Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 141,449
- 283,753
Hizi kazi wakati mwingine msala humpata aliyetenda , Kamuhanda mbona aling'olewa ?Sio mambo sasa swali la kujiuliza nani anayewapa oda
JARIBU UONE AWAMU HII HATUTAKI UJINGA UJINGATungekuwa na msimamo thabiti tungeenda kumtoa makonda pale officine akikataa tunamwathibu
Kumuondoa tuu haitoshi anatakiwa ashtakiwe kwa mauaji.Huu ni wito ambao naupeleka kwa IGP Sirro .
Anayotenda RPC Mambosasa DSM hayana tofauti na aliyotenda Aliyekuwa RPC wa Iringa aliyeitwa Michael Kamuhanda , huyu alisimamia kikamilifu mauaji ya mwandishi wa Channel 10 marehemu Mwangosi , Na kwa kutumia busara ya hali ya juu IGP wa wakati ule bila ya kuchelewa alimng'oa Kamuhanda na kumpeleka Makao Makuu.
Kila mwenye macho amejionea mwenyewe kauli ya jeshi la polisi kukiri kuhusika na mauaji ya mwanafunzi wa NIT , haya ni miongoni mwa mauaji ya kishamba sana kuwahi kufanywa na jeshi la polisi , yaliojaa uzembe wa kiwango kisichopimika , ni mauaji ambayo hata jambazi bwege hawezi kuyafanya .
Ni wakati sasa wa IGP kumpeleka Mambosasa Makao Makuu ili kurudisha amani jijini DSM , ambayo imetoweka moja kwa moja tangu kuingia kwa Mambosasa.
Angalizo - Si kila polisi anaweza kuwa IGP wa DSM .
UKIMJUA UNAFANYAJE? HAPO ULIPO TUU HUJULIKANI UNATUMIA ID FAKE BOYA KABISASio mambo sasa swali la kujiuliza nani anayewapa oda
Hii ni hatua ya kwanza mjomba , kuna kitakachofuatia .Kuondolewa itabadilisha nini? Ndo maana huwa haya maabano yenu yanaishia hewani tu. Mnaji distract halafu kuelekeza energy pasipo. Sad
Tunatakiwa tuzungumzie uwajibishwaji na watu wafunguliwe mashtaka nk. Sasa kuanza kutoa ushauri kwa watu wanaowauwa?
Ndio maana nimemshauri IGP amuondoe kabla ya kuleta hasara kubwa zaidi .Huyu jamaa nashaka hata na uwezo wake w akufikiri, sijuhi waandishi huwa wanamuelewa vipi? yani akiongea huwa anajichanganya sana, na anatumia nguvu na vitisho kuliko hoja.