LAPF hawaaminiki. Tushtuke

Hivi kuna haja ya kuwaamini hawa LAPF

  • Hapana

    Votes: 3 60.0%
  • Ndiyo

    Votes: 3 60.0%

  • Total voters
    5

Ishimba

Member
May 19, 2017
21
75
LAPF wanaweza kuharakisha vifo vyetu

Uwiii, sasa wanachama wanaweza kuliwa hivihivi na hawa jamaa wa LAPF.

Yaani nimekutana na hili gazeti na kulisoma kwa umakini mkubwa, nimegundua kuwa LAPF wanaweza kutuua mapema, yaani pesa zetu wanazowekeza zinadorora, kwamba hazizalishi faida inayotarajiwa?

Kama ndiyo hivyo, nani sasa tumwamini atunze mafao yetu?

Hawa jamaa wamewekeza kwenye majengo ambayo sasa hayaleti pesa.

Jamani jamani, wakati wa kuamka ni sasa.
 

Attachments

Nsuri

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
1,015
2,000
Sidhani kama ni LAPF wa kulaumiwa ila biashara haifanyi vizuri sasa. Hakuna biashara mpya, wafanyabiashara wengi wanafunga biashara,cjui tatizo nini?Je umefikiria hii mifuko mingine itakuwa na wakati gani serikali ikimaliza kuhamia Dodoma?nani atapanga majengo yao yaliyopo dar?Subiri tuu utasikia mengi
 

Ishimba

Member
May 19, 2017
21
75
Sidhani kama ni LAPF wa kulaumiwa ila biashara haifanyi vizuri sasa. Hakuna biashara mpya, wafanyabiashara wengi wanafunga biashara,cjui tatizo nini?Je umefikiria hii mifuko mingine itakuwa na wakati gani serikali ikimaliza kuhamia Dodoma?nani atapanga majengo yao yaliyopo dar?Subiri tuu utasikia mengi
Imani yangu ni kwamba, hawa jamaa hawajajipanga kuyaona haya. Mfuko mmoja, ambao kwenye research yangu unaonekana kujipanga ni PSPF, wao wameweka structures na mfumo ambao utawahakikishia uwekezaji wao haupotea na hautetereki kirahisi. Nitarejea kuweka zaidi, maana hapa sikumbuki haraka
 

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
144
250
Wajameni,

Sio mara moja wala mbili, nimewatahadharisha juu ya hawa LAPF, ni walaghai mno, nimegundua madudu yao meengii na wanashindwa kabisa kujipanga kutumia fedha za wanachama wao.

Nimeshuhudia walivyokuwa wakiwasumbua wateja wao kuwalipa mafao na hata wahudumu wao sio wastaarabu, wanatuona sisi wanachama kama wajinga.

Wanasikitisha sana

Siwawataki hata robo. Hawafaiiiiiiii
 

Nemesis

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
4,685
2,000
Yaani kukosa wateja kwenye jengo ndiyo LAPF isiaminike? Mbona kuna majengo mengi tu ya NSSF yaliyokosa wapangaji.

Kuna jambo moja hulijui LAPF ni mfuko unaosimamiwa moja kwa moja na TALGWU ambacho ni chama huru cha wafanyakazi. Tofauti na hiyo mifuko mingine ambayo ni ya Serikali moja kwa moja.

Kwa mfano walimu wengi wapo PSPF lakini CWT haina usemi pale PSPF. Waandishi na wachambuzi angalieni msije tumiwa vibaya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom