Lazaro Nyalandu, kinyongo cha Uwaziri kitakuponza

Lazaro Nyalandu, kinyongo cha Uwaziri kitakuponza

Ukoko haupo ktk sufuria tu , hata vichwani upo. Ila kwako umejaa mno. Kumbuka Lissu ni Mbunge toka ktk mkoa 1 na Nyalandu, acha ujinga wa kwenu. alichoonyesha kuanzia kwa watoto wale hadi kwa Lissu ni UBINADAMU.
 
Ghafla Nyarandu akaibukia Nairobi kumtembelea Tundu Lissu na kutoa kauli tata akiwa na Wabunge wa CHADEMA.
Uchama usituondolee utu,Lissu ni mtanzania ambaye anaongozwa na serekali ya CCM kama raia ana haki ya kutembelewa na mwananchi yeyote pasipokujali itikadi ya chama anachotoka.

Labda kama CCM ya siku hizi imepoteza ile imani yake ya kuamini kuwa kila binadamu ni sawa na kila mtu anahaki ya kuthaminiwa utu wake na uhuru wake.

Maana yake siku hizi inaonekana kuwa shetani wa CCM ni mwanaccm anayepeana mkono na mpinzani na shetani wa pili ni mpinzani anayetekeleza wajibu wake kama mpinzani kuikosoa serekali ya CCM kiutendaji.
 
Lazaro Nyarandu mbunge wa Singida ametajwa kuwa na kinyongo cha kupitiliza Kutokana na kutoswa Kwenye Uwaziri Kwenye serikali ya awamu ya tano imebainika. Kati ya mawaziri wa Kikwete wanaoumia huyu bwana anashika nafasi ya kwanza.

Baada ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani na Nyarandu kutoingizwa Kwenye Baraza la mawaziri lá Magufuli, huyu bwana alisuka mkakati kuwashawishi Maseneta 7 wa Marekani kuja Tanzania kuonana na Rais Magufuli kuzungumza masuala yanayotajwa ya Kimaendeleo na kumshawishi Rais amteue Nyarandu Kwenye Wizara ya Maliasili ili Marekani iendelee kushirikiana na Tanzania Kwa kutoa misaada ya vifaa vya kudhibiti ujangili nchini.

Mtakumbuka Rais Magufuli aligundua janja hiyo anakataa kuonana na hao wazungu wa Marekani badala yake alielekeza wakaonane na Spika Ndugai Waeleze mambo yao. Kitendo chá Maseneta hao waliokuja na Ndege binafsi kutomuona Rais kiliwakatisha tamaa sana Kwakuwa Ndugai hakuwa mlengwa.

Hata Wakati wa kikwete kumpandisha Nyarandu kuwa Waziri baada ya kujiuzulu Kagasheki ilikuwa ni Shinikizo la Western power, hii iliwahi kuripotiwa na Gazeti Jamhuri mara kadhaa.

Marekani wanamtaka Nyarandu Kwa sababu za maslahi ya Vitalu vya uwindaji na masuala yote yanayohusiana na bidhaa za wanyama Pori . Huyu ni mtu Pekee aliyeweza kucheza fitina zote kuwaridhisha Matajiri wa kimarekani Kwa kukana maslahi ya taifa lake.

Mdogo wake Nyarandu nimesoma Naye sheria tukiwa darasa moja na hadi leo tuko karibu sana, Pamoja na kutomkubali Kaka yake Kwa madai kwamba hana msaada kwa ndugu zake, Anaeleza jinsi Nyarandu alivyokuwa na matumaini ya kurejea Kwenye uwaziri baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 akiamini ana nguvu kubwa nyuma yake. Kwahiyo kitendo chá kuachwa mazima kimjengea kinyongo kupita maelezo na amenukuliwa akimnanga Rais Magufuli na Rc Makonda kwamba sio Viongozi wenye maono.

Hamad ikatokea ile Ajali ya watoto wa Lucky Visent, Wazungu waliokuwa safari Kwenda Karatu wakakutana na Ajali mbaya ya gari lá wanafunzi iliwabidi washuke na kuokoa wale Majeruhi na kuwakimbiza Hospitali Arusha, wale wazungu Kwa kushuhudia Ajali ile mbaya waliingiwa na huruma na kujitolea kuwapeleka wale watoto Marekani kutibiwa, Nyarandu alichomoka kusikojulikana akaingia kati na kujifanya Msemaji wa wa jambo lile Kwakuwa alikuwa anafahamiana na Wazungu wale. Akajipatia sifa kwamba yeye ndiyo kawapeleka Wale watoto Marekani. Mpaka wale watoto wanarudi na kupokelewa Kwa Sherehe pale KIA hakuna Pongezi toka Kwa waziri yeyote , Waziri mkuu, CCM wala Rais Magufuli Kwenda Lazaro Nyarandu. Walijua janja yake.

Ni katika mlolongo huo huo wa kinyongo cha bwana huyu, Mwezi Julay Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli Alikuwa na Ziara mkoani Singida kuzindua barabara ya Itigi -Tabora, Wabunge wote wa CCM mkoani Singida walihudhuria Ziara hiyo isipokuwa Nyarandu hakwenda Kwenye Ziara ya Rais Ndani ya mkoa wake na alikuwepo Arusha amechil tu.

Hamad Tundu Lissu akapata matatizo ya kupigwa Risasi, Mbunge wa wa CCM Turky akasaidia Kwa malikauli Ndege iende Dodoma kumbeba Lissu na kumpeleka Nairobi, yule mbunge amepongezwa na Spika wa Bunge na CCM makao makuu walimpongeza Kwa maandishi Kwa kitendo chá Uungwana kusaidia Ndege ya kumbeba Tundu Lissu.

Ghafla Nyarandu akaibukia Nairobi kumtembelea Tundu Lissu na kutoa kauli tata akiwa na Wabunge wa CHADEMA. "Muelekeo ni mhimu kuliko kasi, wengi hawajui waendako lakini wana kwenda kwa kasi! Ndio maana ni bora inchi moja kwenda kwenye muelekeo sahihi kuliko maili moja kwenda kwenye muelekeo usio sahihi" alisema Nyarandu.

kabla hajaruhusiwa kuingia ndani ya Hospital kumuona Tundu Lissu Nyarandu alipiga picha Kwenye kibao chá Hospitali na kupost mitandaoni haraka hata Kabla hujamuona mgonjwa. Hii inaashiria Lengo lake ni kuonekana ameenda huko ila sio dhamira ya dhati kumuona mgonjwa, wabongo wanaita kutafuta kiki. Na ameipata kiki aliyokuwa anaitafuta. Ila maneno aliyotoa huko Nairobi na Mengine nayahifadhi ni ishara ileile ya kinyongo chake.

MUDA WA KUMJUA WAZIRI JANGILI UMEFIKA?

Gazeti Raia mwema na Jamhuri walitoa ripoti Maalum ya kurasa 7 kuelezea Ujangili unaofanywa na waziri asiyefahamika katika awamu ya nne, ujangili wa waziri huyo Ulikuwa wa waziwazi na Ushahidi uliwekwa. Waziri huyo aliyetajwa kutumia Helicopter kubeba meno ya Tembo maeneo ya Manyoni na kuyapeleka kusikojulikana. Rais Magufuli baada ya kumulika sekta ya madini hamia na Kwenye Maliasili tuwajue wanaohujumu taifa letu.

Itaendelea..............
Una wivu wa kike wewe pumbafu
 
Nimekusoma kwa makini nimegundua. ..Hata wewe unakinyongo dhidi ya Nyarandu!.

Maelezo yako yoote hayana ushahidi wa kina kuthibitisha kinyongo cha Nyarandu...Kila ushahidi ulioutoa ni Wa Mema...

Mf.Kuleta wawekezaji,Kusaidia matibabu ya wanafunzi majeruhi wa Lucky Vicent,Kumjulia Hali Tundu Lissu Nairobi,Kutoa maoni ya kifalsafa mtandaoni n.k..HAPO KINYONGO KIKO WAPI!?..

