Laptop vyuoni, wanachuo huwa mnazitumiaje?!

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
8,458
10,930
Mdogo wangu aling'ang'ania anunuliwe Laptop nikamnunulia, sio kwasababu ya ujinga, hapana.ilikuwa kumridhisha na kwasababu ilikuwa ndani ya uwezo wangu.
Lakini nimekuwa nikimuuliza unaitumiaje?!My,Google, anasema vitu vingi tu, lakini miminimesema, nilikuwaanaandika, notes kwenye daftari na kujisomea vitabu library. Sikuwahi ona mahitaji ya Laptop. Sasa mnisaidie wenzangu, mliowahi kusoma vyuo, na wanafunzi wa leo, hizo laptop mnazitumiaje chuoni?!
Binafsi labda hata angeomba photocopier machine, maana naona ana toa copy sana kuliko hata kuandika.
Lakini kanunua laptop badala yake. Inatumikaje?!
 
Moodle site kuna time table na walimu wsnaweka lecturer notes pre lecture. Ukizipitia lecture unaielewa vizuri zaidi na unalienable umeshajenga maswali ya kuuliza kwa usichoelewa.
Hapa sisi ratiba hutolewa kwenye karatasi, hakuna module sites.
Sisi topic tunaikuta class tunaiacha huko. Hakuna module hapa, hayo mambo ya ulaya huko nasikia.
 
Mapinduzi ya kitechonologia Mkuu siku izi watu wanafundisha in digital style
Sometimes kuna kazi zinafanyika huko huko online sasa ili kua flexible kuzi-handle inahitaji computer mpakato

Pili nature tu ya usomaji wa chuo ni tofauti na level zingine za chini yake so computer haiepukiki ukiwa na uwezo wa kua nayo

Tatu namna ya uhifadhi wa notes chuo watu hawaendi na ma tranka Bali wanaenda na PC kwa sababu notes nyingi zinatolewa/zinapatikana ktk soft copy

So just relax mwache Dogo ale shule
 
Moodle site kuna time table na walimu wsnaweka lecturer notes pre lecture. Ukizipitia lecture unaielewa vizuri zaidi na unalienable umeshajenga maswali ya kuuliza kwa usichoelewa.
daaa umenikumbusha Moodle asee, hata baadh ya mithan hasa IT tulikua tunafanyia kule, Daaa enz hzo Nahonga mpk CW nusura ni disco
 
Kwa nilichoshuhudia Laptop chuoni 90% ya matumizi yake for non-IT students ni kwa ajili ya Entertainment tu (Streaming on youtube, watching or downloading Movies & Series)! Hizo asilimia zilizobakia ndio kuna kuandika proposal & report pia ku google assignments na kuzi edit kisha kwenda printing!
Kukweli Laptop ni gadget muhimu sana chuo, ina raha yake na usipokuwa nayo utanyanyasika sana na wenye nazo, takwimu zinaonesha asilimia 60% ya watoto wa kike wanagongwa ovyo kwa gia ya kuazimwa Laptop na mabazazi hivyo hujakosea kumnunulia huyo ndugu yako laptop hasa kama ni wa kike, umemuokoa ila kama ni wa kiume hakika hatotoka kapa ndani ya miaka yote atakayokuwepo chuoni, lazma apate mama!
 
Mabadiliko ni mengi sana kwa sasa tofauti na kipindi cha nyuma.
..
Zamani ilikua assignment nyingi mnaandika kwa mkono lakini kwa sasa assignment una type kwenye Laptop or desktop then una print unapata hardcopy unasubmit chap. Tena katika kusubmit inategemea na mwalimu kuna wengine wanataka submitting iwe online yan hakuna kupeleka hardcopy kwake.
..
Pia siku hizi mambo yamebadilika tofauti na zamani ratiba ya class unaipata online, notes za darasani, matangazo mbalimbali ya chuo yapo online siyo kila muda utaenda kwenye ubao wa matangazo, pia matokeo yanapatikana online though hayo pia yanaweza kufanyika ukiwa na smartphone lakini laptop ina umuhimu wake.
..
Yan kiujumla Laptop ina umuhimu mkubwa japo hata asipokuwa nayo hakuna kinacho haribika kwa sababu vipo vyuo vinakua na computer rooms(desk top) kwa ajili ya wale wanafunzi wasiokuwa na laptops.
 
Mkuu japo na mie sijahudhuria chuo ila nimeelimika.
Kazi nyingi za chuo wanatakiwa wazifanye kwenye laptop, akisema kila kazi apeleke steshenari gharama itakua kubwa vilevile convenience.

Pili huko wanasoma masomo ya kuhusu kompyuta, wengine kuzitumia kufanyia kazi na kuandaa mambo mbalimbali, wengine kuwa wahandisi wa mifumo ya kompyuta.

