Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

1. ALIFUATA TORATI YA MUSA NA KUWANYONGA WOTE WALIOHUKUMIWA KIFO NA MAHAKAMA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA TANZANIA BILA MZAHA WALA UPENDELEO AKIWEMO KANALI MMOJA TOKA TABORA NAMPENDA SANA KWA HILO
2. ALIWABEBA SANA WAFANYABIASHARA KIASI KWAMBA AJIRA IKAONEKANA NI UPUUZI NA WENGI WALIACHA KAZI SERIKALINI KWAKUWA MISHAHARA ILIKUWA HAIPATIKANI MPAKA WAFANYABIASHARA WAPELEKE FEDHA BANK NDIPO MFANYAKAZI APATE MSHAHARA NI KATIKA KIPINDI CHAKE ALINISABABISHIA NIACHA KUSOMA BAADA YA KUONA KUAJIRIWA HAKULIPI KAMA KUFANYA BIASHARA
3. ALIMDEKEZA SANA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU PROF. KIGHOMA ALI MALIMA AKAJENGA MSIKITI WIZARA YA FEDHA.
4. NI KATIKA KIPINDI WAISLAM WALITAKA TANZANIA IONGOZWE KIDINI NA MKAKATI HUO ULIONGOZWA NA MAREHEMU SHEIKH YAHYA HUSSEIN KWA KUANZISHA BALKUTA NA KUANZA KUVUNJA MABUCHA YA NGURUWE NA NI KIPINDI HICHO NYAMA YA NGURUWE ILIITWA KWA UTANI "YAHYA" AU MBUZI KATOLIKI
5. NI KATIKA UTAWALA WA MWINYI SERIKALI ILIKUWA HAIKUSANYI KODI NA WAFANYABIASHARA WALIKUWA NA NGUVU YA KUFANYA LOLOTE NA IKULU PALIKUWA PANAINGILIKA KIRAHISI SANA HATA UKIWA NA SHIDA YA ADA YA SHULE ULIRUHUSIWA KUMUONA RAIS NA UKIHITAJI KUCHEZA BAO NA PRESIDAA UNAOMBA NA UNAINGIA KAMA ALIVYOFANYA MWENYEKITI WA YANGA NA MBUNGE WA KILOMBERO MAREHEMU ABBAS GULAMALI. NAISHIA HAPO.[/QUOT

Siajabu mpaka leo watoto wetu wangeenda shule pekupeku, dar es salaam pale ilikuwa ukitaka kuangalia mpira lazima uende mnazi mmoja pale, leo mpaka vyumba vya watoto vina computer.
Dar as salaam mji uliishia Magomeni usalama pale kwingine yalikuwa majaruba tu...nchi ilikuwa haina hata hela ya kuagiza meli moja ya mafuta.. Mwinyi ameingia madarakani mkaanza kuvaa viatu, kuvaa nguo baadhi ya maeneo ilikuwa viraka tu, mkaanza kununua Magari, tv, kujenga nyumba na kipindi hicho ndipo dar ilipoanza kujengeka na mji angalau sura ikaonekana...
 
Halafu kuna njemba ilimkataga mabanzi mubashara hadharani yaani watu wana laana dunia hii.

Na upole ule wa Mzee mwinyi unatoa wapi ujasiri wa kumuadhibu na sucker slap...alinifurahisha alipomsamehe. That's was tottaly humane and humble.
Hivi hili neno "mubashara" lina maana gani?
 
Mkuu kinacho nishangaza ni kuwa mfumo wa vyama vingi sifa nyingi anapewa Nyerere wakati aliyekuwepo madarakani ni Mwinyi sijajua kwa nini anasifiwa Nyerere
Duh , ndugu mbona hiyo haipo. NYERERE ndiye aliyeleta siasa ya chama kimoja. Na uzuri wake alikuwa hapendi upinzani , ukimpinga basi unapotea ksiasa na hata kimali.

He was not a cruel dikteta, bali alikuwa dikteta asiyesahau na kusamehe. Kuna waziri aliyetokea upareni ( nadhani alikuwa MGONJA ), alishindwa kufanya kazi na nyerere akaamua kufanya biashara, alifungua Butcher kwao (SAME), basi nyerere aliwa Finance watu kushindana nae kwa kuuza nyama kwa bei ya hasara mpaka mgonja alifunga kazi.

Nyerere alikuwa anakumaliza taratibu na tena huku anacheka.
 
Nyerere alipoacha Urais alibaki mwenyekiti kwa miaka miwili hadi 1987
mwenyekiti wa CCM....

Umekosea kidogo hapo kwenye timeline.

Nyerere aliongoza C.C.M. muhula wote wa kwanza wa utawala wa Mwinyi, mpaka mwaka 1990 ndio akang'atuka.

Wanahistoria wengi wa Marais wanakubaliana kwamba Mwinyi alihitaji a steadying hand kutoka kwa Mwalimu ndio maana hakukuwa na shinikizo kwa Mwalimu kuachia hatamu za chama kama ambavyo Kikwete alishinikizwa kumuachia Magufuli chama ndani ya mwaka mmoja. Peke yake kabisa toka 1985 Mwinyi angeweza kuyumba.
 
Sikua najitambua ila waliontangua home haswa kakaangu mkubwa hua anatuhadithia naman mzee huyu alivyosaidia Taifa na wanyonge,maana inasemekana kabla yake hata wali tu kula ilikua anasa kubwa yaani mpala sikukuu za Idd na Crixmas,mahitaji ya muhim kama sabuni,sukar yaliuza ktk duka la ushirika na ilikua kwa foleni watu walivaa magunia maana ilikua ukikutwa na shati la mtumba moja ama mawili lazma jela ikuhusu,mzee katufungua sana macho kwa uongozi wake japo kizazi cha kulalamika huwa kipo tu,matajiri wa nchi hii wanaoonekana wengi wameibuka enzi za huyu mzee na ndio hapo ambapo wale wazee wa sasa ambao ndio walikua vijana kipindi hicho waliochangamkia fursa sasahivi wanakula bata huko masaki na kwingine,ila kwa wazee ambao walilala na wengine kua busy na madem sasa wamegandwa na umasikini
 
Back
Top Bottom