Laptop vyuoni, wanachuo huwa mnazitumiaje?!

Laptop vyuoni, wanachuo huwa mnazitumiaje?!

Mapinduzi ya kitechonologia Mkuu siku izi watu wanafundisha in digital style
Sometimes kuna kazi zinafanyika huko huko online sasa ili kua flexible kuzi-handle inahitaji computer mpakato

Pili nature tu ya usomaji wa chuo ni tofauti na level zingine za chini yake so computer haiepukiki ukiwa na uwezo wa kua nayo

Tatu namna ya uhifadhi wa notes chuo watu hawaendi na ma tranka Bali wanaenda na PC kwa sababu notes nyingi zinatolewa/zinapatikana ktk soft copy

So just relax mwache Dogo ale shule
Lakini huyu mdogo wangu sikuwahi kusikia au kujua kama hata kasoma zile computer course za mitaani, nimeanza kumuona tu akibeba laptop, anaenda chuo nikajiuliza hivi anaitumiaje huko, na kufanya nini?!
 
  • Thanks
Reactions: a45
hapo mkuu unachekesha walionuna,,, wataka kusema PHOTOCOPIER ingewezaje kufanya kazi bila laptop?
Material yaleyale kila mwaka wanatoa photocopy tu, anayo mengi photocopy tupu. Ndio nikasema bora hata angenunua photocopier
 
Kwa nilichoshuhudia Laptop chuoni 90% ya matumizi yake for non-IT students ni kwa ajili ya Entertainment tu (Streaming on youtube, watching or downloading Movies & Series)! Hizo asilimia zilizobakia ndio kuna kuandika proposal & report pia ku google assignments na kuzi edit kisha kwenda printing!
Kukweli Laptop ni gadget muhimu sana chuo, ina raha yake na usipokuwa nayo utanyanyasika sana na wenye nazo, takwimu zinaonesha asilimia 60% ya watoto wa kike wanagongwa ovyo kwa gia ya kuazimwa Laptop na mabazazi hivyo hujakosea kumnunulia huyo ndugu yako laptop hasa kama ni wa kike, umemuokoa ila kama ni wa kiume hakika hatotoka kapa ndani ya miaka yote atakayokuwepo chuoni, lazma apate mama!
Hahaha ni wakike na hasomi IT, nami ndio nilijiuliza anaifantia nini, naona maphotocopy ya notes kibao. Labda entertainment huko you tube. Maana kusoma naona anasoma hayo ma copy muda mwingi.
 
Mkuu kwa courses za engineering na hata architecture... Unatakiwa sio tu uwe na laptop tu...

Unatakiwa uwe na laptop yenye viwango.

Huwezi kurun softwares like archicad, AutoCAD( Civil & Electrical ) , Adobe kwenye PC za ajabu ajabu.

Kuwa na PC sio mbaya... Ila anaweza akawa nayo inayolingana na matumizi yake.
 
Hahaha ni wakike na hasomi IT, nami ndio nilijiuliza anaifantia nini, naona maphotocopy ya notes kibao. Labda entertainment huko you tube. Maana kusoma naona anasoma hayo ma copy muda mwingi.
Yeah hio ni kwa ajili ya movie, hongera umemkomboa toka kwa vishawishi vya team fisi, wangemla kwa michongo ya laptop tu!
 
Lakini pia mkuu, ukweli ni kwamba hautaweza kula vitini muda wote... Sometimes utarefresh kwa kuangalia movies, music videos, au hata documentaries.

Bado umuhimu wa laptop upo sana aisee ukiachana na needs za academic.
 
Mdogo wangu aling'ang'ania anunuliwe Laptop nikamnunulia, sio kwasababu ya ujinga, hapana.ilikuwa kumridhisha na kwasababu ilikuwa ndani ya uwezo wangu.
Lakini nimekuwa nikimuuliza unaitumiaje?!My,Google, anasema vitu vingi tu, lakini miminimesema, nilikuwaanaandika, notes kwenye daftari na kujisomea vitabu library. Sikuwahi ona mahitaji ya Laptop. Sasa mnisaidie wenzangu, mliowahi kusoma vyuo, na wanafunzi wa leo, hizo laptop mnazitumiaje chuoni?!
Binafsi labda hata angeomba photocopier machine, maana naona ana toa copy sana kuliko hata kuandika.
Lakini kanunua laptop badala yake. Inatumikaje?!
Kama hasomi Computer and IT, kuwa na Laptop yake mwenyewe ni Ub - Shoooooooooooo wa kiwango cha SGR. By the way kila Chuo kinakuwa na mahitaji ya mwanafuzi, uliapata nafasi ya kusoma joining instruction yake ? Kama hapana, ichukue uisome uone kama PC ni miongoni mwa mahitaji.
 
