Lazima niende kugombea ubunge jimbo la Bahi Dodoma

Lazima niende kugombea ubunge jimbo la Bahi Dodoma

issa ramadhani

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
1,319
Reaction score
260
Ndugu zangu wanaJF,jimbo la bahi ni moja ya majimbo hapa nchini yanayoongozwa na CCM tangia mfumo wa vyama vingi uanze na kabla ya.ndugu zangu sifa zote ninazo za kugombea na nia ya dhati kabisa ninayo.

Ninasikia kuna viwatu vinapitapita huko na kudanganya danganya wananchi wangu,naomba waache mara moja. Wananchi wangu CHADEMA ni yenu na yetu sote, mbunge wenu nakuja na naomba msiwasikilize wapumbafu wanaokatiza katiza huko.

Mwenye mawazo ya kunisaidia tafadhari mnaweza kunishauri kwa lolote,karibu wanajamvi.
 
Kuna Badwel Pale aka mwarabu koko, mla rushwa anamalizia ofcourse hawezi kutia pua tena pale, Kuna mtu anaitwa Pascal Mwaja nae anapitapita mazazi wake ni wazawa wa pale bahi ila yeye anaishi Dar, tunahisi ataishiwa mapema tu maana ccm ubunge ni wa kununua.Upande wa CHADEMA chama kubwa kuna Lyadunda huyo mtashindana nae kwenye kura za maoni.
 
Unahitaji kuwatumikia wananchi au wao ndio wakutumikie???....kama unadhamira ya dhati ya kuwasaidia watanzania kupambana na umasikini nenda ila kama dhamira yako ni maendeleo bimafsi basi muogope mungu!!!
 
Ndugu yangu komaa tu jimbo halina mwenyewe kwa sasa kama ni maswala ya nyumba ukifanikiwa kuwa mbunge utapata mkopo usiyo na riba, nunua gari na nyingine jenga, halafu ukiwa mbunge mikopo nje nje,, maposho nje nje, Mungu akupe nini. Anza kujipitisha. Ukienda kule mtafute mtu mmoja anaitwa Joshua Mbijili ni alwatani sana pale, zamani alikuwa CCM lakini nadhani sasa kahama atakusaidia kwa vijana wa pale, mikakati hiyo tunakupa.
 
Ndugu zangu wanaJF,jimbo la bahi ni moja ya majimbo hapa nchini yanayoongozwa na CCM tangia mfumo wa vyama vingi uanze na kabla ya.ndugu zangu sifa zote ninazo za kugombea na nia ya dhati kabisa ninayo.

Ninasikia kuna viwatu vinapitapita huko na kudanganya danganya wananchi wangu,naomba waache mara moja. Wananchi wangu CHADEMA ni yenu na yetu sote, mbunge wenu nakuja na naomba msiwasikilize wapumbafu wanaokatiza katiza huko.

Mwenye mawazo ya kunisaidia tafadhari mnaweza kunishauri kwa lolote,karibu wanajamvi.
Endapo wana bahi watakuchagua, utawafanyia nini? Je, matatizo mahsusi ya wana-bahi unayafahamu?
 
Mmmh!!!vuta soksi mkuu huku kongwa wenzio hatulali kuwahakikishia wananchi kwamba hata Chadema inaweza kuongoza,unajua wamelishwa sumu mbaya sana huku?kwani kwenu mnalala?
 
Issa Ramadhani, kijana 'mzuri' a.k.a hendisamu anayetongozwa sana na wanawake. Kijana 'mzuri' a.k.a hendisamu asiyependa mijibaba yenye ndevu/mzuzu. Kudadadeki... sasa 'ubunge' unavamiwa
 
Nenda kachukue jimbo kamanda. mtu mwoga anakufa mara 2 kabla ya kifo chake, kwahiyo usije angusha wananchi, chama na wewe mwenyewe kwa kutothubutu kuchukua hatua. Vaa gwanda kachukue jimbo pesa si muhimu kuliko kukubalika kwa Tz ya leo.
 
Kila la heri, kagombee hata usipo shinda ila utakuwa umesaidia kuwatapisha walau sumu waliyolishwa.
 
Ndugu zangu wanaJF,jimbo la bahi ni moja ya majimbo hapa nchini yanayoongozwa na CCM tangia mfumo wa vyama vingi uanze na kabla ya.ndugu zangu sifa zote ninazo za kugombea na nia ya dhati kabisa ninayo.

Ninasikia kuna viwatu vinapitapita huko na kudanganya danganya wananchi wangu,naomba waache mara moja. Wananchi wangu CHADEMA ni yenu na yetu sote, mbunge wenu nakuja na naomba msiwasikilize wapumbafu wanaokatiza katiza huko.

Mwenye mawazo ya kunisaidia tafadhari mnaweza kunishauri kwa lolote,karibu wanajamvi.

Nikupongeze tu Bw: Issa kwa dhamira uliyonayo, dhamira kwanza Mengine yatafuata. Ila kwa hakika sijafurahishwa na lugha uliyoitumia, kuna wakati watu hupimwa kwa kile wakitoacho toka kinywani mwao.Kuwaita wanachama wenzako, ndugu zako, mliochama kimoja kwamba ni vijiwatu, vinapitapita, wapumbavu.
Sidhani kama ni kauli za kistaarabu achilia mbali toka kwa mwanasiasa awaye yote. Kumbuka Watangaza nia wa CDM wote mnajenga nyumba moja, chama kwanza.
Usipoteuliwa wewe na Chama, mkumbatie na kumsupport mwezio ili chama kitamalaki. CDM ni cha kidemocrasia na si sahihi kuwaona wenzako hawastahili kutangaza nia, acha democrasia ndani ya chama ifanye kazi.
Mimi binafsi, nikisikia kuna mgombea mmoja ktk jimbo ndani ya chama, nitajitokeza ili tutoe wigo mpana kwa wanachama kupembua anayewafaa, si muumini kabisa wa hii habari ya kupita bila kupingwa, na ikitokea nikawa mtangaza nia peke yangu ndani ya chama ktk jimbo hilo, sitafurahi wala kuona ufahari wowote.
Kwa kauli zako hizi napata mashaka na credibility yako. Naogopa huenda wanaBAHI tayari wanazitumia kauli zako kukupima hivi sasa
 
Issa Ramadhani, kijana 'mzuri' a.k.a hendisamu anayetongozwa sana na wanawake. Kijana 'mzuri' a.k.a hendisamu asiyependa mijibaba yenye ndevu/mzuzu. Kudadadeki... sasa 'ubunge' unavamiwa

huyu kijana watu hawamjui,wale wa mmu na chit chat tunamjua tabia zake,naona huku kwenye siasa anaongea kibabe,akienda MMU lazima utajua si mwanaume kamili
 
Namtambua Mathias Paul Lyamunda mgombea kupitia CHADEMA kaweka kambi mda mrefu sana huku anajenga chama na amewapigania wanabahi mambo mengi sana,kama we ni Kamanda wa kweli nenda tu kwa vike ni haki yako ya kidemokrasia Chadema wanaruhusu ila akisimama Lyamunda utaondoka na kura yako mwenyewe tu.
 
Back
Top Bottom