Lazima tujiulize kwanini JK hakai Ofisini (IKULU). | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lazima tujiulize kwanini JK hakai Ofisini (IKULU).

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sokomoko, Oct 10, 2008.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sana kwanini watendaji wengi Serikali hawakai katika ofisi zao ili kusukuma gurudumu la maendeleo?Mara nyingi wanaingia na kusign attandance kisha wanaenda kwenye Warsha/Semina/Kongamano tena nasikiwa huwa wanahangaika kusaka/kunusa hizo warsha na makongamano kwanini?eti kuna allawances ukikaa ofisini utapiga miayo bure lakini kwenye semina kuna chai mchana lunch na jioni chai kisha unapewa bahasha!

  Nikafikiria na hili la JK kuwa safarini muda mwingi nikalifikiria kwa makini sana nikasema hili halitakuwa na tofauti na hilo nililosema hapo juu. JK anaweza kuwa anafanya ufisadi wa kiungwana maana bila ya kufanya hivyo hana uhakika wa kupata pato la ziada maana si ameona jinsi Wanahabari na Wanaharakati walivyomkalia kooni mzee Mkapa? Ameamua kubuni njia yake ya kujilimbikizia pesa. Akiwa nje ya nchi anakula allowances akija bongo anafanya ziara za mikoani anapiga bingo!

  Na akiwa huko wakuu wa mikoa jirani na mkoa anaofanya ziara wanatia mafuta magari yao na kumfata kwenye mikutano kwenye mkoa husika, wakuu wa wilaya kadhalika! Hapo wanatumia rasilimali za taifa isivyo! sisi ni masikini lakini hatushi kama masikini na matendo yetu si ya kimasikini.

  Tunaomba wanaojua kiasi anachochukua Rais kama allowance akiwa nje ya nchi na akifanya ziara za mikoani. Maana kuna rafiki yangu humu JF anampango wa kumbea Urais pengine inampashauku ku invest more.

  Mwisho si vibaya mkachukulia hii post kama nionavyo mimi na ningeshauri tuijadili mada hii swali hasa ni kwanini Muungwana anapenda safari?

  Shukran.
   
Loading...