Pole ndugu yangu! Usiamini hivyo manake swala la rushwa ni mtandao mpana mno! Hakuna kitakachopatikana manake hao takukuru wana link na Tanapa! Hivyo hwataplay part kuwalinda TANAPA!Waziri Nyalandu amefanya la maana kumulika TANAPA.
Wazawa lazima wapewe kipaumbele maana wanatoa ajira kwa Vijana wa Kitanzania.
Kweli huu ni uzalendo Waziri Nyalanda Nakupongeza.
Pia Nafasi za Ajira TANAPA ziangaliwe, nafasi za Ajira ni kwa ufisadi na kujuana.
Ndo maana hata mambo mengine yanaenda Ovyo ovyo TANAPA.
Sasa naomba mawaziri wengine kama Mary Nagu na Anna Tibaijuka nao wafikiri na kuweke wazawa KWANZA.
Uwekezaji na Uwezeshaji ya MARY NAGU na Wizara Ya Ardhi Anna Tibajuka.
Nashangaa kwa nini wageni wanapata ardhi kwa urahisi wakati Mzawa hawezi kupata??
Kuna mwongozo gani katika hizi wizara ili mzawa aweze kupata ardhi na awekeze. Wasomi wetu wa Vyuo Vikuu watawezaji kujiajiri wenyewe bila kujua njia wazi zilizowekwa na hizi wizara????
Wake up you Ministers and follow path of Magufuli, Mwakyembe, Nyalandu etc. e.tc
Ole Medeye yeye hata wananchi wake Arumeru Mashariki ameshindwa kuwasaidia, sembuse Taifa....
Hakuna MTALII anayekuja kutalii nchini kwa mkopo. Ahsante Tours wanaikopa TANAPA kwa nini? Tuziache taasisi za UMMA zijiendeshe zenyewe. TANAPA ina bodi yake ya wakurugenzi. Sheria iliyoianzisha TANAPA haimjui NAIBU WAZIRI. Mambo kama haya ndio yaliyoifikisha TANESCO hapo ilipo sasa.
Takukuru isiishie ktk kuchunguza kufungiwa kwa Ahsante Tours tu ndani ya Tanapa. Iangalie ndani zaidi kuhusu namna wanavyotoa tenda ktk Shirika. Ni kweli wakuu wengi wa Idara hapo Tanapa makao makuu wana kampuni zao, na wanapotangaza tenda ni kama danganya toto tu. Kwani tayari wanakuwa wameshapanga ni nani atachukua tenda hiyo miongini mwao. Bahati mbaya huwa najizuia sana kutaja majina ya watu, lakini wababe hao wawili ndiyo wahusika wakuu wa mfumo huo na hata Mkurugenzi mkuu hana sauti kwao kwa sababu ya ukwasi walio nao. Kifupi ni kwamba si rahisi kupata tenda hapo Tanapa kama haumo ndani ya system.
unampongeza nyalandu kwa uzalendo gani anaouonyesha?,kulinda kampuni inayokwepa kulipa kodi au?,hiyo kampuni ya ahsante tours ni mabingwa wa kuiba njia na kupenyeza watalii kwa kutumia nia za panya na hata tanapa wanalifahamu hilo,sasa badala ya nyalandu kuagiza kampuni hiyo ichunguzwe kujua nani walishirikiana naye kuruhusu wageni kwenda mbuga za wanyama ama mlima kilimanjaro bila kulipa ada yeye anakurupuka na kuwaagiza takukuru wachunguze tanapa.
hapa kuna kitu kimejificha,hakuna utaratibu kwa mawakala wa utalii kupeleka wageni iwe kwenye mbuga za wanyama au mlima kilimanjaro bila kulipa ada,huo utaratibu haupo na hata hao Ahsante Tours wanahafamu maana kuna kadi zinaitwa smart card zinazotumiwa na mawakala wote kulipa fedha benki ya crdb na kadi hiyo kuingizwa kwenye mfumo wa ki-electronic ambao husoma na kudhibitisha malipo kabla mgeni hajaanza safari ya kutembelea mbuga za wanyama au mlima kilimanjaro au mlima meru.
swali ni je hiyo kampuni ya Ahsante Tours ni katika mazingira gani ikaweza kupeleka wageni mara kwa mara bila kuwalipa tanapa hadi wakalimbikiza deni kubwa kiasi hicho? na ni kwa nini ni kampuni hiyo tu iliyopewa upendelea wakati yapo zaidi ya makampuni 200 ya wakala wa utalii wakiwamo wazalendo wenzetu kama huyo ahsante tours?
kwanza kampuni hiyo imemdanganya nyalandu kwamba ilipatwa na mtikisiko wa uchumi baada ya kutokea vurugu za kidini kule zanzibar miezi miwili iliyopita,kwa sababu wewe unayempongeza nyalandu pamoja na nyalandu mwenyewe hamna uelewa na masuala ya utalii pata somo kidogo hapa.
makampuni ya uwakala wa utalii hupokea booking mapema kutoka kwa wageni na malipo hufanyika kupitia booking hizo,hivyo basi mtalii anapofika nchini anakuwa tayari ameshalipia kila kitu na sehemu ya malipo hayo yanatumiwa na wakala kuilipa tanapa na kuonyesha idadi ya wageni na muda wa siku watakazotumia kama ni kwenye mbuga au mlimani.
swali ni kwa mazngira gani kampuni hiyo ikapokea mamilioni ya dola kutoka kwa wageni lakini yenyewe isilipe tanapa?,hapa nyalandu amekurupuka ama anatafuta sifa ambazo kwa wenye uelewa na masuala ya utalii wanamshangaa saana na asitumia neno uzalendo maana wazamendo ni wengi wapo pia wakwepa kodi kama kina ahsante tours nao ni wazalendo.
