunga mlango wa demokrasia.
Kwa mara kwanza tangu miaka ya 1960, Watanzania wakaanza kushuhudia majukwaa ya upinzani dhidi ya Chama tawala na serikali. Ukizungumzia mwanzo wa mageuzi ya kisiasa basi lazima utayakuta ndani ya kipindi cha Mwinyi.
Kama kuna eneo lililoung’arisha mapema utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi basi lilikuwa ni lile la Uchumi. Mwinyi aliaswa na wataalamu wa uchumi kuwa aachane kabisa na fikra zilizoshindwa na Mwalimu Nyerere kama alitaka kufanikiwa katika eneo hili.
Foleni zilikuwa za kusukumana kwani watu walikuwa wengi kuliko bidhaa. Ndiyo kusema, wengine walirudi nyumbani mikono mitupu baada ya jitihada za kusukumana ili kulifikia dirisha la duka kushindikana. Wengine walizirai kwenye foleni! Ugumu hasa ulikuwa katika kupata sukari au mchele uliokuja kwa nadra.
Teh teh teh
Nimechekaa eti huduma yake inaitajikaYule jamaa aliyemzaba kibao hivi bado yupo, naona huduma yake inahitajika haraka sana.
Legacy yake ni vile vibao alicharazwa msikitini! Yule jamaa angempiga ngumi kabisa!View attachment 448507
Rais mtaafu Mzee ALI HASSAN MWINYI ambaye nadhani ki historia ni mmoja ya watu wachache sana duniani ambao waliwahi kuwa rais wa nchi mbili tofauti. Al Hajj Mwinyi aliwahi kuwa Rais wa Zanzibar na Tanzania pia leo ametimiza miaka 91 toka azaliwe.
Je GREAT THINKERS wa JAMIIFORUMS mnaweza kutupatia dondoo za legacy yake na cha kujiuliza je mnadhani hawa watawala tulionao wangejifunza nini toka kwa Mzee Ali Hassan Mwinyi?
Shairi zuri zana hili ukioimbaaMungu akupe maisha marefu na afya tele mzee wetu mzee ruksa iliikuta nchi iliyokuwa hohe hae inchi imejichokea na sera za ujamaa kila kitu foleni na hata ukiunga foleni huna hakika ya kupata bidhaa lakini ukaja ukaufungua mlango wa ruksa hakika ruksa ikaifaa sana nchi yetu.
Kipindi kile nchi ilihitaji kiongozi mwenye haiba yako ukaamua kwenda kinyume na asili ya ujamaa ili inchi ipone hakika baadhi ya mazuri ambayo tunayashuhudia hadi leo yalitokana na jasho lako.
Uliyafanya haya kwa ujasiri japo haiba yako yaonekana ya upole ila ulifanikiwa kuivusha nchi katika kipindi kigumu kweli kweli.
Nakumbuka ukituaga kwenye hutuba yako ukatuambia "MABAYA YANGU NIACHIENI LAKINI MAZURI YANGU TUGAWANE". Hakika ni kweli leo mazuri yako tunagawan.
Hongera sana mzee ruksa mola aendelee kukupa afya njema na miaka mingi zaidi.
Mwinyi na Magufuli wote wamekua marais kwa bahati.
Mwinyi walikubaliana na nyerere kwamba mwinyi kwemye kikao akatae ili nyerere aendelee.. kumbe mwingi baada ya kumwambie mkewe.. akaambiwa kama atakataa asirudi nyumbani..
Mwimyi baada ya kuulizwa akajibu nipo tayari na nashukuru kwa fursa na ndio mwanzo wa nyerere kusema mtu unashauriwa mkeo kitandani .
Wote hawakuwa na mpango nini watalifanyia taifa hili.
Kweli mkuu, mi nakumbuka nikiwa mdogo miaka hiyo(nilikulia Kariakoo,Tandamti na Jangwani,au tuseme, Tandamti na Msimbazi),nikimwona mtoto kavaa kandambili pea moja(yaani zinazofanana), nashtuka! nahisi kwao matajiri! maana kwetu ya kushoto azam,kulia yanga,au kushoto simba, kulia ..... yaani ni kawaida kuvaa kimasikini-masikini.Surely u weren't on 80's pale mafundi cherehani walipata kipato kwa kuria viraka nguo kwenye viraka.
Mtu ynatumia 4hrs kupanga foleni ili upate pakti moja ya maziwa mche mmoja wa sabuni a kilo of sukari maybe sembe!
Hakika hukukuta hata makuli walitajirika kwa kushirikiana na maofisa ugawaji kufanya ulanguzi!
Utawala julius miaka hiyo wanadunzi sio muhimu kuvaa sare aje tu shule kwa chochote alichojaaliwa kuvaa!
Mwinyi alileta mengi ya manufaa kwa nchi yetu