Pia kuna mifumo ya kuwasaidia hawa wanascola kufanya tafiti au kuwasaidia kutekeleza majukumu yao wakiwa chuo na watakapoajiriwa, mfano, mifumo ya kuchakata taarifa kuzalisha takwimu, mifumo ya kusaidia michoro ya kihandisi, n.k

Kumbuka kwamba kwa mambo yalivyopiga hatua, mtandao umekua chanzo muhimu cha upatikanaji wa taarifa na tafiti zinazowasaidia wanachuo kushiriki vizuri masomo yao.

Anaandaliwa kwenda kufanya kazi baada ya kuhitimu, huko ataenda kufanya kazi kwa kutumia kompyuta sio photocopy mashine. Enzi zimebadilika, mnunulie tu.
 
Kwa watu wa computer na IT laptop ni muhimu sana kwaajili ya programming, graphic n.k
Pili kwa wanafunzi wengine generally laptop hutumika kuchapa kazi kisha kwenda kuiprint stationery.
Kusoma pdf na softcopy nyingine utahitaji
Pia entertainment inahusika kwa hiyo pc muhimu Zaidi ya simu kwa sababu inafanya vitu vingi.
Pia kuna course nyingine zinzhitaji computer kwaajili ya practical ambazo zinasomwa na wote.
Though unaweza kuazima ila ni usumbufu.
 
Kwa nilichoshuhudia Laptop chuoni 90% ya matumizi yake for non-IT students ni kwa ajili ya Entertainment tu (Streaming on youtube, watching or downloading Movies & Series)! Hizo asilimia zilizobakia ndio kuna kuandika proposal & report pia ku google assignments na kuzi edit kisha kwenda printing!
Kukweli Laptop ni gadget muhimu sana chuo, ina raha yake na usipokuwa nayo utanyanyasika sana na wenye nazo, takwimu zinaonesha asilimia 60% ya watoto wa kike wanagongwa ovyo kwa gia ya kuazimwa Laptop na mabazazi hivyo hujakosea kumnunulia huyo ndugu yako laptop hasa kama ni wa kike, umemuokoa ila kama ni wa kiume hakika hatotoka kapa ndani ya miaka yote atakayokuwepo chuoni, lazma apate mama!
Umepitwa na wakati bro, this age aint no stone age!
 
Mdogo wangu aling'ang'ania anunuliwe Laptop nikamnunulia, sio kwasababu ya ujinga, hapana.ilikuwa kumridhisha na kwasababu ilikuwa ndani ya uwezo wangu.
Lakini nimekuwa nikimuuliza unaitumiaje?!My,Google, anasema vitu vingi tu, lakini miminimesema, nilikuwaanaandika, notes kwenye daftari na kujisomea vitabu library. Sikuwahi ona mahitaji ya Laptop. Sasa mnisaidie wenzangu, mliowahi kusoma vyuo, na wanafunzi wa leo, hizo laptop mnazitumiaje chuoni?!
Binafsi labda hata angeomba photocopier machine, maana naona ana toa copy sana kuliko hata kuandika.
Lakini kanunua laptop badala yake. Inatumikaje?!
Kwa iyo icho cha kuprint angekiandika na pen??
 
Kazi ya Laptop kwa wanafunzi wa chuo

1 Kuhifadhia notes - Mara nyingi lectures huwa kwenye Softcopy kwaiyo ukiwa na laptop inakusaidia kuhifadhi

2 Kujisomea - kazi nyingine kubwa kuliko zote ya laptop kwa mwanafunzi ni kujisomea hutokuwa na haja ya kukusanya mavitabu mengi na madesa mahand out

3 Kutayarishia kazi - kuna kazi kama za group assignment au individual utazifanya kwa wepesi sana kama ukiwa na laptop kuliko kwenda stationery kupanga foleni
 
Laptop zina umuhimu sana kwa wanachuo, huzitumia kwenye kujisomea notes hasa ambazo zinatolewa kwenye soft copy na kubwa zaidi kama mnapewa assignment na inabidi u-type kama huna laptop utakuwa unagongea mpaka mwenyew utajionea kero.
 
Ulisoma course gani ndugu na Chuo gani? Maana ninavyojua pale UDSM kama hauna laptop utabaki kuazima azima tu! Siku hizi kuna adi assignment zinazokusanywa online.
 
Mdogo wangu aling'ang'ania anunuliwe Laptop nikamnunulia, sio kwasababu ya ujinga, hapana.ilikuwa kumridhisha na kwasababu ilikuwa ndani ya uwezo wangu.
Lakini nimekuwa nikimuuliza unaitumiaje?!My,Google, anasema vitu vingi tu, lakini miminimesema, nilikuwaanaandika, notes kwenye daftari na kujisomea vitabu library. Sikuwahi ona mahitaji ya Laptop. Sasa mnisaidie wenzangu, mliowahi kusoma vyuo, na wanafunzi wa leo, hizo laptop mnazitumiaje chuoni?!
Binafsi labda hata angeomba photocopier machine, maana naona ana toa copy sana kuliko hata kuandika.
Lakini kanunua laptop badala yake. Inatumikaje?!
hapo mkuu unachekesha walionuna,,, wataka kusema PHOTOCOPIER ingewezaje kufanya kazi bila laptop?
 
Back
Top Bottom