Lazaro Nyalandu vs Khamis Kagasheki vs Government Policy | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lazaro Nyalandu vs Khamis Kagasheki vs Government Policy

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by George Smiley, Oct 30, 2012.

 1. G

  George Smiley JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  [​IMG]

  Kama kawaida ile anatomy of stupidity toka kwa mawaziri wetu inaendelea.

  Kuna barua imetumwa wiki iliyopita a waziri Nyalandu kwenda kwa wawezekaji wa hospitality industry ambayo imetaka maelezo kwa nini zile concessions za investments kwenye national parks zilizotolewa kwenda kwa investors hazijawa utilized na kwenye hiyo barua yake kazi ametishia kuwa ifikapo January mwakani ata zi cancel zote.

  Katika vitu ambavyo waziri Lazaro Nyalandu amekuwa gifted navyo naweza kusema kuwa ni memory loss. Lakini pia saa zingine nafkiria inawezekana ikawa huyu waziri hajui policy ya serikali ambayo yeye ni mtumishi wake.

  Nyalandu (najua ni msomaji sana wa JF) umesahau kuwa waziri wa Utalii aliyeondolewa ndugu Ezekiel Maige mwaka jana alizuia developments zote katika hizo national parks?

  Sasa kwenye barua aliyoandika Nyalandu kwenda kwa wawekezaji (wa ndani na nje) amewashutumu kuwa hawana lolote zaidi ya ku sabotage uchumi wa Tanzania. Hivi inawezezakana vipi huyu Nyalandi na nafasi aliyonayo asijue policy ya serikali, na hususana wizara yake? Hivi Nyalandu hana wasaidizi ambao wangempa taarifa kabla ya kuandika hizi barua za kutisha wawekezaji? How daft kama a deputy minister be?

  I seriously doubt akikaa kwenye Cabinet kama huwa anasema kitu huyu na sasa nishajua kwa nini hakuwa promoted kuwa waziri kamili. Inavyoonekana huyu Nyalandu hajui kinachooendelea ofisini/wizarani kwake.

  Kwa kifupi ni kuwa ban aliyopiga MAIGE bado haijawa lifted sasa haya mambo ya kusend mixed messages kwa wawekezaji yanafanya watu wasijue cha kufanya. Maana wakiendelea na hizo developments watakuwa wame violate existing order au watakuwa wame risk ku poteza mali zao kwa kufuata hiyo order.

  Nadhani mnakumbuka Maige alipo washtua investors na ambao tayari walishatoa fees ili wapate concessions na wengine walishatengeneza michoro na wengine walishaanza tender process kisha out of blue Maige being Maige akapiga marufiku kila kitu & basically this put the entire investment and capital outlay ambazo wawekezaji walishazifanya at risk.

  Well, JK naye hakumchelewesha amfukuza kazi akaishia kulalamika humu JF na kwingineko kuwa kaonewa. Nafasi yake ilichukuliwa na balozi Kagesheki ambaye mpaka naandika huu uzi ile bado hajaiondoa.

  So what is Lazaro going on about? Katika mazingira ya kwaida kwa kusoma hiyo barua yake, if anyone smacks of sabotaging investors it is him with such thoughtless utterances. If anything he should apologize to the investors and the nation for committing such blunders. Im sure his peers kule Waldorf College watakuwa so dissapointed na huyu jamaa. Cha kujiuliza alikuwa wapi wakati maige amepiga marufuku wa ujenzi wa camps na lodges kwenye hizi national parks?

  Huyu ni waziri of the so called wamawaziri vijana ambaye bado ana investment mentality ya ki 1970's ambayo hayana nafasi kwenye dunia hii ya 2012. Kila kukicha Nyalandu yuko kwenye maonyesho ya kuvutia watalii Tanzania toka alipokuwa wizara ya biashara halafu hao watalii wakija wanaanza kupewa mixed signals na the likes of Nyalandu ambaye haijulikani anatekeleza sea ya chama kipi na serikali ipi. Hii ni typical stupidity from our politicians ambao hawako consistent na kwenye utekelezaji wa hizi policies.

  Hivi Nyalandu kashajua repucursions za hawa wawekezaji wakienda kushtaki for the investment, loss of income and profit for the duration for which the concession is valid kule East African Court of Justice? Je wakishinda compensation atatoa mfukoni mwake au walipa kodi wa kawaida ndio watakatishwa?

  Sijajua kama Waziri Kashasheki kashamsomea huyu depututy wake (Lazaro) the riot act, maaana tangu appointment yake he has established himself as a no nonsense man mithili ya fagio la chuma, sweeping deadwood from the corridors of his ministry and cracking down hard on lazy officers from Changombe to the swathes of TANAPA all over the country and those not toeing the line or embarrassing him and I suggest Bwana Kagasheki kama umeisoma hii mwambie huyo Lazaro aandike barua ya kujieleza na pia amuulize kama anaweza kukumbuka kupost mapicha yake na status zake kwenye Twitter anashindwa vipi kujua kuhusu policy ya ndani ya wizara yake?
  BTW here below ndiyo CV ya LAZARO NYALANDU

  [h=2]Member of Parliament CV[/h] [TABLE]
  [TR]
  [TH="colspan: 3, align: left"]GENERAL[/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Salutation[/TD]
  [TD]Honourable[/TD]
  [TD="width: 42%, align: center"]Member picture
  [​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]First Name: [/TD]
  [TD]Lazaro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Middle Name: [/TD]
  [TD]Samuel[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Last Name:[/TD]
  [TD]Nyalandu[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 20%"]Member Type:[/TD]
  [TD="width: 38%"]Constituency Member[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Constituent: [/TD]
  [TD]Singida Kaskazini[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Political Party: [/TD]
  [TD]CCM[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Office Location: [/TD]
  [TD]P.O. Box 9503, Dar es Salaam[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Office Phone: [/TD]
  [TD]+255 784 777 020/+255 784 273 272/+255 754 382 625[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Ext.: [/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Office Fax: [/TD]
  [TD]+255 22 2648028[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Office E-mail: [/TD]
  [TD]lnyalandu@parliament.go.tz[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Member Status: [/TD]
  [TD]Current Member[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Date of Birth [/TD]
  [TD]18 August 1970 [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TH="colspan: 5, align: left"]EDUCATION[/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="width: 35%"]School Name/Location [/TH]
  [TH="width: 27%"]Course/Degree/Award [/TH]
  [TH="width: 15%, align: center"]Start Date[/TH]
  [TH="width: 13%, align: center"]End Date[/TH]
  [TH="width: 10%, align: center"]Level[/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Waldorf University College (U.S.A)
  [/TD]
  [TD="align: center"]BA. (Business Administration)[/TD]
  [TD="align: center"]1994[/TD]
  [TD="align: center"]1996[/TD]
  [TD="align: center"]GRADUATE[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Wartburg University College (U.S.A)
  [/TD]
  [TD="align: center"]BA. (International Business)[/TD]
  [TD="align: center"]1997[/TD]
  [TD="align: center"]1998[/TD]
  [TD="align: center"]GRADUATE[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Pohama Primary School[/TD]
  [TD="align: center"]Primary Education[/TD]
  [TD="align: center"]1980[/TD]
  [TD="align: center"]1984[/TD]
  [TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Mrumba Primary School[/TD]
  [TD="align: center"]Primary Education[/TD]
  [TD="align: center"]1985[/TD]
  [TD="align: center"]1986[/TD]
  [TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Kibaha Secondary School[/TD]
  [TD="align: center"]O-Level Education[/TD]
  [TD="align: center"]1987[/TD]
  [TD="align: center"]1990
  [/TD]
  [TD="align: center"]SECONDARY[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Ilboru Secondary School[/TD]
  [TD="align: center"]A-Level Education[/TD]
  [TD="align: center"]1991[/TD]
  [TD="align: center"]1993[/TD]
  [TD="align: center"]HIGH SCHOOL[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TH="colspan: 4, align: left"]EMPLOYMENT HISTORY [/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TH]Company Name [/TH]
  [TH="align: center"]Position [/TH]
  [TH="align: center"]From Date[/TH]
  [TH="align: center"]To Date[/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]The Parliament of Tanzania[/TD]
  [TD]Member - Singida North Constituency[/TD]
  [TD="align: center"]2000[/TD]
  [TD="align: center"]2015[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Equal Opportunity Trust Fund
  [/TD]
  [TD]Advisor-International Affairs and Development
  [/TD]
  [TD="align: center"]1999[/TD]
  [TD="align: center"]2000[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Northwest Bank, Minneapolis ,USA[/TD]
  [TD]Banker, Operations[/TD]
  [TD="align: center"]1998[/TD]
  [TD="align: center"]1999[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]USA-Minneapolis Division One Corporation[/TD]
  [TD]Staff - Technical Call Centre[/TD]
  [TD="align: center"]1996[/TD]
  [TD="align: center"]1996[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]USA-Waldorf College Foresty City[/TD]
  [TD]Student Service representative[/TD]
  [TD="align: center"]1994[/TD]
  [TD="align: center"]1995[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TH="colspan: 4, align: left"]POLITICAL EXPERIENCE [/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TH="class: text_menu, width: 47%"]Ministry/Political Party/Location [/TH]
  [TH="class: text_menu, width: 31%, align: center"]Position [/TH]
  [TH="class: text_menu, width: 12%, align: center"]From[/TH]
  [TH="class: text_menu, width: 10%, align: center"]To[/TH]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Chama Cha Mapinduzi, CCM[/TD]
  [TD]Assistant Commander - UVCCM , Singida [/TD]
  [TD="align: center"]2009[/TD]
  [TD="align: center"]Todate[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Chama Cha Mapinduzi, CCM[/TD]
  [TD]Chairperson - Singida Regional Youth Association[/TD]
  [TD="align: center"]2001[/TD]
  [TD="align: center"]2003[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Chama Cha Mapinduzi, CCM[/TD]
  [TD]Chairperson - Youth Members of Parliament[/TD]
  [TD="align: center"]2001[/TD]
  [TD="align: center"]2005[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Chama Cha Mapinduzi, CCM[/TD]
  [TD]Member - District Political Committee[/TD]
  [TD="align: center"]2000[/TD]
  [TD="align: center"]2005[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,495
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo!!! :ranger:
   
 3. N

  Ng'ongoampoku Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 18, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu umejaribu kuandika kumponda tu lazaro, inaonesha wazi unachuki binafsi, hapa hatutaki majungu vile vile lugha yenyewe uliyoitumia haijanyoka, mwenye busara akisoma tu atajua hizo ni chuki za siasa
   
 4. M

  MTK JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  You sound so bitter and personal; unneccessarily too long and winding!! una bifu gani na waziri Nyalandu?! kumbuka Nyalandu alikuwa trade wakati Maige anapiga ban ile! na hajawahi kuwa deputy wa Maige kusema kwamba labda walishare notes wakati huo; why all this bitter and acidic language na kashfa nyingi!!

  Kwa nini usimpe Nyalandu the benefit of the doubt kwamba inawezakana Maige alipiga ban lakini hakuirasimisha (formalize) na kwa hiyo hakuna document pale wizarani to that effect! Nyalandu aote?!! Maige mwenyewe alikuwa aina ya mtu wa ku-shoot kwanza na kulenga baadae; kama unauelewa huo msemo?!

  Why dont you get bold and seek audience na Waziri ili afafanue! msaidie kama unaona amekosea sio kumkashifu as a person! CV yake has nothing to do with your concern! Stop being judgmental and self righteous; you are not st Jibril!! you have no monopoly of facts and data.!

  Nadhani tufike mahali kwenye jamvi hili tujifunze ku-argue na sio ku-shout! vitriol and name calling does not pay wala haisaidii nchi yetu kusonga mbele, we all stand to learn from each other; tusemezane na kuelimishana ili tutengeneze a win win situation, kila mmoja wetu anufaike na mijadala mbalimbali inayokuwa posted kwenye jamvi hili.
  Wasaalam and Stay blessed !
   
 5. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Watu hawajui tu........Hakuna Wizara ngumu kama ya Utalii toka tuingie kwenye soko huru.
  Bahati mbaya sana imeanza kusikika hivi karibuni.
  Kifupi hii Wizara na wanaohudumiwa na Wizara hii (Mahoteli, Wawindaji n.k) kuna Mafia ndani yake.

  Na akina siye makabwela ni kushabikia Mawaziri wanaoshughulikiwa na hawa watu ndiyo kazi yetu. Na tazameni akiingia Waziri mla rushwa sugu na ambaye ni Mafia pia hamtasikia sauti yeyote wala habari kutoka Wizara hiyo, na mtaona poa tu maisha yanaendelea.

  Lakini wakitokea wachimvi na wazalendo (angalau kiasi) na wakafanya kazi .....kila kashfa kuwahusu mtazisikia na siye akina Kabwela ndiyo tutakuwa wa kwanza kusema .............Waondokeee!!
   