Hasomi engineering wala IT, basi tu sielewi hata mimi.
 
ukiachana na mambo hayo ya chuo kwa hao waliyopitia, laptop ni basic bwana ni muhimu kuwa nayo sema ndo vile vile kibongo bongo inaonekana luxury
 
ukiachana na mambo hayo ya chuo kwa hao waliyopitia, laptop ni basic bwana ni muhimu kuwa nayo sema ndo vile vile kibongo bongo inaonekana luxury
Huo umuhimu ni upi sasa?!
 
Lakini huyu mdogo wangu sikuwahi kusikia au kujua kama hata kasoma zile computer course za mitaani, nimeanza kumuona tu akibeba laptop, anaenda chuo nikajiuliza hivi anaitumiaje huko, na kufanya nini?!
hata mimi najua kutumia laptop tho sijawahi kuhudhurua hizo classes

maIT wengi wakubwa hawajawahi kusomea computer
 
Hasomi engineering wala IT, basi tu sielewi hata mimi.
Haina shida, hiyo inatumika kama fashion tu, si unajua watoto siku hizi wanaenda na wakati bila kujali kuwa pesa inatakiwa kuelekezwa kwnye matumzi sahihi na kwa wakati sahihi. Hatahivyo, ni vizuri kuwa umemnunulia na kumwepusha na vishawishi maana angeweza kuitamani hadi kumwomba mtu amnunulie na kumwingiza kwenye majaribu.
 
Anaitumiua tu wala hata ucwaze wanaelekezana na pia kuna kuwaga na course za computer kwa baadhi ya vyuo we mpatie PC kwa roho moja mwache akale shule
Lakini huyu mdogo wangu sikuwahi kusikia au kujua kama hata kasoma zile computer course za mitaani, nimeanza kumuona tu akibeba laptop, anaenda chuo nikajiuliza hivi anaitumiaje huko, na kufanya nini?!
 
Pamoja na mengine mengi yaliyotajwa hapo juu pia unatoka chuoni matumizi ya kawaida yakutumia kompyuta utakuwa powa kama typing speed na mengine maana makazini pia utaenda kutumia kompyuta sio unatoka chuo huwezi kuandika chochote kupitia kompyuta maana kama hauna yako binafsi bila shaka hizo kazi zakutype utakuwa unawapa wenye nazo
 
Kwa karne hii ilivyo si kutegemea kukutana na swali dizaini hii kabisa! Laptop ni muhimu narudia tena Laptop ni muhimu!
 
Mdogo wangu aling'ang'ania anunuliwe Laptop nikamnunulia, sio kwasababu ya ujinga, hapana.ilikuwa kumridhisha na kwasababu ilikuwa ndani ya uwezo wangu.
Lakini nimekuwa nikimuuliza unaitumiaje?!My,Google, anasema vitu vingi tu, lakini miminimesema, nilikuwaanaandika, notes kwenye daftari na kujisomea vitabu library. Sikuwahi ona mahitaji ya Laptop. Sasa mnisaidie wenzangu, mliowahi kusoma vyuo, na wanafunzi wa leo, hizo laptop mnazitumiaje chuoni?!
Binafsi labda hata angeomba photocopier machine, maana naona ana toa copy sana kuliko hata kuandika.
Lakini kanunua laptop badala yake. Inatumikaje?!
Kuna ku-type assignments.... Kuweka notes za kusomea zilizo kwenye soft copy... Kuhifadhi documents nyingine muhimu n.k

Ina matumizi mengi sana tu
 
Anaitumiua tu wala hata ucwaze wanaelekezana na pia kuna kuwaga na course za computer kwa baadhi ya vyuo we mpatie PC kwa roho moja mwache akale shule
Anayo tayari, ila sikujua kama kuna uhitaji wa laptop chuo ndio maana nikaona niulize, ni siku nyingi nimetoka chuo hatukuwahi kutumia laptop.
 
  • Thanks
Reactions: a45
Back
Top Bottom