Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Ukisha kunywa uropoke huko,uone kama hujanyea ndo
 
Usisiasishe hoja bwana, hao wanaochafuana kwenye siasa labda ndiyo mchezo wao unavyochezwa. Sisi hapa tunataka sheria ifuate mkondo wake. Lowassa ashitakiwe, Full stop!!
Kama hamchezi siasa mnataka ashitakiwe na nani wakati waliomchafua mnawaona? Waliokuwa kila siku wakija na hoja bungeni za kuunda kamati za Bunge ndo waliomchafua; washaurini walete hoja nyingine za kuunda kamati za bunge za kumsafisha!
 
KWELI IJULIKANE MBIVU NA MBICHI

USHAHIDI KWA SERIKALI NI WATANZANIA AKIWEMO
Mambo ya ushahidi ni wakati Kesi itakapoanza. Nataka kujua wewe unataka Lowassa afikishwe kwenye mahakama ya Mafisadi?
 
Sasa wewe si mtanzania?una haki ya kufungua mashitaka hivyo kusanya ushahidi nenda mahakamani,unataka Nani akusaidie wakati hawaoni ufisadi wake
 
nimekuelewa mtoa hoja. Lazima afikishwe mahakamani haraka........vinginevyo wimbo wa ufisadi tuufute. Chadema baada ya kufanya uchunguzi wa kina waligundua kuwa ni uzushi tu, wakafuta cd yao ya ufisadi dhidi ya EL.
Kuna taarifa kuwa Dk. Slaa alikula dili na waliokuwa wanamwinda EL, wakampa makablasha ya kimagumashi na yeye akawamezesha wenzake, wakaunda bendi na kuanza kufanya shoo za wimbo wa Lowassa ni fisadi kwenye mafiesta kote nchini
 

Hahaha mnajidanganya
 
Hapa ndipo kwenye kila kitu!!?

Kwa nini hawakuwataja mpaka leo!!?
 
Eti "nitashangaa kweli kweli",,,,,who care ukishangaa au usiposhangaa??

Kama hii issue inamhusu Lowassa and he is no longer in power, ni kwanni Kikwete na hata huyu Magufuli hawakuivunja huo mkataba?

Kwanini Kikwete na serikali yake hawakumpeleka Lowassa mahakamani mpka leo?

Wewe ni nani unaekuja kulialia hapa wakati wahusika (Kikwete) ambao walikua na obligations ya kumshitaki hawakufanya mpka wanatoka madarakani?

Lazma mkubali mlishashindwa mapema mno maana hiki kinachoitwa Mahakama ya mafisadi ni kisingizio tu maana hata Mahakama hizi zilizopo zingetosha kumfikisha Lowassa huko... these are the delay tactics as you have no substantive reasons and evidence on this matter...

Simtetei Lowassa, lakni ninyi ni waoga mno na hakika mnaujua ukweli wa Richmond na kama mnajiamini sana nendeni mahakamani leo msisubiri kesho...
 
Keanu hayo majengo hayajakamilika? Si mwende mkafungue? Mmegwaya logme in; visandarusi; vijisent; vya mboga;escrow;green finance;meremeta and so on. Mnakuwa kama nyani asiyeweza kujiona makalio yake lakini anawacheka wenzake. Mnakoipeleka nchi hii siko alikopenda Mungu. Am sure atawachanganya lugha tu muwe kama Mara wa babeli
 
mleta uzi kwa kuwa wewe ni Raia na unadai Lowasas alihusika na ufisadi huo kwa uthibitisho wa bunge na taarifa nyingine,nakupa ushauri wa bure kwa kuwa unalipa kodi na unauchungu na kodi unayotoa ambayo pia ilitumika na inatumika katika kuilipa hiyo kampuni pamoja na kwamba imebadilishwa majina mara mbili,hiyo mahakam ikianza kufanya kazi MARA MOJA WAHI UKAMFUNGULIE KESI LOWASSA,nitakufadhili wanasheria ili wakuaidie
 
Asante Allen kwa kuiweka hii hotuba hapa.

Nilimsikiliza Lowasa siku ile akizungumza bungeni sikumuelewa na mie pia nilijazwa ushabiki na kumnanga kwa makofi, vifijo na hoe hae nyingi pale alipotamka kujiuzuru.

Pia nimeendelea kuisikia hotuba hii mara kadhaa na kuipuuza lakini siku aliposema mwenye ushahidi aende mahakamani na hakuna aliyejitokeza hapo nikaingiwa na kigugumizi.

Leo nimeisoma tena na tena, kuna kitu kikubwa sana nimejifunza khs Lowasa na hasa baada ya hekaheka za mwaka wa jana.

Mungu ambariki Lowasa, hotuba hii inaishi na kuna siku mambo yatatoka hadharani ni suala la muda tu.

[emoji29] [emoji29] [emoji29]
 
Hata akishitakiwa mawakili wa serikali wenyewe hawapo serious a.k.a v***** lowassa atachomoa tuuu....
 
Hata akishitakiwa mawakili wa serikali wenyewe hawapo serious a.k.a v***** lowassa atachomoa tuuu....
Hilo la kuchomoa kwa Lowassa sisi wengine wala halitusumbui. Lakini tunachotaka ashitakiwe!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…