Langa Aongelea Uteja Wake

Navoyne

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
874
373

Msanii Langa ameelezea jinsialiyokuwa mteja kwa kipindi cha zaidi ya miaka 6 , ambapo uteja ulimradhimu kukimbia nyumbani,kuwa mwizi (kibaka) mtaani na pamoja na kuishi ghetto.
Langa aliongea hayo kupitia online show ya Cheusi Dawa TV inayoongozwa na Fid Q,ni wakati sasa jamii kujua kwamba madawa yapo na yanaharibu vijana.

<span style="font-family:century gothic;"><span style="color:#0000cd;">
 
Last edited by a moderator:
duuh inasikitisha sana! Mungu amfungue kutoka kwenye hayo makamba kwajina la Yesu!
 
yaani jinsi huyu dogo
alivyokuwa smart
mpaka kuwa teja kibaka
inasikitisha mno...
 
Huyu jamaa alikua anasoma CBE dodoma kila mara ukikutana nae kwenye korido anatembea anadunda ka mpira wa kitenesi na kuchana mistari, ukikutana nae usiku sasa anaimba ragga tena kwa sauti ya juu huku akiwa anatembea barabarani, mkute ashapiga mambo yake sasa...ndo kama zezeta. Kuna wakat mapolisi walimuwekea mtego alikuwa na shoo ukumbi wa Royal village (wellcome fleshers) wakamuona anapanda tax tokea CBE kuelekea kufata dawa maeneo ya mlezi wakamnasa ila aliwatoa ngawira wakamuacha. Kifupi unga ulimuharibu sana
 
Mara ya mwisho nilimuona pale container regency hakuwa katika hali ya kawaida kabisa aisee
 
Kwani hata kwenye nyimbo zake si alikuwa akisifia mihadarati,SIKILIZA WIMBO WA MATAWI YA JUU,wakishapata umaarufu tu wanawehuka......
Msanii Langa ameelezea jinsialiyokuwa mteja kwa kipindi cha zaidi ya miaka 6 , ambapo uteja ulimradhimu kukimbia nyumabani,kuwa mwizi (kibaka) mtaani na pamoja na kuishi ghetto.Langa aliongea hayo kupitia online show ya Cheusi Dawa TV inayoongozwa na Fid Q,ni wakati sasa jamii kujua kwamba madawa yapo na yanaharibu vijana.
 
Last edited by a moderator:
This should be inspiring to our youth, wajifuze unga sio mpango!, he still sound smart aint sure kama kweli kaacha, coz if so why is he still calling himself 'rais wa mateja'
Also BIG UP to FID Q, kwa kumtafuta dogo na kumrudisha kwenye ramani.....ups & downs happens its only few that can understand
 
Inauma sana, nampongeza kwa kuwa jasiri kuelezea ukweli.LANGA ni mtoto wa kishua na nakumbuka aligombona na wazazi wake alikuwa hataki shule akaamua kuhama kwao mara ya mwisho nilimsikia anasoma CBE.Huko darasani haonekani,asignment watu wanamfanyia natumaini atakuwa mfano mzuri kwa vijana wengine.Hongera FIDQ kwa project yako
 
Eeee MUNGU wa Mbinguni nakuomba wahurumie hawa watoto wetu waache hii tabia ya kutumia madawa ya kulevya, MUNGU nakuomba usikie kuomba kwangu.
 
Kwa kweli dogo ni mkali na kwa nguvu ya Mungu tunamuombea aachane na madawa if hajaacha bado. Na kwa hakija Mungu atamsaidia
 
Hawezi kuacha kwa hali aliyofikia! Labda kwa msaada wa wafadhili kutoka nje. Kama huamini nenda pale Mikocheni A karibu na kanisa la TAG Samaria Church, kwenye soko kongwe na maarufu kama Gezaulole! Hapo ndipo anapolala uwani peupeee! Baada ya kutimuliwa na msamaria aliyekuwa akimsitiri chumbani mwake. Baadhi ya wasanii nguli wanachangia kuwa hivyo alivyo kwani huwa wanakuja hapo kinyemela na kumjulia hali na kumpatia vijihela kidogo naye huendeleza libeneke lake. Hali ya huyu dogo imekuwa mbaya nasema mbaya kama ninavyomjua kwa yakini. Na hii ni changamoto kwa wasanii wote wa kada zote katika sanaa kujikusanya na kuweka mkazo ktk suala la maslahi na ushirikiano wa dhati ili inapotokea mmoja wao amepata mushkeli ktk jema na baya waweze kusaidiana ktk msingi wa tatizo badala ya kumtembelea mwenzao na kumuachia vijihela bila kudili na mzizi wa tatizo alilonalo.
 
jamani maisha haya....kwani hana wazazi huyu kijana jamani wajaribu kumsitiri mtoto wao!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom