Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

kwa hii serikali dhaifu ya ccm usitegemee kitu kama hicho. afu sasa cha ajabu utaendelea kuishabikia hiyo serikali wakati haiwezi kuchulia hatua za kisheria watuhumiwa, sasa sijui utakuwa mtu wa aina gani?!
Hivi Lowassa alijiuzuru au alistaafu maana huwa nasoma Waziri mkuu mstaafu!!!!
 
Alitajwa na yule mwenzake. Sasa si imeshasemwa kuwa atalindwa!?
Acha ubwege. Ripoti ya Richmond ilimtaka ajipime kati ya kujiuzulu au kuendelea na wadhifa. Akaona bora ajiuzulu. Kama hakuhusika kwa nini ajiuzulu?? Acha mahaba ya kijinga wewe!
 
Mtashangaa mahakama hii ya mafisadi inakosa kesi za kuamua. Maana nani atasimama kumshitaki nani kwa ushahidi gani usiomhusisha mshitaki kama mhusika wa ufisadi. It is more political rather than a pure will
 
Ninyi vijana wa UKAWA nani kawaloga? Mbona mnakuwa kama Wagalatia kushabikia mambo msiyoyajua. CCM hawakuwa wajinga kumkata MTU wenu!
 
Gangongine hebu soma hii uje tena na mitusi yako!!

Nakushukuru mheshimiwa Spika kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili nimpongeze Dr. Harrison Mwakyembe Mwenyekiti wa Kamati teule,kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri sana.Kwa kazi nzuri kwa maoni yao na wameiwasilisha vizuri.Lakini Mheshimiwa Spika, nimesimama kuweka kwenye Kumbukumbu kutokuridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.

Mhesimiwa Dr. Harrison Mwakyembe ni mwanasheria tena daktari alikuwa anafundisha wanafunzi Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni Natural justice. Wewe pia Mheshimiwa Spika ni Mwanasheria, unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba katika Kamati Teule, imesikiliza watu wengine wote, pamoja na waliowaita minong’ono ya mitaani. Wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja!

Mheshimiwa Spika. Nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya bunge mpaka ofisini kwangu hata wangeniita ningeenda kwa mguu kama hamna gari. Na nilikuwa tayari kufanya hivyo.Hawa ni watu makini sana, siwezi kuamini kwamba wanaweza kufanya Oversight kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga, walisema Waziri Mkuu ilikuwa hivi, kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza, Waziri Mkuu wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa ni kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano Mheshimiwa Spika, kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema, wenye Richmond nifulani uka- table Record na ushahidi kwamba ni fulani.

Mheshimiwa Spika Taifa letu ni taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa Demokrasia pa kubwa katika nchi yetu pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendendeka, Mheshimiwa Spika nchi haitakwenda vizuri.

Hapa ndipo tunategemewa kuonyesha umakini, umahiri wetu katika mambo ya Demokrasia. Kwa hiyo nilichofanyiwa Mheshimiwa Spika napenda kuweka kumbukumbu sahihi…sawa. Kwamba naona si sahihi, na nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana na nimeonewa sana katika hili. Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja kuelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo, mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani kuniuliza. Kwa nini muamini minong’ono ya mitaani kuliko maelezo yangu?

Sisi wote hapa ni wanasiasa, tukianza kuamini minong’ono ya mitaani, niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi… Tume wamepewa muda wa kutosha kabisa, lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Lakini mheshimiwa Spika, hata pale uliponinong’oneza ukaniambia “una ushahidi wowote”? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Ofisi ya Waziri Mkuu, hata mmoja! Lakini kitabu cha Majedwali kimejaa majedwali meengi pamoja na Magazeti mpaka ya Udaku, lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika. Mimi naamini ingekuwa ni heshima wangeliweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii na hii na hii. Mimi nadhani ingejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni, tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki, amefanya hiki bila kumsikiliza, nachelea kuuliza, hivi watu wa chini itakuwaje?

Lakini Mheshimiwa Spika nimetafakari kwa makini sana jambo hili, nikajiuliza, hivi hasa kulikoni. Mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu, wenye heshima zao. Mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo, kulikoni?

Mimi nadhani, they have a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, ionekane Waziri Mkuu amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe. Mheshimiwa Spika. Nimetafakari sana, kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.

Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa, kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini na kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge wa kunisingizia.

Mheshimiwa Spika nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili, namshukuru sana mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Mawaziri, nawashukuru waheshimiwa Wabunge, na wanachama wa CCM tuliosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama chama Mapinduzi. Baada kusema hayo nakushukuru Mheshimwa.
 
Magu mwenyewe anasema anadili na ufisadi wa miaka mitano iliyopita, je ndani ya hiyo miaka Lowasa alihusika na nini?
Kwanza kama anadili na ufisadi wa miaka mitano iliyopita ule mkangafu wa kwenda bagamoyo ambao unadaiwa utafanyiwa marekebisho aliununua nani?
 
Kama kweli Lowasa ni mhusika wa ufisadi mahakama zilikuwepo hawakumshtaki. Au walisubiri mahakama ya mafisadi!!! Mahakama ni ileile tu kuwa ya mafisadi ni jina tu. Majaji walewale. Hakuna jipya hapo. Watakaopelekwa ni wadogo wadogo tu
 
Amekura ameshiba mpaka amelala mchana na kuota ndoto, unashindwa hata kuwaza namna ya kumsaidia mamayako ila lowassa tu.
 
Mtashangaa mahakama hii ya mafisadi inakosa kesi za kuamua. Maana nani atasimama kumshitaki nani kwa ushahidi gani usiomhusisha mshitaki kama mhusika wa ufisadi. It is more political rather than a pure will
Subiri utaona. Bado kidogo!!
 
Mama yangu alishutumiwa kwenye mambo ya Richmond?
Utakuwa umetumwa!; kwanza unaifahamu ile nyumba ya serikali pale ubungo karibu na sisimizi bar ambayo huyu jamaa yako aliihonga kwa yule binti aliyezaa naye wakati tunasoma naye udsm?
 
huku kwetu kulikuwa na mkutano wa kijiji siku moja basi hiyo maada ya Lowasa ikachomekwa katika mazungumzo,baada ya hapo wananchi wote wakaapa kwamba Lowasa asipopelekwa ktk mahakama ya mafisadi basi wote watachukua kadi za CHADEMA na 2020 ccm chaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…