Kwa upande mwingine kuna harufu ya rushwa hata kwa hao ahsante tours na nyalandu mwenyewe,kwa nini wafunge safari kwenda kwa nyarandu,na akakutana nao bila kuhusisha maofisa wengine wa wizara yake?,alipewa nini na hao ahsante tours?.
Kwanza suala la kampuni hiyo kufungiwa kupeleka wageni halikufanywa na tanapa kama tanapa,ni maamuzi ya bodi ya tanapa,hivyo nyalandu anaingilia maamuzi halali ya bodi ya tanapa,je ana maslahi gani katika kampuni hiyo?,tunaomba takukuru wasiishie kwa tanapa wasonge mbele hadi kwa nyalandu maana ni nyalandu huyo huyo aliyekuwa na mgogoro na dk.chami kwa kutoa maamuzi kinzani na ya waziri wake ambaye ndiye sheria inamtambua na si naibu waziri
nampa ushauri wa bure nyalandu na wewe unayempongeza,fanyeni utafiti kwanza kabla ya kutoa maamuzi maana hata wewe umempongeza bila kufafanua unampongeza kwa lipi hasa la maana alilolifanya,ama kwa sabubu umesoma kwenye magazeti na kuingia kwenye jf kutoa pongezi zako bila kufafanua ili hali si wote wanaosoma magazeti.

Ok,kumbe ni ya Cathbert Swai?Na Nyalandu anadili na Babu Sambeke?nyalandu ni fisadi kama mafisadi wengine,kuna taarifa sahihi kwamba mwezi julai mwaka huu akiwa bungeni mjini dodoma kwenye bunge la bajeti nyalandu aliagiza ndege ya swahiba wa mkurugenzi wa ahsante tours,cathibert swai aitwaye babu sambeke kupeleka wazungu wake wawili dodoma kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro( Kia),sasa anaposema hao wakurugenzi wa ahsante tours hawafahamu,na huyo sabeke alifahamiana naye lini hadi kupewa upendeleo wa wazungu wake kupelekwa bure dodoma kama si kupitia kwa cathibert swai wa ahsante tours?
kama hamna data za kutosha msichangie mada ambazo zitawaumbua baadaye,isitoshe nyalandu anapotosha umma wa watanzania,tanapa haikumkopesha ahsante tours,kilichofayika ni ahsante tours kupewa upendeleo wa kuingiza wageni kwenye hifadhi za taifa bila kulipa ada utaratibu ambao haupo kwa mujibu wa kanuni za tanapa,na kama nyalandu anabisha aonyeshe huo mkataba wa tanapa na ahsante tours waliowekeana saini ya kukopeshana hizo dola 70,000 kama anavyodai nyalandu.
tusiwapumbaze watanzania,sio wote ni hamnazo wapo wenye uelewa kumzidi mapa huyo nyalandu,ambaye anataka kuamsha hasira kwa mawakala wengine nao wahoji iweje wao hawapewi huo upendeleo?,kwa nini ahsante tours?,lazima nyalandu ana hisa hapo ahsante tours si bure wakubwa,
hivi huyo nyalandu anamfahamu vyema cathibert swai na mkewe?,cathibert swai ni mjanja wa mo-town,kule kenya wanaitwa wakora,hata alivyopata hizo mali kuna wingu zito nyalandu hawezi elewa chochote,awaulize wajanja wa mo-town watampa cv ya cathibert swai,hakika usilolijua ni sawa na usiku wa giza
UMECHEMKA kaka, fanya utafiti kabla hujaandika kitu..Angalia sana mwenzetu. Mambo ya kuwaacha wenyewe ni ya hatari sana. Wanajichotea wanavyotaka huko TANAPA. Kumbuka wanakusanya pesa wao na kuzitumia watakavyo kama unavyopendekeza, Ndani ya TANAPA nani ataziacha?
Hiyo bodi ya Wakurugenzi unaifahamu ni akina nani? Unajua kwamba wabunge wamegoma kujiondoa ktk hizi bodi? Akina Jenesta Muhagama wamo ktk bodi za TANAPA! wana ufahamu wowote ktk uendeshaji wa mbuga/utalii? Kuna umoja kati ya TANAPA na hao watu wa Bodi. Wanachota watakavyo.
Mkurugenzi aliyeondoka, Bw. Bigulube, alichota mpaka akachoka na kuota kiburi. Alipoondoka ameajiliwa tena na hao hao waliochota naye. Huyu wa sasa naye, Kijazi, kisha anza. Ni mfululizo wa ulaji bila kikomo.
Makampuni mengi ya utalii yana miradi ya mawaziri na watumishi wa TANAPA. Kuna hao akina Zara ndo kabisa! pamoja na kujiita ni ya wazawa, imekuwa ni sehemu ya wanasiasa kununua au kuweka hisa zao. Vijana wanyonge unaodhani wanapewa ajira wanafaidi unyanyasaji wa makampuni. Kodi hukwepa kila siku kwa msaada wa wakuu wa TANAPA na wanasiasa. faida wanapeana pembeni.
Hii ni nchi iliyooza.