Mkuu Kwetu,
Hapo uko sawa kabisa. Nakumbuka siku tumeshushiwa Complex number na mwalimu Sambayuka pale TCA (Arusha), nilitoka kapa. Na hii huwa ni kawaida yangu kwani kwenye lectures huwa nafikiria vitu vingine kabisa kama sielewi. Tumemaliza tu nikaanza kucheka kuwa hizi namba ni madudu matupu. Jamaa mmoja aitwaye Misonge (na yes, alikuwa Misonge kweli kwani aliondoka na A zote - Ila nasikia aliacha UDSM) aliniambia "ahh mbona rahisi?" Nikamuuliza kama alikuwa anadanganya, akasema hapana, yeye kaelewa vizuri tu hata anaweza kwenda kufanya mtihani. Nikamwambia kama anaweza kunishushia hizo namba, akasema no problem. Masaa matatu baadaye nilikuwa nashusha na mimi Complex number.
Misonge, popote ulipo nasema asante kijana.....