Hivi vituko vya kuhama hama vyama bila msimamo wa kueleweka vinashangaza sana. Halafu mtu mzima anaondoka tena anarudi alikotoka na bila aibu anarudi na maneno ya kulaumu alikoenda mwenyewe kwa utashi wake wala siyo kwamba alinunuliwa. Na mara zote wakisharudi wanasema uongozi wa Chama walichohamia una matatizo. Jambo hili linaibua fikra za ajabu kidogo. Wakati mwingine inakuwa kama inamaanisha walitaka wakapewe uongozi wa juu wa hicho chama walichohamia ghafla ili wakisambaratishe. Inaposhindikana basi inabidi warudi walikotoka na maneno ya kashfa. Itoshe tu kukiri kwa kusema kwamba siasa zetu zina dosari tena dosari za kijinga sana.Chadema mmafanyaga makosa sana kuchukua oil chafu toka ccm. Mkimaliza kuisafisha wanawaachia uchafu wanarudi ccm na kuanza kuwachafua.
Nyalandu
Sumaye
Lowassa
Lembeli
Next tym wakija msiwape uongozi wowote. Wawe wanachama wa kawaida.