 6. G

  George Smiley JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  blah blah blah

  mawaziri 2

  serikali moja

  wizara moja

  policy 2 tofauti

  wapi na wapi?
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Binafsi naamini
  nchi yetu ina meeengi mno ya kuandikwa kwenye Guinnes book of records
  kwa mambo ya uongozi na siasa tu
   
 8. FOR 2015

  FOR 2015 JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 539
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sina hakika sana na kilichoandikwa najaribu tu kujisadikisha kisha nitoe ushauri kidogo kuwa:

  Ni vizuri Mawaziri wanaoteuliwa na hasa kama hawakuwahi kuwa watumishi wa Umma wakawatumia sana makatibu wakuu hasa katika masuala ya 'GOVERNMENT BUREAUCRACY'. Hawa Makatibu Wakuu wa Mawizara wana wataalam wanaozijua vizuri sera, kanuni, sheria, mipango na mikakati mbalimbali ya Wizara husika. Hakuna kitu itafanyika ndani ya Wizara bila Katibu Mkuu na Wataalam wake kujua.

  Mawaziri wawatumie sana hawa ili kuepuka kufanya maamuzi ya kukurupuka na hatimaye kuliingiza Taifa Hasara. Mambo kama haya yatawafanya wananchi wawafikirie mara mbili ifikapo 2015
   
 9. s

  speechwriter Senior Member

  #9
  Nov 22, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
   
 10. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Waziri Nyalandu amefanya la maana kumulika TANAPA.

  Wazawa lazima wapewe kipaumbele maana wanatoa ajira kwa Vijana wa Kitanzania.

  Kweli huu ni uzalendo Waziri Nyalanda Nakupongeza.

  Pia Nafasi za Ajira TANAPA ziangaliwe, nafasi za Ajira ni kwa ufisadi na kujuana.

  Ndo maana hata mambo mengine yanaenda Ovyo ovyo TANAPA.

  Sasa naomba mawaziri wengine kama Mary Nagu na Anna Tibaijuka nao wafikiri na kuweke wazawa KWANZA.

  Uwekezaji na Uwezeshaji ya MARY NAGU na Wizara Ya Ardhi Anna Tibajuka.

  Nashangaa kwa nini wageni wanapata ardhi kwa urahisi wakati Mzawa hawezi kupata??

  Kuna mwongozo gani katika hizi wizara ili mzawa aweze kupata ardhi na awekeze. Wasomi wetu wa Vyuo Vikuu watawezaji kujiajiri wenyewe bila kujua njia wazi zilizowekwa na hizi wizara????

  Wake up you Ministers and follow path of Magufuli, Mwakyembe, Nyalandu etc. e.tc

  Ole Medeye yeye hata wananchi wake Arumeru Mashariki ameshindwa kuwasaidia, sembuse Taifa....
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  unampongeza nyalandu kwa uzalendo gani anaouonyesha?,kulinda kampuni inayokwepa kulipa kodi au?,hiyo kampuni ya ahsante tours ni mabingwa wa kuiba njia na kupenyeza watalii kwa kutumia nia za panya na hata tanapa wanalifahamu hilo,sasa badala ya nyalandu kuagiza kampuni hiyo ichunguzwe kujua nani walishirikiana naye kuruhusu wageni kwenda mbuga za wanyama ama mlima kilimanjaro bila kulipa ada yeye anakurupuka na kuwaagiza takukuru wachunguze tanapa.

  hapa kuna kitu kimejificha,hakuna utaratibu kwa mawakala wa utalii kupeleka wageni iwe kwenye mbuga za wanyama au mlima kilimanjaro bila kulipa ada,huo utaratibu haupo na hata hao Ahsante Tours wanahafamu maana kuna kadi zinaitwa smart card zinazotumiwa na mawakala wote kulipa fedha benki ya crdb na kadi hiyo kuingizwa kwenye mfumo wa ki-electronic ambao husoma na kudhibitisha malipo kabla mgeni hajaanza safari ya kutembelea mbuga za wanyama au mlima kilimanjaro au mlima meru.

  swali ni je hiyo kampuni ya Ahsante Tours ni katika mazingira gani ikaweza kupeleka wageni mara kwa mara bila kuwalipa tanapa hadi wakalimbikiza deni kubwa kiasi hicho? na ni kwa nini ni kampuni hiyo tu iliyopewa upendelea wakati yapo zaidi ya makampuni 200 ya wakala wa utalii wakiwamo wazalendo wenzetu kama huyo ahsante tours?

