PostGE2025 Larry Madowo: Yaliyopo kwenye ripoti ya CNN ni machache kati ya mengi yaliyotokea, na yote tunaweza kuyathibitisha

PostGE2025 Larry Madowo: Yaliyopo kwenye ripoti ya CNN ni machache kati ya mengi yaliyotokea, na yote tunaweza kuyathibitisha

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
440
Reaction score
3,211
Mwandishi wa CNN Larry Madowo amesema pamoja na uwepo wa kampeni na jitihada kubwa za kufubaza ukweli zinazoendelea kwa siku mbili sasa kwenye mitandao ya kijamii tangu watoe ripoti yao ambayo ameiita ni sehemu ndogo tu ya uchunguzi wao, waliainisha mambo ambayo tu wanaweza kuyathibitisha.

Natoa rai kwa Serikali hii dhalimu, kama kawasingizia basi mshtakini ili tulipwe matrilioni ya dola kama yale ya makinikia ili kila mtanzania apate Noah, tukomeshe kabisa tabia ya vibaraka wa mabeberu kuingilia mambo yetu ya ndani

Vinginevyo hatutaki kusikia nywinywinywiiiii za kwamba CNN wamedanganya.

 
Watumishi wote wa serikali ni wapumbavu sana..haiwezekani unyama km huu wamefanyiwa ndugu zako, jirani, rafiki zako halafu wao wanabehave as if nothing happened..tanzanians need to change that behavior, ishi maisha halisi..kibaya ni kibaya bila kujali nani kafanya!
 
Angekuwa na uwezo huo angefanya hivyo.

Asingekuwa anatisha tisha watu.
 
Kituo cha habari cha CNN kimesisitiza kuwa ripoti yake kuhusu matukio ya Oktoba 29, 2025 nchini Tanzania imejengwa kikamilifu juu ya ushahidi likibainisha kuwa hakikuchapisha taarifa yoyote ambayo halikuweza kuithibitisha.

Akizungumza na SABC News, mwandishi wa habari wa CNN, Larry Madowo alisema uchunguzi wao ulifanywa kwa kutumia mahojiano na zaidi ya Watanzania 100, uchambuzi wa kitaalamu wa sauti, ulinganifu wa video, na picha za satelaiti ili kufuatilia matukio ya vurugu, vifo na madai ya makaburi ya pamoja.

“Tulifanya kazi kwa umakini mkubwa. Tulihakiki kila ushahidi tulioupata na hatukutohoa taarifa yoyote bila kuwa na uthibitisho wake. Tuliikagua kila video na kila sauti, na ushahidi unaonesha wazi kuwa raia wasiokuwa na silaha walipigwa risasi na polisi au watu waliokuwa na bunduki,” alisema.

Alisema hakuna mtu wala mamlaka yoyote iliyokanusha ukweli wa taarifa zao tangu ziwekwe hadharani: “Tangu tulipotangaza ripoti hii, hakuna yeyote aliyesema kuwa tulidanganya au tuliandika taarifa za uongo.”

Wakati CNN ikisema imetekeleza uchunguzi wa kina, Serikali ya Tanzania kupitia Msemaji Mkuu wake Gerson Msigwa imepinga ripoti hiyo, ikieleza kuwa ina makosa ya kiweledi na imeegemea upande mmoja.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma, Msigwa alisema uhakiki wa maudhui ya CNN unaendelea lakini akasisitiza kuwa shirika hilo “halikutoa nafasi sawa kwa upande wa serikali.” Amesema mwandishi wa CNN hakuwasiliana na mamlaka za Tanzania na alitumia picha za simu bila kuzingatia taratibu za kiweledi.

“Hawakufuata maadili. Uandishi wa habari unatakiwa kuwa wa pande zote. Hatusemei vifo vilivyotokea; sote tumesikitishwa. Lakini kwa nini kutengeneza maudhui yanayoongeza maumivu na hasira kwa wananchi?” Alihoji Msigwa na kuongeza,

“Ni kinyume cha maadili kuchapisha picha mbaya ambazo hazijathibitishwa ipasavyo. Tume imeundwa kuchunguza na itatoa ripoti. Tunatoa wito CNN waje upande wa serikali wasikilize, na wachapishe taarifa zenye uwiano na ukweli.”
1763970532262.png
 
Huyo jamaa akiona hata mkulima kapalilia shamba anasema kaburi la halaiki
 
Wanadhani watu wanafanya kazi kizembe kama wao, huku nje mambo ni tofauti sana. Msigwa mwenyewe anajua ukweli lakini hawezi kuusema sababu na yeye anaweza kupotezwa. Inaweekana hata cha kuongea kaandikiwa na walioamuru watu wauwawe. Ni huzuni kuona mpaka tunakataliwa na watu tuliosaidia kupigania uhuru - south africa. Maana yake tumerikoroga mno. Uchu wa madarka ni mbaya, cha ajabu mtu unapokufa hauendi na utajiri kaburini. Wale waliojari wengine ndo wanaopata dhawabu. Unaenda uchi na madhambi au wema wako mbele za Mungu. Tuwe makini sana na mambo ya kuuwa, kuteka na kunyanyasa raia, ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom