Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Inconvenient Truths

JF-Expert Member
Oct 21, 2014
439
354
mwinyi1bc.jpg
Rais mtaafu Mzee ALI HASSAN MWINYI ambaye nadhani ki historia ni mmoja ya watu wachache sana duniani ambao waliwahi kuwa rais wa nchi mbili tofauti. Al Hajj Mwinyi aliwahi kuwa Rais wa Zanzibar na Tanzania pia leo ametimiza miaka 91 toka azaliwe.

Je GREAT THINKERS wa JAMIIFORUMS mnaweza kutupatia dondoo za legacy yake na cha kujiuliza je mnadhani hawa watawala tulionao wangejifunza nini toka kwa Mzee Ali Hassan Mwinyi?
 
Kisiasa, Uongozi wa Mwinyi ulifanikiwa katika mambo makuu mawili; kufunguliwa kwa milango ya demokrasia na Uhuru wa Vyombo vya Habari. Dhana ya demokrasia, japo haikutumika katika chaguzi za kipindi chake, lakini angalau miaka miwili kabla ya kuondoka madarakani nchi ilifungua mlango wa demokrasia ambapo siasa za vyama vingi zilianza wakati yeye akiwa madarakani.Kwa pamoja na Uhuru wa Vyombo vya habari, nchi ikajenga mazingira mapya kutoka yale ya utawala usiokosolewa kuja utawala uliokosolewa hadharani. Kwa mara ya kwanza ikashuhudiwa demokrasia ya Rais kuchorwa na kusemwa vibaya.

Vijana wa Chuo Kukuu cha Dar es Salaam wao walifikia hatua mbaya zaidi pale walipoifuja demokrasia hiyo kwa kuchora picha za matusi dhidi ya Rais Ali Hassan. Kama tutakavyoona katika kipengele cha elimu, Mwinyi alileta nafuu kubwa ya maisha ya Wanataaluma Chuoni hapo.

Japo wanataaluma walianza kuonesha mfano mbaya wa matumizi ya uhuru wa kujieleza ambao haukuwepo enzi za Nyerere lakini bado Mwinyi hakufunga mlango wa demokrasia.

Kwa mara kwanza tangu miaka ya 1960, Watanzania wakaanza kushuhudia majukwaa ya upinzani dhidi ya Chama tawala na serikali. Ukizungumzia mwanzo wa mageuzi ya kisiasa basi lazima utayakuta ndani ya kipindi cha Mwinyi.

Kama kuna eneo lililoung’arisha mapema utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi basi lilikuwa ni lile la Uchumi. Mwinyi aliaswa na wataalamu wa uchumi kuwa aachane kabisa na fikra zilizoshindwa na Mwalimu Nyerere kama alitaka kufanikiwa katika eneo hili.
 
Asante sana Ritz kwa kuweka bayana hayo
Muda mfupi tu baada ya Mwinyi kuingia madarakani na kubadili mtazamo wetu wa kiuchumi, mambo yakaanza kubadilika kiasi cha kuwashangaza watu. Magenge ya ulanguzi yakatoweka baada ya bidhaa kupatikana kwa wingi.

Watanzania wakaanza kufanya biashara na nchi nyingine, waliokwenda Kenya kupeleka machungwa, na wao kurudi na sabani za kufulia na kuogea, waliokwenda Uganda, waliokwenda Uarabuni, Ulaya, Marekani, alimuradi kila mmoja alikwenda alikotaka.

Soko la bidhaa mbalimbali likashamiri. Badala ya watu kutafuta bidhaa, bidhaa zikatafuta watu. Nguo mpya za dukani bwerere, mitumba bwerere, sabuni kibao, fegi hahahah teletele, magari makubwa na madogo kibao, Televisheni kibao, Radio kibao.
 
Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
 
Surely u weren't on 80's pale mafundi cherehani walipata kipato kwa kuria viraka nguo kwenye viraka.
Mtu ynatumia 4hrs kupanga foleni ili upate pakti moja ya maziwa mche mmoja wa sabuni a kilo of sukari maybe sembe!
Hakika hukukuta hata makuli walitajirika kwa kushirikiana na maofisa ugawaji kufanya ulanguzi!
Utawala julius miaka hiyo wanadunzi sio muhimu kuvaa sare aje tu shule kwa chochote alichojaaliwa kuvaa!
Mwinyi alileta mengi ya manufaa kwa nchi yetu
 
Alijitahidi kuweza kuleta mabadiliko wakati nyerere akiwa bado hai, pamoja na criticism nyingi alizokuwa anapata kutoka kwa nyerere, kama anavyofanya Magufuli kwa sasa kuwatumbua wateule wa mzee wa msoga wakati bado ni Mwenyekiti wa ccm
 
...Humu ndani kuna watu mna akili nzuri sana, ila wakati mwingine huwa mnajipachika kurukwa akili.

Muda mfupi tu baada ya Mwinyi kuingia madarakani na kubadili mtazamo wetu wa kiuchumi, mambo yakaanza kubadilika kiasi cha kuwashangaza watu. Magenge ya ulanguzi yakatoweka baada ya bidhaa kupatikana kwa wingi.
...Nakumbuka tulikuwa tunapiga mswaki kwa mkaa, kwamba unang'arisha meno! Colgate ilikuwa deal kweli kweli.

