beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri Ardhini (Latra) imetoa mwongozo wa namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona kwa wamiliki wa magari yanayosafirisha abiria na mizigo.
Mwongozo huo unaowalenga pia waendesha bodaboda na bajaji umetolewa leo Alhamisi Februari 25, 2021 na mkurugenzi mkuu wa Latra, Gilliard Ngewe akiwataka abiria kuzingatia mambo mbalimbali ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni wanapoingia na kutoka katika vituo vikuu vya mabasi na treni.
Ngewe amewataka abiria hao kufunika mdomo na pua wanapokohoa na kupiga chafya kwa kutumia sehemu ya ndani ya kiwiko cha mkono.
Pia amewataka abiria kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu wakati wa kusubiri usafiri vituoni.
“Kuvaa barakoa wakati wote unaposafiri na basi, daladala, treni, bodaboda au bajaji hasa pale unapohisi kuwa na dalili za corona ili kumlinda mwenzako na kutumia barakoa ambazo zimeidhinishwa na kupitia Wizara ya Afya ama za kitambaa cha kushona mwenyewe,” amesema Ngewe.
Amewataka waendesha teksi, bodaboda na bajaji kuhakikisha abiria wanapaka vitakasa mikono kabla ya kuwapakia kwenye vyombo vyao.
“Abiria waendelee kutumia njia za asili za kujikinga na maradhi kabla na baada na baada ya kutumia vyombo vya usafiri,” amesema.
Chanzo: Mwananchi