Tuhuma za kutomsadia mdogo wake,kutompokea JPM Singida,Kupost ujumbe wenye utata(kwa maoni yako)
Yoote ni masuala binafsi (ni sawa na umbea)hayana maslahi kwa umma!!

Kuhusu waziri jangili wa awamu ya4 asiyefahamika...lakini alifanya ujangili waziwazi Na ushahidi upo!!
Hapa kosa siyo la Nyarandu ni Kosa la serikali ya awamu ya5 kushindwa kumchukulia hatua!

Itaendelea....
 
Mkuu sijakuona siku nyingi sana, sijui shida nini nini??? Asante sana kwa kumpa maneno ya ukweli huyu mwana sisiemu mwenzako... Salamu nyingi sana kutoka kwa Comred Komba a.k.a Mswati

Nipo sana Mkuu na mara nyingi napatikana humu humu JF na hata huyo ' Comrade ' nawasiliana nae mara kwa mara kwani ' Urafiki ' wangu wa Mimi na Yeye ni kama wa Kikwete na Lowassa ambao kamwe hauwezi kutenganishwa na yoyote / lolote / chochote kile labda mmoja wetu atangulie mbele za haki.

Ngoja Mwenyezi Mungu aninyooshee njia ya baraka zaidi ila huyo ' Comrade ' namuandalia bonge la ' Zawadi ' Yeye na Familia yake nzima. Kwangu ni zaidi ya Rafiki na kilichobaki sasa ni Mimi na Yeye tu kukubaliana kufanya ule ' Utamaduni ' wa zamani wa Mababu zetu ' walioshibana ' Kiurafiki kwa kuamua ' Kuchanjana ' na Wembe ' Kimila ' kisha tunapakana damu zetu na hatimaye tunakuwa sasa kama Ndugu kamili.

Nitakutafuta ' Comrade ' wangu wala usijisikie vibaya bado sijatulia kwa sasa ila nikitulia tu tutakutana pale pale Victoria mkabala na Hospitali ya Kairuki tuyajenge zaidi na uzidi kunipa ' Nyeti ' za yule Mama wa CARTRACK kwani ninamkubali mno na sana. Natumai sasa umeshahamia rasmi Dodoma au? Angalia tu huko ' Dally Kimoko / UKIMWI ' ni nje nje na sitaki nimpoteze mwana SAUT na hasa mwana Darfur Hostel mwenzangu yoyote kwa huo ' Ugonjwa ' tafadhali. Naomba mjilinde sana ' Wadau ' zangu.

Kila la kheri.
 
Kuna ubaya gani NYALANDU kwenda kumwona TUNDU LISSU na ni MBUNGE mwenzake?
 
Rubbish..


Hakuna cha maana zaidi ya kulalamika....inaonesha unachuki binafsi na Nyalandu au umetumwa
 
Asee jaribu,unaweza kabisa,tena kabisa kuwa Mchawi,yaani una roho mbaya ya kuwa mchawi
 
Huyu mleta uzi utakuwa mnazibuana mitaro ya maji taka na bashite/le madolez
 
Tatizo kwenda kwa Lissu kakojoe ulale muulize mwenyekiti wako ataua wangapi? Ila naye atakufa tu hizi ni nafasi za Dunia akumbuke tunapita
 
Lazaro Nyarandu mbunge wa Singida ametajwa kuwa na kinyongo cha kupitiliza Kutokana na kutoswa Kwenye Uwaziri Kwenye serikali ya awamu ya tano imebainika.
Na yule mbunge wa CCM mwenye utu,aliyeonyesha utu wake kwa kutumia malikauli ndege ya kumpeleka Lisu Nairobi kutibiwa ikapatikana,ambaye Ndugai na CCM waliteka utu wake na kujifanya kuwa waliofanya ni CCM,kutokana na utu wa huyu mbunge,mwanaCCM halisi,mlibaini kuwa alikuwa na kinyongo gani mpaka akatumia utu wake kumsaidia Lissu kwenda kutibiwa Nairobi?.
 
Back
Top Bottom