  kwanza kampuni hiyo imemdanganya nyalandu kwamba ilipatwa na mtikisiko wa uchumi baada ya kutokea vurugu za kidini kule zanzibar miezi miwili iliyopita,kwa sababu wewe unayempongeza nyalandu pamoja na nyalandu mwenyewe hamna uelewa na masuala ya utalii pata somo kidogo hapa.

  makampuni ya uwakala wa utalii hupokea booking mapema kutoka kwa wageni na malipo hufanyika kupitia booking hizo,hivyo basi mtalii anapofika nchini anakuwa tayari ameshalipia kila kitu na sehemu ya malipo hayo yanatumiwa na wakala kuilipa tanapa na kuonyesha idadi ya wageni na muda wa siku watakazotumia kama ni kwenye mbuga au mlimani.

  swali ni kwa mazngira gani kampuni hiyo ikapokea mamilioni ya dola kutoka kwa wageni lakini yenyewe isilipe tanapa?,hapa nyalandu amekurupuka ama anatafuta sifa ambazo kwa wenye uelewa na masuala ya utalii wanamshangaa saana na asitumia neno uzalendo maana wazamendo ni wengi wapo pia wakwepa kodi kama kina ahsante tours nao ni wazalendo.
  Kwa upande mwingine kuna harufu ya rushwa hata kwa hao ahsante tours na nyalandu mwenyewe,kwa nini wafunge safari kwenda kwa nyarandu,na akakutana nao bila kuhusisha maofisa wengine wa wizara yake?,alipewa nini na hao ahsante tours?.

  Kwanza suala la kampuni hiyo kufungiwa kupeleka wageni halikufanywa na tanapa kama tanapa,ni maamuzi ya bodi ya tanapa,hivyo nyalandu anaingilia maamuzi halali ya bodi ya tanapa,je ana maslahi gani katika kampuni hiyo?,tunaomba takukuru wasiishie kwa tanapa wasonge mbele hadi kwa nyalandu maana ni nyalandu huyo huyo aliyekuwa na mgogoro na dk.chami kwa kutoa maamuzi kinzani na ya waziri wake ambaye ndiye sheria inamtambua na si naibu waziri

  nampa ushauri wa bure nyalandu na wewe unayempongeza,fanyeni utafiti kwanza kabla ya kutoa maamuzi maana hata wewe umempongeza bila kufafanua unampongeza kwa lipi hasa la maana alilolifanya,ama kwa sabubu umesoma kwenye magazeti na kuingia kwenye jf kutoa pongezi zako bila kufafanua ili hali si wote wanaosoma magazeti.
   
 12. M

  Manyerere Jackton Verified User

  #12
  Dec 11, 2012
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 2,357
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Mimi nilishasema mapema kabisa kwamba Nyalandu ni tatizo kubwa Maliasili. Akili ya kawaida kabisa inakataa kuwa si weledi, kwa waziri kusimama kuitetea kampuni isiyolipa kodi. Yaani huo mtikisiko wa uchumi, tena uliosababishwa na Uamsho, uliigusa kampuni hii pekee? It's a matter of time mtamjua Nyalandu ni aina gani. Sitaki kutafuna maneno.

  Manyerere Jackton
  Kwembe-Kati
  Dar es Salaam
   
 13. M

  Matawana JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 630
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Soma vizuri kabla ya kuchangia hoja. Hiyo kampuni haidaiwi kodi bali ni mkopo ambao wameshalipa kwa asilimia kama hamsini hivi. Kiasi wanachadaiwa around US 39k ni ujinga kuifungia kampuni yenye confirmed booking ya zaidi wa watalii 1,000. Well done Nyalandu kwa kuingilia kati, endelea kuweka interest za wazawa mbele maana tunakwazwa na mashirika yetu wenyewe huku wageni wakipeta
   
 14. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,926
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Sometimes jeikei anaboa sana

  watu kama nyalandu sijui huwa anawaokota okota wapi??

  Hopless kabisa..
   
 15. z

  zamlock JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kama ana ubavu awatoe matajiri wakubwa wa tanapa na wanaoagiza nguo zao za kuvaa kutoka nje zimeandikwa majina yao na watu hao ni eng matolo, chitanda, na wengine wengi tu hapo tanapa ila hawa niliowataja wanamiliki kampuni ambazo zninajichukulia tenda hapo hapo tanapa hilo liko wazi hao ndio mataita wa tanapa.
   