...Naona kama tunaweza rudi kule. Hii issue ya sukari haijakaa vizuri. Tulisha sahau bidhaa kuadimika madukani, au kuuzwa kwa magendo.

Watanzania wakaanza kufanya biashara na nchi nyingine, waliokwenda Kenya kupeleka machungwa, na wao kurudi na sabuni za kufulia na kuogea, waliokwenda Uganda, waliokwenda Uarabuni, Ulaya, Marekani, alimuradi kila mmoja alikwenda alikotaka.
...Hapa ndio watu wakaanza kupunguza umasikini, kwani fulsa ziliongezeka.

Soko la bidhaa mbalimbali likashamiri. Badala ya watu kutafuta bidhaa, bidhaa zikatafuta watu. Nguo mpya za dukani bwerere, mitumba bwerere, sabuni kibao, fegi hahahah teletele, magari makubwa na madogo kibao, Televisheni kibao, Radio kibao.
...Umenikumbusha mbali, ndugu.

...Hatutamsahau Mzee wetu, Al-Haj A. H. Mwinyi.
 
more please

akina pasco, mkandara, william malecela, ritz, mohammed said njooni mtupe elimu

ilikuwaje mtu wa Kisarawe kama sijakosea akaja kuwa rais wa zanzibar kisha na rais wa Tanzania?

Tunaomba wasifu wake familia yake, alikosoma, maandishi yake, etc...

Kwa nini anaonekana ametelekezwa kwa maana hakuna taasisi au vitabu au vitu vyenye kumtambulisha kitaifa zaidi tofauti na viongozi wengine kama akina Mkapa na JK na Nyerere?
 
...Humu ndani kuna watu mna akili nzuri sana, ila wakati mwingine huwa mnajipachika kurukwa akili.

...Nakumbuka tulikuwa tunapiga mswaki kwa mkaa, kwamba unang'arisha meno! Colgate ilikuwa deal kweli kweli.

...Naona kama tunaweza rudi kule. Hii issue ya sukari haijakaa vizuri. Tulisha sahau bidhaa kuadimika madukani, au kuuzwa kwa magendo.

...Hapa ndio watu wakaanza kupunguza umasikini, kwani fulsa ziliongezeka.

...Umenikumbusha mbali, ndugu.

...Hatutamsahau Mzee wetu, Al-Haj A. H. Mwinyi.
Foleni zilikuwa za kusukumana kwani watu walikuwa wengi kuliko bidhaa. Ndiyo kusema, wengine walirudi nyumbani mikono mitupu baada ya jitihada za kusukumana ili kulifikia dirisha la duka kushindikana. Wengine walizirai kwenye foleni! Ugumu hasa ulikuwa katika kupata sukari au mchele uliokuja kwa nadra.

Teh teh teh
 
Alkua anaambiwa na WB na IMF Nae anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
...Unajua alichokuwa anaambiwa? Pamoja na kwamba SAP zilikuwa na machungu yake, uchumi ulianza funguka na bidhaa zikajaa maduka, watu wakiwekeza katika miradi kwa jinsi ya uwezo wao.

...Kwako wewe, hakukuwa na kitu bora. Wengine, kipindi chake kilitutoa katika umasikini na tukawa na ahueni. Tulikuwa tunavaa nguo zenye viraka.

...Mwenyezi mungu amzidishie maisha Mzee wetu!
 
Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
Sijui kama ulikuwepo hicho kipindi daah!!

Mwinyi alikuta foleni za unga wa njano na magendo ya bidhaa. Hata ‘sigara kali’ achilia mbali ‘sports’ na SM, ziliuzwa kwa bei ya kuruka! Foleni zilikuwa ndefu, na za kuchosha ambazo wakati mwingine zilikuwa za kusubiria bidhaa ambazo hata dukani hazijafikishwa kutoka RTC/Ugawaji.

Kabla ya mikokoteni kufikisha magunia mawili-matatu ya unga wa njano, au mchele mdundiko, au kitumbo uliotoka Japan, watu kwanza walipanga mawe au makorokoro yoyote yale kwa sababu ya jua kali la saa nane mchana.

Muulize mzee hapo nyumbani au wakubwa wengine wewe umazaliwa umekuta hotpots mezani tu.
 
Foleni zilikuwa za kusukumana kwani watu walikuwa wengi kuliko bidhaa. Ndiyo kusema, wengine walirudi nyumbani mikono mitupu baada ya jitihada za kusukumana ili kulifikia dirisha la duka kushindikana. Wengine walizirai kwenye foleni! Ugumu hasa ulikuwa katika kupata sukari au mchele uliokuja kwa nadra.
...Si bora ukae kwenye foleni, baadae upate hiyo ration yako/yenu. Unaweza kaa, foleni ndio imetoa wanne, mnaambiwa "unga wa ngano umeisha". Dah, chapati ilikuwa anasa!

...Acha sukari au mchele. Unakumbuka sabuni nayo ilikuwa shida?
 
Back
Top Bottom