Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,886
- 50,761
- Thread starter
-
- #81
Tumeshachoka na ujinga wao!!Mleta mada utasababisha ujenzi wa hiyo mahakama usitishwe haraka sana maana unaonekana unadondosha mbegu za mahindi ili kuku aingie kwenye mtego.
Naona unatuchokoza sisi wakaazi wa msogaKama wanashindwa kufungua Kesi mbona wana wepesi sana kufungua midomo yao na kubwabwaja mambo wasiyoyaweza? Kama Lowassa ni fisadi basi kesi yake iwe ya kwanza kufikishwa kwenye Mahakama ya mafisadi!!
Aminia kamandaHaya mkuu!pamoja sana
Hayo ndiyo maneno!!Lowassa lazima aende mahakamani
Hakuna ubishi
Huyu ni fisadi tena awamu hii lazima ashitakiwe
Njia moja wapo ya kutekeleza ilani zao kwa manenoTumeshachoka na ujinga wao!!
Tena sisi tunawahimiza kwa sipidi ya Mabasi ya Mwendokasi huku tukiwaombea!!Njia moja wapo ya kutekeleza ilani zao kwa maneno
Kiongozi mkuuu nuru ya chamaLowassa is out of date.....tuangalie wanasiasa vijana wenye maono mapya
Teeeeeeh teeeeeeeeh, hapo ndio imeshatoka hapo ilani imeshatekelezwaTena sisi tunawahimiza kwa sipidi ya Mabasi ya Mwendokasi huku tukiwaombea!!
Sasa mbona mwakyembe ndio ndio stering wa mahakama ya mafisadi?Ni kweli lazima ashitakiwe kama mshtakiwa wa Kwanza. Hata Mimi pamoja na UKADA wangu naona dhahiri Richmond ilikuwa galasa la kisiasa kwa EL. Mwakyembe alifanya siasa na kamati yake ili kuweza kumwepusha MTU mwingine na kikombe kile. Basi apelekwe Mahakama ya Mafisadi akahukumiwe baada ya kuhukumiwa na Mwakyembe the lawyer..
Ni kweli lazima ashitakiwe kama mshtakiwa wa Kwanza. Hata Mimi pamoja na UKADA wangu naona dhahiri Richmond ilikuwa galasa la kisiasa kwa EL. Mwakyembe alifanya siasa na kamati yake ili kuweza kumwepusha MTU mwingine na kikombe kile. Basi apelekwe Mahakama ya Mafisadi akahukumiwe baada ya kuhukumiwa na Mwakyembe the lawyer..
Lumumba sasa hivi mnaishi kwa kudra za mwenyezi munguLowassa lazima aende mahakamani
Hakuna ubishi
Huyu ni fisadi tena awamu hii lazima ashitakiwe
Kiashiria cha udhaifu kwa binadamu wakati mwingine ni pale anaposhindwa kulifikisha mwisho jambo la muhimu analotakiwa kulikamilisha. Sisi kama taifa tumekuwa tunatangatanga na Jambo lililosababishwa na mtu mmoja tu na sisi kama taifa tumeshindwa kufikia mwisho wake.
Tarehe 7/2/2008 aliyekuwa Waziri wa Mkuu wa Tanganyika wakati ule, Edward Ngoyai Lowassa alijiuzulu wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa Zabuni ya Ufuaji Umeme iliyosababisha kuletwa kwa Kampuni ya Ufuaji Umeme ya Richmond nchini. Tangu kujiuzulu kwa Lowassa mpaka sasa imeshapita miaka zaidi ya 8 na miezi kadhaa, lakini bado suala la sakata la Richmond halijaisha
Mitambo iliyoletwa na Kampuni ya Richmond ambayo bado ipo Pale Pale ilipofungwa na Kampuni ya Richmond, imeshabadilishwa umiliki wake mara mbili. Imetoka kwa Richmond ikanunuliwa na Dowans na sasa inamilikiwa na Kampuni ya Symbion ya Marekani. Lakini sisi kama taifa tumeachwa pale pale tulipokuwa Mwaka 2008.
Kwa kuwa kuna Mahakama ya Mafisadi inaundwa na sisi kama taifa tunayumbishwa na suala la mtu mmoja tu, ambaye si kiongozi wa serikali kwa sasa, nashauri Kesi ya Kwanza kwenye Mahakama ya Mafisadi iwe ni hii ya "Ufisadi" wa Edward Ngoyai Lowassa kuhusu Ufisadi wa zabuni ya ufuaji umeme iliyosababisha Sakata la richmond.
Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili kama yeye anao ushahidi tofauti na ule ambao wapinzani wake wanao aje nao mahakamani ili upimwe kwenye mizani ya kisheria tujue nani mkweli kati yake yeye na wapinzani wake.
Haiwezekani mitambo ile iliyoletwa na Kampuni (Feki?) ya Richmond bado ipo nchini mwetu, inafua umeme, Tannesco wanalipa Capacity charges tanesco wanauziwa umeme kutokana na mitambo ile ile iliyokuwa ya Richmond, mkataba ule ule wa kati ya Richmond na Tannesco ndiyo umekuwa ukihuhishwa na Dowans na sasa Symbion, lakini sisi kama taifa bado tunakumbushana mambo ya mwaka 2008.
Kuukata Mzizi wa fitina ni lazima Lowassa na kama wapo na wengine waliohusika na sakata la Richmond wafikishwe kwenye Mahakama ya mafisadi mara tu Mahakama hiyo itakapoanza kazi. Tunataka Kesi ya kwanza kwenye mahakama hiyo iwe dhidi ya Lowassa na wenzake waliohusika na suala la Richmond.
KESI YA LOWASSA ISIPOKUWA YA KWANZA KWENYE MAHAKAMA YA MAFISADI NITASHANGAA KWELI KWELI!!
Yule naye alinyamaza kwa maslahi yake ya baadaye. Na kumbuka wakati ule wa "wanamtandao" naye alikuwemo na kama vile alikuwa amejitayarisha kupata wala nafasi ya kumrithi Jakaya. alikosea step hapo katikati!!Basi,kumbe hata muheshimiwa spika alipewa huo ushahidi,yaani anaujua,sasa na yeye mbona kanyamaza nao sana?
Usisiasishe hoja bwana, hao wanaochafuana kwenye siasa labda ndiyo mchezo wao unavyochezwa. Sisi hapa tunataka sheria ifuate mkondo wake. Lowassa ashitakiwe, Full stop!!Kuna watu walijenga political career yao kwa kumnanga Lowassa na ufisadi... Waangalieni kwanza hao, kabla ya kushauri ashitakiwe.
Hii thamthilia ni kali kinomanomaYule naye alinyamaza kwa maslahi yake ya baadaye. Na kumbuka wakati ule wa "wanamtandao" naye alikuwemo na kama vile alikuwa amejitayarisha kupata wala nafasi ya kumrithi Jakaya. alikosea step hapo katikati!!
Hayo ndiyo maneno!!