 16. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  JK anaupako na ma-celebrity kama akina nyaraNDU mtasema hadi mtakauka mate.dawa ni kupiga chini sisiem na watuwake
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hakuna MTALII anayekuja kutalii nchini kwa mkopo. Ahsante Tours wanaikopa TANAPA kwa nini? Tuziache taasisi za UMMA zijiendeshe zenyewe. TANAPA ina bodi yake ya wakurugenzi. Sheria iliyoianzisha TANAPA haimjui NAIBU WAZIRI. Mambo kama haya ndio yaliyoifikisha TANESCO hapo ilipo sasa.
   
 18. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,271
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mimi natokea mikoa ya kaskazini,kwa ambaye ana data kamili kuhusu hii kampuni atuambie,maana kuna asante tours na ahsante tours...na nijuavyo mimi moja ina mkono wa mafisadi,,,i am very worried Lazaro naye ana hisa huko pia.watu mnachukulia poa sana hii ishu,these people make billions.....kwanza naomba nijue ni asante au ni ahsante,ili niweze kufunguka zaidi


  Ahsante Tours - Tanzanian Adventure Travel
  www.[B]asantetours[/B]afaris.com
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ni Asante Tours. Nyalandu hakupewa Job description yake na JK. Hajui kwamba TANAPA ina bodi yake na yeye kama NW hana mamlaka kisheria kuiagiza Menejimenti ya TANAPA. Wanasiasa wetu wanazivuruga sana taasisi zilizochini ya wizara wanazoziongoza hasa kama wakuu wa taasisi hizo "hawatoi ushirikiano wa kutosha".
   
 20. C

  Clemence Baraka JF-Expert Member

  #20
  Dec 11, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 1,599
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Msimamo wa waziri kutetea kampuni za kizalendo ni wakupongeza kwa kila namna. Ni ukweli usiopingika kwamba kwa muda
  mrefu kampuni za kizalendo zimenyanyaswa sana na manunguniko ni mengi lakini hakuna aliyetaka kuona wala kusikia hata kwenye ngazi ya wizara. Makampuni ya nje ambayo yalikua yanapeleka wageni kwa makampuni ya wazalendo yamemiminika Tanzania na kufungua maofisi ambapo wanapokea wageni wao wenyewe. Sheria iliyotungwa mwaka 2007
  inayotaka shughuli za kupandisha mlimani zifanywe na makampuni ya wazalendo tu kama ilivyo mahali popote duniani imekua danganya toto. Association za mawakala wa kitalii zimepigia kelele jambo hili kabla ya uongozi wa sasa wa wizara ya utalii lakini bila mafanikio kutokana na nguvu za kifedha waliyotumia makampuni haya ya kigeni yenye maofisi hapa nchini. Hali hii ikiachwa iendelee ilivyo siku moja utakuta hakuna hata kampuni moja ya kizalendo inafanya utalii na badala yake ni kampuni za kigeni tu. Lakini je siku makampuni hayo yakiondoka yote na wakati huo wazawa wameshamalizwa hali ya utalii itakuaje? Pwani ya Kenya Malindi iliwahi kutokea mohoteli ya kigeni yakahamia zanzibar. Sasa anapotokea waziri kama Nyalando tusibeze juhudi zake. Hata kama kuna anayejua mapungufu yake lakini tuangalie kila jambo na mazuri yake. Muda mrefu tumesubiri waziri wa kusemea wazalendo wala tusichukulie swala hili kisiasa na kusema pengine ana maslahi ndani. Tanapa walivyokubali iwakopeshe bila shaka nao walitizama uzito wa kazi yao. Kama kampuni inaingizia serekali au hata shirika lolote lile dola bilioni mbili kwa mwaka ni busara kabisa wakikwama popote pale wasaidiwe na mkopo wa dola 70000 ni nini basi? Ungekuwa waziri wewe na ukajiwa na kampuni ya namna hiyo na tena inakuonyesha bookings zao 3000 mkononi tayari ungesemwa NO wapigwe panga? Lakini ingekua kampuni ya kigeni nakuhakikishia Tanapa isingewafungia wala hatungekua na nafasi ya kilisoma jambo hilo kwenye magazeti. Watanzania tuwe na tabia ya kupongeza pale panapostahili. Tuondoe tabia kutu. Tutamalizana wanyewe kwa wenyewe na kamwe tutazidi kudidimia na kuwapa fursa wageni kutokana na kutokua na umoja na mapendo. Mtanzania mwenzetu anaposaidiwa kwa njia dhahiri tufurahi kwani kwa njia hiyo hiyo aliyosaidiwa nasi tutadai tusaidiwe.
   
Loading...