Hebu tuache kushabikia porojo hao watu 120,000 Zenj ni almost 1/3 ya wazanzibari wote that translate into total vanishing of Island dwellers in just three to four years. Well na hiyo mpya yenye nafuu na ujiko i.e 60,000 deaths per yr ina maana watu wataisha zenj kwa malaria hata kabla ya 2015 au ndio muungwana anamaanisha utokomezaji. Na hii ya vyandarua milioni 100 du?????? Kama kweli kaka yetu aliyasema haya kazi ipo?????????? Huyu kweli ni mkulu?
I am proud I didn't give him my vote anyways.....................
Ahsante sana Nyambala kwa hili. Wanasiasa mara zote wanapenda kutoa takwimu za kuwafurahisha wananchi waonekane kuwa wanafanya kazi. Miradi mingi inafanyika kama zimamoto ili kujipatia popularity ya haraka itakayo wawezesha kuwadanganya wananchi baada ya miaka 5.
Takwimu za umoja wa mataifa zinaonyesha duniani, watu 250,000,000 huugua malaria kila mwaka. Na kati ya hawa vifo vinafikia 1,000,000. Kawa numba ya mkuu hapa ya Zanzibar kuwa 60,000 ya vifo zanzibar, ina maana kwa afrika pekee yenye watu takribani 922,000,000 basi vifo ambavyo vingetegemewa baada ya haya mafanikio ya zanzibar ni 55,322,000. Hizi sijui ni takwimu za wapi huyu muungwana anataka kuwa danganya wananchi.
Halafu jamaa anatudanganya kuwa Zanzibar malaria haijaisha kwa kuwa eti Bara haikushirikishwa. Mbu hawewezi kuvuka bahari kwa kuruka, na idadi ya mbu wanaobebwa na vyombo vya usafiri haiwezi kuwa tishio kubwa kiasi hicho. Tatizo angesema ni kwa nchi za mailand kama Kenya, Uganda Msumbiji n.k
Pili, misaada mingi haina mafanikio yadumuyo (not sustainable), kwa kuwa tatizo sio leo tuna njaa kwa hiyo tunahitaji chakula. Ila tufanye nini ili tuweze kujitafutia chakula. Ni aibu kuwa kila rais ajae atakuwa kazi yake ni kuzurura tu kuomba misaada, haitakuwepo siku zote. Sisi kama taifa tunatakiwa tujipange, ili tuone vyandarua na dawa za mbu pamoja na hospitali zinapatikana je. Wananchi wanahusishwa vipi kujiwezesha kumiliki vyandarua na kupulizia dawa bila kusubiri msaada wa Bush (huyu Nov ndio mwisho).
Tatu, Propaganda za siasa ziachwe katika mambo ya msingi. Kuwe na mkakati wa kuwaelimisha wananchi juu ya umaskini unaowakabili na wanatakiwa kushiriki vipi kupambana nao. Na serikali iwe tayari kuwapa watanzania furusa ya kujiletea maendeleo yao badala ya kuwa na mtizamo kuwa wazungu na wahindi ndio watakaoibadilisha nchi hii.
Kutokomeza Malaria inawezekana tu, pale tutakapotokomeza umaskini.